NIFANYE NA MIMI KAKA DICK-37
Mtunzi:Juma Hiza
Age:18+
ILIPOISHIA....
Safari yetu ilikwenda kuishia Mbezi Beach mbele ya nyumba moja ya kifahari sana, niliitazama nyumba hiyo katika macho ya matamanio, Ilionekana kuwa ni nyumba ya kisasa ambayo ilisheheni kila kitu cha kuvutia, kama ungepata bahati ya kuitazama hakika ungeyasahili maneno yangu.
SONGA NAYO.....
“Hapa ni wapi?” nilimuuliza Precious kisha akatabasamu, hakunijibu lolote badala yake alipiga honi kuashiria kuwa alikuwa nje na baada ya dakika chache geti liliweza kufunguliwa na kijana mmoja ambaye kwa macho ya harakaharaka alionekana kuwa mlinzi.
Hatimaye tukaingia ndani ya nyumba ile ya kifahari kisha Precious akaenda moja kwa moja mpaka eneo maalumu la kuegesha gari, akaliegesha vyema kisha tukashuka.
Macho yangu yalikumbana na gari la kifahari aina ya BMW 545 yenye thamani ya shilingi milioni hamsini na sita lililokuwa limeegeshwa pembeni na pale ambapo Precious alikuwa ameegesha gari lake. Sio siri nilizidi kujionea maajabu tu! kwani mpaka kufikia wakati huo Precious hakuwa ameniambia lolote lile.
“Vipi mpenzi,” aliniambia Precious kisha akanisogelea na kunishika mkono, tukaingia ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa imekamilika kila kitu ndani, hakukuwa na kasoro yoyote.
“Unaionaje hii nyumba?” aliniuliza swali nililoliona kuwa kama la kunikejeli kwani ukweli nyumba ilikuwa ikionekana kuwa nzuri hata bila kuulizwa lolote.
“Mbaya tu!” nilimjibu huku nikijifanya kama sielewi. Alicheka kisha akajizuia.
“Baby embu acha masihara ujue mimi nakuuliza kwa kumaanisha.”
“Kiukweli nyumba ni nzuri sana inaonekana kukamilika kwa kila kitu kasoro kitu kimoja tu!”
“Kitu gani?”
“Hakuna watu,” nilijibu kisha akacheka tena.
Alionekana kuwa na furaha sana, uso wake ulitawaliwa na tabasamu mwanana lililozidi kumfanya aonekane kuwa wa aina yake.
“Dick,” aliniita baada ya ukimya mfupi kutawala.
“Niambie malkia wangu,” nilimjibu huku nikimshika kiuno chake laini kilichogawanyika mithili ya mdudu nyigu.
“Asante sana kwa zawaidi uliyoweza kunipa katika maisha yangu, siwezi kukusahau.”
“Zawadi?”
“Ndiyo.”
“Zawadi gani?”
“Mimba.”
“Unasema?”
“Nina mimba yako Dick,” aliniambia kisha nikajifanya kama nimeshtushwa na taarifa hizo ambazo sikuzitegemea.
“Nini mbona umekuwa hivyo?”
“Hamna, siamini kama nimeweza kukupa ujauzito.”
“Amini Dick, wewe ndiyo mwanaume pekee ambaye umeweza kunibadilisha jina, naamini hivi karibuni na mimi nitakwenda kuitwa mama wa mwanao, nimebeba kiumbe chako Dick,” aliniambia.
“Ujue siamini kabisa.”
“Amini Dick nina kiumbe chako tumboni.”
“Dah!”
“Ila baby usijali unakumbuka nilikuahidi nini?”
“Nini?”
“Nilikuahidi vitu vingi sana ila kubwa ni kukununulia nyumba, usafiri pamoja na kukupa mtaji utakaoanzia katika biashara yako ya vitabu.”
“Ndiyo nakumbuka.”
“Basi hivi vyote unavyoviona mbele yako kuanzia sasa vipo chini yako,” aliniambia Precious maneno ambayo nilihisi wenda alikuwa katika utani, alikuwa akinitania lakini haikuwa hivyo bali kila ambacho alichokuwa akikizungumza alikuwa akikimaanisha.
“Ina maana ile BMW na hii nyumba unataka kuniambia vyote kuanzia sasa ni mali yangu?” nilimuuliza.
“Ndiyo baby,” alinijibu Precious huku akionekana kutojali lolote lile.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mimi kumiliki nyumba nzuri, gari la kifahari na pia kukabidhiwa kiasi cha pesa ambacho nilikitumia kama mtaji wa kutoa vitabu vyangu. Niliamua kuhama Tandale na sasa maisha yangu yakahamia Mbezi Beach.
