Choo cha Mlimani City Kinyaaaa...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Sina hakika na aina ya Mktaba ulioingiwa katika ujenzi wa jengo la Mlimani city Mall sijui ni Design Bulid and Operate (DBO), Turnkey au lah. Lakini kwa ujumla hadhi na hali ya Jengo zima la Mlimani City haliwezi kufika miaka 50 ambayo inadaiwa kuwa ndio ya mkabata wa "ku-manage" ile Mall kati ya Chuo Kikuu na wabia katika Uwekezaji.

Miongoni mwa maeneo ambayo yanatia kichefuchefu ni sehemu ya haja, hii picha ni maliwato ya kiume (Gentles Toilet). Huko kuna harufu nzito na kali balaa anayo imechanganyika na joto kali sana kutoka nyuma ambako kuna jiko la mmiliki wa Samakisamaki (Fish Fish). Kwa ujumla kama ilivyio tabia za watanzania za kutiojali, ila kwa pale tumeliwa tena! Inaonekana sehemu nyingi zimejengwa kwa materials cheap na hazidumu kabisa. Choo hiki kichafu kulikovya baa za uswahilini!!.


MLIMANI CITY.jpg DSC01131.JPG
 
KHAAAAAAAAA. MAMA WEEEEEE..PESA WANAPELEKA WAPI? fukuzeni director..kazi yake ni nini?vyombo vya habari mmelala?
 
mweh! nimeshindwa kula..

MKuu lile ndo eneo la mashalo -B wa Bongo sijui wanakulaje pale samaki katika hali hii!! Hakika Bongoz mambo uvumilivu, mtu unaumia kwa hela yako. Pale Samakisamaki kuna menyu moja ya fish inafika mpaka 65,000Tshs. lakini kuboresha mazingira pale ni zero!!.
 
MKuu lile ndo eneo la mashalo -B wa Bongo sijui wanakulaje pale samaki katika hali hii!! Hakika Bongoz mambo uvumilivu, mtu unaumia kwa hela yako. Pale Samakisamaki kuna menyu moja ya fish inafika mpaka 65,000Tshs. lakini kuboresha mazingira pale ni zero!!.
wanashindwa kumlipa mtu kila siku tsh 10.000 asafishe?ningekuwa mmiliki nafukuza wote madirector
pumbafuuuuuuu
 
Haya ndio matokeo ya kukosa upeo (foresight) katika fani nzima ya maendeleo ya elimu ya juu.
Leo eneo la Mlimani Campus linageuzwa kuwa sehemu ya makunywaji na mambo yasiyo husu maendeleo ya elimu ya juu, na kuishia kuingizwa mkenge.
Ni jambo la kushangaza sana kuwa eneo hili la Mlimani kugeuzwa kuwa sehemu ya biashara badala ya kuendelezwa kwa kujenga miundombinu zaidi ya shule tofauti za Chuo Kikuu na Taasisi za utafiti.
Kwa bahati nzuri mimi nimesoma Uingereza miaka kadhaa iliyopita na najua jinsi utafiti wa kisayanzi unavyoweza kuhitaji miundombinu na nafasi ya kutosha.

Katika chuo nilichokuwa Uingereza palikuwepo na nafasi ya eneo la kutosha kufundishia wanafunzi kuendesha /kusimamia na kutengeneza mitambo in real time.
Kwa wale wanaofanya utafiti wa kutengeneza mitambo inayaruka kama ndege vile vile kulikuwepo na kiwanja kidogo.
Kwa wale wanaofanya utafiti wa mitambo ya majini kulikuwepo na bwawa kubwa sana na lenye kina.
Hata wale waliokuwa wakifanya tafiti za tabia za kibinadamu kulikuwepo na eneo kubwa tena sana tu kwa tafiti hizo.
Najua kuwa kuna maProfesa pale Mlimani ambao wamepitia chuo hiki na vyuo vingine vinavyo lingana na hicho.

Sasa nasikitika sana kuona sehemu ya taaluma inageuzwa kuwa Pombe shop.
Kwa hili in less than 50years waTanzania watawadai na kuuliza hivi upeo wenu wa kusoma sana uliishia wapi.
 
Asante mkuu kwa kuliweka wazi mie nilikuwa najiuliza hili jengo kwa muonekano huo wa maliwatoni ni kama lina miaka 20 tayari
anyway labda watafanya matengenezo kiukweli inatia kinyaa
 
Choo cha pale samaki samaki ndio kero kabisa! Ukiingia kuna joto na harufu kali sana! Utafikiri upo jehanam!
Inamaana mwekezaji wa pale samaki samaki hawez kufunga AC kwenye kale kachoo???
 
Oooh boy! yani sasa bado vyoo vya kike, kweli ni too much! joto la haja na harufu kaliii, tissue zimeisha mara choo hakiflashi halafu maji hayatoki kwenye sinki kunawa mikono baada ya kujisaidia...kazi kweli kweli!!..magonjwa nje nje

Bora umeweka hiyo picha wajionee wahusika..
 
Tulikuwa na mabwana afya, naona siku hizi kazi yao ni kufungia mama ntilie tu... sheria hazifuatwi kabisaa pahala pengi katika nchi yetu, maana kama zingelifuatwa na hali hiyo ya utata kuthibitishwa, hakika thread hii ingelisababisha jengo lifungwe mara moja kwa kukiuka kanuni za afya bora!!
 
Back
Top Bottom