Christmas 2016: Shamrashamra hakuna

jsenyinah

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
249
339
Heri ya sikukuu ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo,mwokozi wa maisha yetu.

Awali ya yote, napenda kumshukuru Mungu wangu, mwingi wa rehema kwa kuiona siku hii adhimu ya Krismasi.

Krismass ya leo mwaka 2016 imekuja kipindi ambacho waTZ wakiwa kwenye malalamiko, manung'uniko, hasira, gadhabu, stress na ufinyu wa pesa mifukoni, kwa kile kinachoaminika 'Rais amekaza uzi'.

Si hicho tu, bali ni tumbua tumbua iliyofanywa na Mh Rais kwa viongozi wenye dhamana ambao wakionekana kutumia vibaya madaraka yao,kiasi cha mkate kuliwa na walio wachache, wenye visu vikali!

Shamrashamra hakuna uku mtaani kama huko nyuma.Mwezi ujao n mwezi dume, mwezi wa kodi, ada za watoto, malengo mapya nk.Fujo hakuna, mbwembwe hakuna, wengi wapo majumbani na famila zao wakisubiri kung'ata kidogo kilichopatikana kwa ajili ya siku ya leo.

Hata kwa wale wenzetu wachaga, jum za magari zimekuwa tofauti (chache) kwa wiki hii yote tofauti na miaka ya nyuma. Wengi wao wamelazimisha safari zao kwa kile kinacjoelezwa 'kwenda kihesabiwa'.

TUNAJIFUNZA NINI?

Tukubali system iliyopo.Tusibeze dhamira za wakubwa zetu. Tuwasupport.

Asante mama Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
FB_IMG_1467814957248.jpg

swissme
 
Mleta mada ni fisadi mkubwa aliyebanwa.

Sasa alichobakiza ni kutangaza majungu kila siku,
Kwanza alitangaza mabasi ubungo yamekosa abiria lkn mwishowe akaambulia Aibu.

Pili akatangaza Jangwani breeze hamna watu pia mwishoni ameambulia aibu.

Utaaibika mpaka ukome,
Shetani yuko upande wako fisadi mkubwa wewe.
 
Daaaaaah me mwenywe hapa home naona pamekauka balaa hata sioni majirani kuja soda kununuliwa yani papo papo tuuu wakati sio kawaida yake daaaaaaah
 
Heri ya sikukuu ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo,mwokozi wa maisha yetu.

Awali ya yote, napenda kumshukuru Mungu wangu, mwingi wa rehema kwa kuiona siku hii adhimu ya Krismasi.

Krismass ya leo mwaka 2016 imekuja kipindi ambacho waTZ wakiwa kwenye malalamiko, manung'uniko, hasira, gadhabu, stress na ufinyu wa pesa mifukoni, kwa kile kinachoaminika 'Rais amekaza uzi'.

Si hicho tu, bali ni tumbua tumbua iliyofanywa na Mh Rais kwa viongozi wenye dhamana ambao wakionekana kutumia vibaya madaraka yao,kiasi cha mkate kuliwa na walio wachache, wenye visu vikali!

Shamrashamra hakuna uku mtaani kama huko nyuma.Mwezi ujao n mwezi dume, mwezi wa kodi, ada za watoto, malengo mapya nk.Fujo hakuna, mbwembwe hakuna, wengi wapo majumbani na famila zao wakisubiri kung'ata kidogo kilichopatikana kwa ajili ya siku ya leo.

Hata kwa wale wenzetu wachaga, jum za magari zimekuwa tofauti (chache) kwa wiki hii yote tofauti na miaka ya nyuma. Wengi wao wamelazimisha safari zao kwa kile kinacjoelezwa 'kwenda kihesabiwa'.

TUNAJIFUNZA NINI?

Tukubali system iliyopo.Tusibeze dhamira za wakubwa zetu. Tuwasupport.

Asante mama Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Kama hakuna kwako pole, vumilia. Hayo ndio maisha.
Mimi na familia yangu tunasheherekea kama mwaka jana, juzi nk.
 
Haya ndio maisha yetu halisi,
ile awamu iliyopita tulikua tunaishi maisha fake..
Maisha hewa hewa tu,kila kitu kilikuwa hewa tu....
 
Back
Top Bottom