Chonde chonde wabunge wa mkoa wa Kagera

Chonde chonde wabunge wa mkoa wa Kagera

Mkoa wa Kagera na hasahasa wilaya ya Bukoba vijijini ina matatizo makubwa ya maji, mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa michache sana Tanzania ambayo wananchi wanagombea maji na mifugo,katika karne hii kukosa maji ya bomba au Kisima ni aibu.

Katika vijiji vya wilaya ya Bukoba vijijini, Nkenge na Muleba maji usombwa na bodaboda na ndoo ni mpaka sh 700.

Najua mkoa huu una wabunge japo ni aina ya Wabunge ambao kwao ni Dar Es Salaam, hawajui matatizo na mahitaji halisi ya majimboni mwao, na ndio maana michango yao ni kuulizia viwanja vya ndege so and so kitajengwa lini etc.

Nilitegemea katika bajeti ya wizara ya maji wabunge hao wapigie sana kelele na kuondoa mashilingi kuhusu suala la maji majimboni mwao, lakini as usual walikuwa kimya tu na kuachia wengine wa mikoa mingine na ambao wengi wao wana maji tayari wakiongezewa mitandao ya maji majimboni mwao.

Honestly kama by 2015 hakuna maji ya uhakika na salama katika mkoa wa Kagera especially wilaya za Bukoba vijijini na Muleba, Nkenge basi ni bora waheshimiwa wetu msichukue fomu kabisa kwani hata mimi nitatumia hela yangu kufanya malicious campaign.

Ngoja mkome kuchagua mibunge mijingamijinga inayojali maslahi yao.
 
Nilikuwa Kyaka, kwa kweli wanaishi maisha ya shida. Ukienda na nguo nyeupe lazima zibadilike. Maji ya kuswaki wamanunua ya chupa. Sijui mbunge wa eneo la Kyaka ni nani? Inasikitisha sana. Hapo ndipo mto mkubwa unapita, wakati wakai wa Bukoba hawana maji.

Ni nkenge hapo; ni fyatu Asumpta Mshama
 
Mhe. Ngonani, Wilaya mpya ya Kyerwa iliokuwa sehemu ya Karagwe ina wakazi zaidi ya 400,000 (Sensa 012). Hadi sasa, hakuna hata kaya moja yenye umeme au maji. Katika eneo zima la wilaya hiyo hakuna hata mita moja ya barabara ya rami. Hakuna hata shule moja yenye A-level ya Serikali. Hakuna Hospitali hata moja ya Serikali. Hakuna hata kachuo ka-ufundi. Mbunge wa Jimbo Mhe. Eustace Katagira ndiye mnunuzi mkuu wa Kahawa za wapiga kura wake! Kweli, ukishangaa ya Muleba, BK-Vijijini na Nkenge, utayaona ya Kyerwa!

Dah; Eustace Katagira sijawahi kumsikia kabisaaa. Sjawah kusikia jina kama hilo kwa wabunge
 
Kwanza mimi zamani nilijua kuwa wahaya ni wtu wanjanja sana kumbe nilikosea,nimekuja kuwagundua kuwa ni bogaz sna nikiwafananisha na watu Wa mkoa dare es salaam ambao nilidhani kwakuwa vituo vyote vya hbari viko kwao tv,redio,magazeti na serikali nikitegemea hawa ndio wangekuwa kitovu cha upinzani nchini,kumbe sivyo Wako ccm kwa miiguu miwili na vidole pamoja na hali halisi ya kiutambuzi,ndivyo kagera wasomi wapo lakini uhelewa ziro mkoa mzima ukiondoa biharamulo wko kwa majangili mkome tena mkome
 
Kweli wabunge wa mkoa wa Kagera hawafai na ni mizigo. Assumpta huwa kazi yake kusifia baba ridhiwani tu. Inaonenakana ubunge alipewa kama zawadi kwa kazi anayoijua yeye. Anaongeaga kama waziri akitetea serikali badala ya kuisimamia na kuwakilisha watu wake. Tibaijuka yeye kazi yake kushawishi madiwani wa Kigamboni wakubali mji mpya, ambao ni mradi hatari sana kwa manufaa ya marekani. Wabunge wengine wa Kagera hata hawasikikagi!
 
Mihaya hii inalalamika mitandaoni lakini hairudi kwao kupiga kura wakati wa election!
 
Umeshasema wilaya mpya. unalalamika hivyo kama vile tanzania ni huko tu. Kyerwa ni wilaya imetoka karagwe ambako hiyo lami sio kihivyo. Wabunge wenu ni ndio tu pale bungeni.

Mind you kabla ya kuwa wilaya Kyerwa lilikuwa jimbo la uchaguzi kwa muda mrefu na Kategire sio mkuu wa wilaya mpya bali mbunge wa jimbo husika.
 
Back
Top Bottom