Chonde chonde viongozi wa dini. Tanzania haina dini

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,476
2,651
Wasalaam,

Tarehe 24 viongozi wa dini wanategemea kufanya kongamano kuombea uchaguzi mkuu na taifa hii ni sawa kabisa.

Inasikitisha kuona viongozi wetu hawa wakichanganya dini na Siasa, mnafanya maombi huku mkipigia kampeni CCM haya ni machukizo mbele za Mungu. Mnamwalika mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli kana kwamba Mungu ni CCM, ingekuwa vema mngeliombea taifa nyie kama nyie mkaachana na siasa mnatukwaza waumini wenu.

Maendeleo yana vyama.
 
Ndugu Mtoa Mada!

Soma Hadithi ya Sauli na Daudi kwenye Biblia utakuwa umemaliza kila kitu kwenye tafakuri yako!!

Hakuna tofauti kati ya Sauli na Magufuli, na kati ya Mfalme Daudi na Tundu Lissu

1. Sauli aliteuliwa na Mungu kuwa Mfalme baada ya Watoto wa Eli na Baba yao kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu na wana Israel kudai sasa wanataka mfalme, rejea kipindi cha kampeni 2015 watanzania kudai diktekta, na Magufuli kuwa Raia namba 1

2. Sauli baada ya kupata ufalme akaanza kukengeuka. Rejea mambo aliyoanza kufanya Jiwe baada ya kuchukua uongozi

3. Mungu alivyoona Sauli nae anakengeuka akaamua kumnyanyua Daudi, Rejea kunyanyuka kwa nguvu kwa Tundu Lissu baada ya Magufuli kuanza udiktekta uchwara!

4. Sauli alipoona Daudi anataka kuwa mfalme akajaribu kumuua ila Mungu akamponya Daudi, Rejea jaribio la mauaji la Tundu Lissu na kuponywa kimiujiza kwenye risasi 16

5. Wana Israeli walianza kumpenda Daudi badala ya Sauli na Sauli alianza kuwatesa wana Israel, Rejea upendo wa watanzania ulivyozidi kuwa maradufu kwa Lissu na jinsi Magufuli anavyowatesa wakosoaji wake Mf. Erick Kabendera, Tito Magoti na Mdude Nyangali

6. Sauli kukimbilia kwa manabii wa uongo baada ya kuachwa na Mungu( Hadi mwisho kwenda kwa mganga wa kienyeji), Rejea Magufuli anavyojiweka karibu na kuambatana na watu wanaojiita viongozi wa dini kumbe ni manabii wa uongo, Rejea pia Mganga wa Kienyeji I Sheikh Sharif Majini anavyomtabiria Jiwe na kujiweka karibu nae.

7. Mungu kumkataa Rasmi Sauli na kumfanya Daudi kuwa Mfalme!

Hili ndo jambo la mwisho linaloenda kutokea hapo October 2020. Sababu kuu aliyotumia Mungu ni kwa Sauli kutegemea nguvu zake pamoja na za waganga wa kienyeji, Kuna mtu anawategemea viongozi wa dini pamoja na waganga wa kienyeji kama Sheikh Sharif Majini ili wamfanye kuwa Raisi, Sasa Mungu hapendi hili na anaenda kujibu kwa hasira hapo October kwa kumthibitisha ikulu Tundu Antipas Lissu( Mfalme Daudi)

Tukutane October!!!
 
Back
Top Bottom