Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,271
- 2,903
Tumekuwa tukishuhudia mambo mbalimbali yakifanyiwa uamuzi wa papo kwa papo kuendana na shutuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na watu husika. Na katika hili mawaziri wamekuwa wakishindana kwa kile kinachoitwa 'kutumbua majipu' katika hili wakati flan tunaona kuwa hata mihemko inakuwepo.Unapomwona waziri anafoka kumfokea mtuhumiwa kana kwamba ni mtoto mdogo n.k . Binafsi naunga mkono kabisa juhudi za kutokomeza ufisadi,ufedhuli,uhujumu,rushwa n.k lakini waswas wangu naona kama njia inayotumika ni ya kimlipuko sana. Na ndo maana tunaona haya yanafanyika kwa kutumiwa wanasiasa hata kwenye nafasi ambazo si za kisiasa. Najiuliza kwa sasa takukuru/pcb ,polisi wana kazi gani? Tukitegemea tu mpaka waziri mkuu au waziri flan ndo akafichue uozo kuna wilaya ngap tanzania ambazo atazipitia kuyafukua hayo? Na je zile ambazo alishapita ina maana sasa zipo huru?maana hawez rud tena ghafla. Wazo langu lilikuwa tusisubir waziri aende na vyombo vya hbr kufoka na kukemea. Tunataka watenda maovu washughulikiwe wakat wote na popote pale kwa kutumia vyombo stahiki. Maana hii pia itaepusha mihemko kwa mawaziri hawa. Lakini pia tuende mbele zaidi. Nini chanzo cha hayo majipu? Kwa nini tusizuie kabisa ugonjwa badala ya kusubiria yachomoze?na pia nasikia kuna majipu humea ndani kwa ndani...