Christopher Mariba, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga na mwenzake, watuhumiwa kuomba na kupokea rushwa, wasimamishwa kazi

Huyu Mariba sina uhakika anatokea wapi. Lkn huyu msaidizi wake NJAU atakua mnyasa huyu. Wanyasa wana sifa ya kupenda sana nyama na pombe. Bila pesa hivi vitu Nyama na pombe huvipati. Ndio maana wakunyumba NJAU alijitosa akidhani anajiongesa.
NJAU hakusikia kwamba kuanzia leo hakuna kumpelekea mahabusu chakula. Inamaana hata masingasinga na waturuki watakua wanakula kama wengine
 
TAKUKURU KWA NIA YA DHATI KABSA NAOMBA MTUSAIDIE KUUDHIBITI MPAKA WETU WA SIRARI DHIDI YA MAAFISA WA TRA WASIO WAADILIFU.
TRA WANAPOKEA RUSHWA SANA. WANA ZILE GARI ZAO WAKISHA FAHAMU KUNA DILI LA KUVUSHA MIZIGO WANAOMBA CHAO MAPEMA ALAFU WANAONDOKA ENEO LA TUKIO KWA KUMPIMIA MWENYE MCHONGO MUDA WA KUVUSHA.

WANA MTINDO WA KUFICHA GARI VICHOCHORONI NA KUWAITA WENYE MIZIGO ILI KUMALIZANA NAO.

TRA MPAKANI SIRARI WAMEISHIA KUWAKATA BODABODA WABEBA SIMENTI NA SUKARI HUKU WAKIRUHUSU WENYE MIZIGO KUIVUSHA KUTOKA KENYA.

TAKUKURU MULIKENI HAWA TRA MPAKA WA SIRARI,TARIME.
 
KUNA CLIP ZIPO YOUTUBE KUPITIA TANZANITE TV ZINAONGELEA MADUDU YA TRA,,, UKISIKILIZA UTATAMANI TRA YOTE IBOMOLEWE KUANZIA MKUU WA TRA HADI MFAGIAJI.
TAKUKURU KWA NIA YA DHATI KABSA NAOMBA MTUSAIDIE KUUDHIBITI MPAKA WETU WA SIRARI DHIDI YA MAAFISA WA TRA WASIO WAADILIFU.
TRA WANAPOKEA RUSHWA SANA. WANA ZILE GARI ZAO WAKISHA FAHAMU KUNA DILI LA KUVUSHA MIZIGO WANAOMBA CHAO MAPEMA ALAFU WANAONDOKA ENEO LA TUKIO KWA KUMPIMIA MWENYE MCHONGO MUDA WA KUVUSHA.

WANA MTINDO WA KUFICHA GARI VICHOCHORONI NA KUWAITA WENYE MIZIGO ILI KUMALIZANA NAO.

TRA MPAKANI SIRARI WAMEISHIA KUWAKATA BODABODA WABEBA SIMENTI NA SUKARI HUKU WAKIRUHUSU WENYE MIZIGO KUIVUSHA KUTOKA KENYA.

TAKUKURU MULIKENI HAWA TRA MPAKA WA SIRARI,TARIME.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO WA HABARI

IMETOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM
MACHI 20, 2020

WATUMISHI WAWILI WA TAKUKURU
WASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa — TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma kwamba, watumishi wake wawili akiwemo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, wamesimamishwa kazi kuanzia leo Machi 20, 2020 ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

Hatua hii imefikiwa leo baada ya watumishi hao:
Christopher Mariba — Aliyekuwa Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga na Hilton Njau — Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Tanga, kuhusishwa na tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa na TAKUKURU.

Kosa hili ni kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia naKupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu Waandishi wa Habari,Kama ambavyo nimekuwa nikiuleza umma mara kwa mara, chombo hiki ndicho chenye dhamana ya kuongoza mapambano dhidi ya rushwa nchini — jukumu ambalo tumepewa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007.

Kwa msingi huo, watumishi wa TAKUKURU wanapaswa kuwa na uadilifu na weledi wa hali ya juu wakati wote wanapotekeleza majukumu haya nyeti kwa mustakabali wa maendeo na ustawi wa Taifa letu.

Ndugu Waandishi wa Habari,Ili kuhakikisha kuwa chombo hiki hakichafuliwi, ipo SERA ya ndani ya chombo hiki YA KUTOMVUMILIA MTUMISHI YEYOTE ANAYETUHUMIWA KUJIHUSISHA NA VITENDO WA RUSHWA. Hivyo basi, kwa msingi huo, watumishi hawa wamesimamishwa kazi kuanzia leo Machi 20, 2020 ili kupisha uchunguzi dhidi yao na uchunguzi huo utakapokamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.

Wakati uchunguzi huu ukiendelea, nimemteua Dkt Sharifa Bungala kukaimu nafasi ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tanga kuanzia leo Machi
20, 2020.

BRIG. JEN JOHN BUNGO (ndc)
KAIMU MKURUGENZI MKUU - TAKUKURU
Safi sana,tunatumia mbinu za kinyerere
Huwezi kudaka watu wazito kama hao,bila ya kutumia mtego wa kwa wao kufuatiliana
Kama kawaida NJAU yumo,dah!
 
Mbona hicho kiasi walichoomba na kupokea kama rushwa hakijatajwa kama ilivyo ada?
 
Tuliowapa dhamana ya kupambana na kuzuia rushwa ndo wala rushwa...so sad
Yaani Tanga pale pameoza kwa rushwa Masikini wanaonewa sana na watu wenye vijicent ,hata wakienda kushitaki kwenye mamlaka husika bado watazungushwa sana maana unakuta tajiri kesha toa rushwa alafu wwe unapigwa danadana,Mungu kwa kweli inabidi aingilie kati masikini wapate haki zao bila kuzungushwa!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom