Chonde chonde Chadema Muwe makini katika hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde chonde Chadema Muwe makini katika hili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jibaba Bonge, Sep 19, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mgombea urais wa Ccm amekuwa akifanya mikutano ya kampeni sehemu mbalimbali nchini. Mikutano hiyo imekuwa ikifanywa ionekane mikubwa sana kwa kusomba watu kwa mabasi na malori kutoka sehemu za mbali na mkutano husika.

  Watu wengi katika mikutano hiyo wamekuwa katika mavazi ya rangi kijani na njano, rangi za ccm. Watu hawa wako katika makundi yafuatayo:- 1. Wanachama wa ccm wa jimbo ambapo mkutano unafanyika (wanaolipwa kanga, kofia na mashati yenye rangi za ccm) , 2. Wanachama wa ccm toka majimbo ya mbali (wanaolipwa kanga, kofia na mashati yenye rangi za ccm na zile elfu mbilimbili ua tanotano au hata kumikumi na petrol kama ilivyofanyika Arusha ), 3. Wasio wanachama wanaotafuta mlo wa siku kwa kufuata upepo unakovumia (hawa hufanyiwa ka no. 2 hapo juu), 4. Wanaofuata maonyesho ya wasanii waliopo kwenye mikutano hiyo.

  Lengo la ccm kufanya hivi ni ili mikutano yake ionekane mikubwa sana na hivyo kuuhadaa umma kuwa inapendwa sana na wananchi. Hii inatokana na watu waliokuwa kwenye mkutano jimbo A ni haohao unawakuta Jimbo B na Jimbo C n.k , kazi ya malori na mabasi ya kukodiwa au ya wanaodaiwa wakereketwa.
  Kama hawa watu ni wanachama wa ccm wa majimbo inapofanyikia mikutano ya kampeni, walikuwa wapi wakati wa kura za maoni? Mbona idadi ya kura zote za wagombea , nzuri na zile zilizoharibika hazifanani na idadi ya watu wenye sare katika mikutano? Sehemu nyingine jumla ya kura za maoni haikufika hata 10,000 kwa jimbo zima (na kutokana na jiografia ya sehemu hizo siyo rahisi wote wakawepo kwenye mkutano mmoja bila kuwezeshwa), hawa watu wengine wametoka wapi? Ni makundi mane niliyoeleza hapo juu.
  Kwa sasa chama tishio kwa ccm ni chadema, kama alivyo sema memba mmoja humu kuwa mti wenye matunda ndiyo unaopopolewa mawe; hayo yamedhihirika kwa chadema kufanyiwa rafu mbalimbali wakati huu wa kampeni.

  Chadema chonde chonde pamoja na kampeni zinazoendelea, muandae pia mikakati ya kulinda kura wakati wa upigaji na uhesabuji. Ccm wanaweza kuchakachua kura kwa kuingiza kura za mgombea wao wakati wa upigaji kura au kuondoa kura za wapinzani wakakti wa kuhesabu. Watajifanya kujastify matokeo yao na mahudhurio ya watu kwenye mikutano yao. Yalishafanyika hayo miaka ya nyuma kule zanzibar, Ubungo na sehemu nyingine nyingi. CHADEMA MUWE MAKINI KULINDA KURA.
   
 2. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  kaka, hapo umenena!!!
   
 3. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema imeshashinda kazi ni namna ya kulinda ushindi
   
 4. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hii imekaa vizuri, chadema jiandaeni na usimamizi mzuri wakati wa uchaguzi
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This is so nice buddy!!!!!!!!!!!
   
 6. Jahmercy

  Jahmercy Member

  #6
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Haya sasa kaz ndo hyo, wanachadema na wapenda haki watz wote kwa pamoja tushiriane kuhakikisha tunadhibit wiz huu wa kura, HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE. Jaman napenda kuwasalim wanajamii wote mm ni mgen humu.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Good News!.
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Well said mkuu. Hata hivyo CHADEMA hawapaswi kubweteka, waongeze kasi ya upigaji wa kampeni kila kona ya nchi na kuongeza idadi ya mabango ya kumnadi Dr. Slaa. Nina imani kwamba ushindi unawezekana lakini si lelemama. Visije tafutwa visingizio hapo baadaye, kuna haja ya kutumia nguvu ya ziada kuwafikia watu wote mahali pote nchini kwa njia ya redio (karibu kila mkoa na wilaya sasa hivi ina redio tuzitumie hizo), TV, magazeti na pia tusambaze picha na mabango ya kumnadi mgombea wa CHADEMA kwa kasi ya ajabu hasa katika muda wa wiki mbili au tatu kabla ya uchaguzi. Hii itaibua hamasa mpya kwa wananchi pale watakapoona mabango ya rangi tofauti na kijani na njano walizozoea kuziona, na ambazo kwa wakati huo zitakuwa ni za kawaida tu kwao.
   
 9. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I am ready to die for my country!! Hii kazi siyo ya Chadema tu ni yetu wote kama wapenda nchi, wenye kujali haki na amani. Tunapenda kuona chama fulani kinashinda kwa haki siyo kwa mizengwe ya kutuibia.

  Chadema, mtuongoze namna ya kulinda kura tafadhali. Toeni tamko, hata kuwasema tu nako inaashiria kujua mbinu zao. Dr Slaa, waseme kwa umma kuwa wanasomba watu kuhudhuria mikutano kutoka mbali.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Off all the things twaweza dharau lakini ili la vituo vya kupigia kura na uhesabuji wa kura ni la msingi bse all the efforts will be meaningless.
  Mimi niko tayari kusimamia kituo chochote kwa gharama zangu ili mradi haki ifuate mkondo wake
   
 11. D

  Dopas JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli kama alivyosema Mbowe kuwa mwaka huu kura haziibwi. Ulinzi makini uwepo. Nina hakika haki ikitendeka, CCM hairudi madarakani. Chadema iwe macho, kura za haki zisipotee.
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Kwani kuvaa sare za CCM (au kijani na njano) ni lazima uwe mwanachama wa CCM?! Kama sio; Sasa suala la kwamba mbona kwenye kura za maoni hawakuonekana linatoka wapi? Wapiga kura kwenye kura za maoni ni lazima wawe wanachama wa CCM lakini sare za CCM au zinazofanana na za CCM zinaweza kuvaliwa hata na CHADEMA; tafuteni hoja za msingi zenye mashiko kwenye vichwa vya wa2 wenye akili zao!!!
   
 13. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hauko peke yako mkuu, Mimi binafsi nimejitolea kuwa wakala wa CHADEMA kwa garama zangu binafsi.
   
 14. MAWANI

  MAWANI Member

  #14
  Sep 19, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jibaba, hapo umenena. Sasa nani anaweza kutudokeza namna gani tulinde kura zetu ili Mh. Dr. Slaa atangazwe mshindi kwa kura zetu??
  Ni muhimu tuwe na mkakati mapema iwezekanavyo.
   
 15. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sure kaka..lakini hata wewe unaweza kuwa mlinzi pia..!
  Ukishapiga kura usiende Kulala..sogea mita 100 kutoka katika kituo chako..then kaa ukisuburi matokeo...Hakuna kulala mpaka kieleweke...!
  Kazi ya kulinda kura ni ya wapiganaji wote....!
  Pamoja tunaweza.....!
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi na kichwa chako
   
 17. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ajenti wa mafisadi utamjua tu kwa maneno na matendo. ni kweli wao wanajifanya wanaakili sana kuliko watanzania wote ndiyo maana wanatuibia usiku na mchana, but mwaka huu ndio mwisho wenu nchi tunairudisha mikononi mwa watanzania wenyewe.
   
 18. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2010
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  hii ishu ya kulinda kura ni muhimu sana,tuwe na wasimamizi waelewa na wenye uchu na mabadiliko,mikakati ianze mapema na ni wajibu wetu kulinda kura zetu mpaka kieleweke hakuna kulaa.
   
Loading...