Chuki, Majivuno, Ubinafsi unavyomtawala mtu

Chuki, Majivuno, Ubinafsi unavyomtawala mtu

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Hey! kwa wote wa humu ndani ya mmu

Nimefurahi tena kuwepo nanyi kwa muda huu kwani kipindi cha juzi kati nilipatwa na msiba ambao ulinifanya niwe
na huzuni kwa kuondokewa na kipenzi changu. Nashukuru sana kwa faraja zenu wanajamvi wenzangu na kunitia moyo na kunipa ahueni tena kurejea jamvini kwa mada motomoto kama ya leo.

Leo tena nimeona niingie na kitu hicho hapo juu ya wanadamu ambao mioyoni mwao mumejaa husuda, chuki, majivuno na ubinafsi uliokithiri sana.

Kwanini leo nimeona niseme jambo hili hapa ni kutokana na tabia hii iliyokithiri miongoni mwa watu ambao wamependa kujilimbikizia mali na utajiri pasipo kuwatambua na kuwaona wengine kuwa nao ni wahitaji.

Mara nyingi wale wenye kupenda fedha, mali, ama utajiri hawangalii wenzao wamebaki na ule umimi, Ninaowazungumzia hapa ni wale ambao wako katika nyadhifa za juu katika fani mbalimbali, sitaki kusema unyadhifa gani bali mwenye kuona, kusikia ataelewa kinachozungumziwa hapa.

Wengi wao wana majivuno yasiyoneneka na wanajiona kuwa wamewin hawaangalii wengine, ni nafsi zao tu, kwanini ninasema haya hapa? Nimeona kwa macho yangu mwenyewe jinsi nchi yetu ilivyoporomoka kwa umaskini uliokivuka mipaka.

Hata raia wa kawaida kwake chakula imekuwa ni ndoto za abunuasi kwake mlo ni mmoja kwa siku, na wengine mikoani wanakufa kwa njaa kwani hata mlo mmoja hawauoni. Jamani tunakwenda wapi sasa.

Hata katika familia upendeleo na majivuno na ubinafisi, chuki vinakuja kwa wazazi kupendelea mtoto yule anayeonekana anavyo ndio wanampetipeti, wengine wamediriki hata kuonesha wazi upendo wao kwa mtoto mmoja na kubagua wengine hiyo yote ni ubinafsi tu .

Hebu tuangalie kwa ufupi katika maandiko; Tunaona Isaka na Rebecca walivyokuwa wakiishi kwa na watoto wao Esau na Yakobo, Esau alipendwa na baba yake, na Yakobo alipendwa na mama yake, upendeleo wa mgawanyo wa vitu pale home ulionekana wazi kwani Esau yeye alikuwa mwindaji wanyama na yakobo alikuwa anakaa na mama yake home, Tunaona chuki ilivyoingia ndani ya ile nyumba na upendeleo kujengeka waziwazi bila kificho.

Kwanini nimesema chuki iliingia kwao, ni kutokana na kipindi kile ambaacho babayao Isaka alivyozeeka na kutaka kuwarithisha urithi wanawe, yeye alitaka kumrithisha esau lakini mama yake aliposikia na kwa ivile alipenda yakobo mwanae akajenga chuki kwa mwanawe wa kwanza esau na kumfanya yakobo apokee ule urithia ambao ni wa mtoto wa kwanza. upendeleo na chuki vilifanya wale watoto watake kuuana na ndipo yakobo alikimbia kwao. Hiyo ni habari ndogo tu ambayo inaonesha jinsi CHUKI, UBINAFSI, NA MAJIVUNO ambavyo vinaweza kusababisha matabaka kati ya mtu na mtu au nchi au nchi.

Hata leo CHUKI, UBINAFSI vimeleta maangamizi makubwa kwa mataifa mbalimbali wengine, wanagombea ardhi, wengine uchumi, na wengine hata kuuana ilimradi tu apate alichokuwa anakihitaji kwa wakati huo.

Wapendwa wenzangu hebu tufikie hatua ya kukataa kujijenga katika hali hizi kwani zinaleta maafa kwa Taifa letu, familia zetu na hata wewe mwenyewe binafsi, kataa hali ya kumchukia mwenzio kwa kuona yeye ameendelea, au amefanikiwa, kataa hali ya ubinafsi kwa kujipendelea wewe mwenyewe pasipo kuwatanguliza wengine, kataa hali ya majivuno kwa kujiona kuwa wewe ni wewe wengine ni takataka tu mbele zako.

Mungu hapendi kabisa tabia hizo na anasema atakutapika soma Ufunuo 21:1- utaelewa vyema, HEBU TUWE NA UPENDO WA KWELI NDANI YETU TUTAWEZA KUSHINDA VIKWAZO HIVI VYA ULE UMIMI (UBINAFSI) CHUKI NA HASIRA AMBAYO HULETA KIFO, NA MAJIVUNO NA DHARAU KWA WENGINE. ONDOKANA NAVYO VISIKUTAWALE ILA WEWE UVISHINDE

Be blessed
 
Be nice to people as you go up
You may meet them as you go down.
::
 
Back
Top Bottom