GE2025 Chongolo amkimbiza Deo Sanga kura za Maoni ubunge Jimbo la Makambako ameongoza kata zote 12

GE2025 Chongolo amkimbiza Deo Sanga kura za Maoni ubunge Jimbo la Makambako ameongoza kata zote 12

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, anaongoza kwa tofauti kubwa katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Makambako mkoani Njombe. Katika kinyang’anyiro hicho kilichowakutanisha wagombea wawili pekee – Daniel Chongolo na mbunge aliyemaliza muda wake Deo Sanga (Jah People) matokeo ya awali yanaashiria mwelekeo mpya wa kisiasa katika jimbo hilo.

Chongolo ameendelea kujizolea kura nyingi katika kata mbalimbali, huku taarifa zikionesha kwamba hadi kufikia jioni ya leo ameshinda katika kata 10 kati ya 12, zikiwemo Kivavi, Majengo, Kitisi, Utengule, Makambako, Mwembetogwa, Mjimwema, Lyamkena, Mahongole na Mlowa. Katika kata ya Kivavi, Chongolo alipata kura 985 dhidi ya 35 za Deo Sanga.

Majengo aliongoza kwa 289 dhidi ya 13, na Kitisi akapata 376 huku Sanga akipata 68. Vilevile, kata ya Utengule ilimpa Chongolo kura 605 dhidi ya 45, Makambako alipata 574 dhidi ya 26, Mwembetogwa 175 dhidi ya 16, Mjimwema 318 dhidi ya 26, Lyamkena 319 dhidi ya 19, Mahongole 761 dhidi ya 74, na Mlowa 731 dhidi ya 13. Kata mbili pekee- Kitandililo na Maguvani ndizo bado hazijatoa matokeo yao wakati wa kuchapisha habari hii, lakini kwa mwelekeo wa kura unaoendelea, nafasi ya Chongolo kupewa ridhaa ya chama inaonekana kuwa na nguvu kubwa.

Chongolo, ambaye aliwahi pia kuwa Katibu Mkuu wa CCM kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, amekuwa akijinadi kwa ujumbe wa mabadiliko, kuimarisha huduma za kijamii na kusimamia maendeleo ya miundombinu katika jimbo la Makambako, ambalo linachukuliwa kama lango muhimu la kiuchumi kati ya mikoa ya kusini mwa Tanzania.
1000524213.jpg

IMG_20250804_200607_200.jpg
 
Jah People pamoja na kujipendekeza kote kule! Wanamtandao wameamua kumpiga chini.
 
Jah People pamoja na kujipendekeza kote kule! Wanamtandao wameamua kumpiga chini.
Wanamtandao wakiongozwa na " the king maker" Rostam Azizi wapo tayar kwa lolote . Hata magufuli alinyoosha mikono na kumwita lowasa na Rostam lumumba
 
Huyo sanga alikosea nini watu mbona kachinjwa hivyo
 
Back
Top Bottom