Sikutaka kufikiria lolote kuhusu mume wa Precious pamoja na taarifa zile za ujauzito. Nilichokuwa nakiangalia kwa wakati ule ni ule utajiri wa ghafla! niliyoweza kuupata katika maisha yangu, ulikuwa ni utajiri ambao kwa kweli kama ingetokea ukaniuliza niliupata katika njia zipi, jibu pekee ambalo ningeweza kukujibu ni kuwa nilitembea na mke wa mtu kisha akaweza kunihonga wala hakukuwa na njia nyingine. Siyasemi haya ili nikushinikize na wewe unayeyasoma maandishi haya uende ukafanye kama mimi nilivyofanya lahasha! isipokuwa ipo sababu ya msingi ya kukuandikia haya kwani naamini mwisho wa siku utaweza kujifunza kitu kupitia mimi Mr. Chombezo au ukipenda unaweza kuniita Dick Mapenzi. Majina haya ndiyo yaliyoweza kuniponza Dick mimi ambaye leo naishia kusimulia tu!.
****
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kipekee sana kwangu, kwanza nakumbuka nilimtafuta Mick simuni kisha nikamuelezea kila kitu kichokuwa kimetokea, aliweza kunishangaa sana.
“Dick ujue una michezo hatari sana,” aliniambia.
“Kwanini unasema hivyo?”
“Unajisifia kabisa umempa mke wa mtu mimba halafu kakupa nyumba unafurahi kabisa.”
“Sasa wewe ulitaka ninune au? Kwanza yeye mwenyewe ndiyo kaniletea shobo mimi nifanye nini sasa?”
“Ndugu yangu unapotea.”
“Acha uzoba wewe hapa ni mjini na mjibu kuishi ni mipango hivi unafikiri kwa maisha haya yalivyo magumu halafu anatokea mtu anakupa pesa utaanzaje kuzikataa.”
“Dick mke wa mtu sumu.”
“Hayo ni maneno tu! siku hizi tunakula mpaka vya nyongeza.”
“Unajua unafanya masihara lakini ipo siku hivyo vitu vitakutokea puani.”
“Ndugu yangu sasa naona unafika mbali kama vipi baadae ngoja leo nitafute kahaba nilale naye huku maana tayari nimeshakuwa Don,” nilimwambia kisha nikakata simu.
****’
Kitendo cha kuhamia Mbezi Beach kilikwenda kuufungua ukurasa mpya hata katika upande wa wasichana niliyokuwa nikitembea nao, sikutaka kuendelea kutembea na wasichana kama akina Helena ambao walionekana kuwa na shida, niliamini kama ningeweza kuwa nao basi hakukuwa na kitu cha ziada ambacho kingeweza kubadilika sanasana ndiyo kwanza wangezidi kunipa mawazo ya kuwahudumia wakati mimi mwenyewe nilikuwa nikihudumiwa.
Nilianza kubadilika kimavazi, kila siku nilionekana kupendeza sana hata wale wasichana waliyokuwa wakiziona picha zangu Instagram nilizokuwa nimezipost huku nikiwa nimeegemea gari langu la BMW hakika ziliwachanganya sana.
“Mbona umehama bila kuniambia?” aliniuliza Evadia usiku mmoja nilipoamua kumpigia simu.
“Nisamehe mpenzi nilisahau kukuambia,” nilimjibu.
“Umehamia wapi?”
“Sasa hivi nimehamia Mbezi ila usijali kesho lazima nikuone na utakuja kupafahamu.”
“Sawa Mume wangu nitafurahi.”
“Ukitoa wewe hakuna mapenzi tena, wewe ndiyo maana ya mapenzi yangu.”
“Umeanza na vijimaneno vyako.”
“Huo ndiyo ukweli.”
“Halafu nimekumis baby.”
“Nimekumis pia.”
“Njoo basi sasa hivi mpenzi, nauhitaji ukaribu wako.”
“Nikija siunajua nini kitatokea?”
“Haya nakuja.”
“Njoo tu! babyyy nitakupa ondoa shakaa.”
“Hodi.”
“Karibu.”
“Asante, mbona sasa hujachojoa nguo?”
“Tayari baby.”
“Sawa, sogea basi.” “Tayari baby nipeee,” aliniambia kwa sauti ya kimahaba ambayo ilinifanya akili yangu ibadilike na kuanza kufikiria ngono na kila ambacho nilikuwa nikikizungumza kwa wakati huo hakikuwa na maana nyingine zaidi ya ngono.
Kilichoendelea kusikika kwa upande wa pili ni miguno pamoja na sauti za kimahaba alizokuwa akizitoa Evadia, alikuwa akilalamika kana kwamba nilikuwa nikifanya naye mapenzi kumbe yalikuwa ni mapenzi yaliyofanyika simuni. Kutokana na uhodari wangu katika kucheza na michezo hii nilizidi kumpagawisha kwa kumpa muwashawasha uliyozidi kumuacha mpaka akawa analia kwa kuomba utamu wangu.
“Ooooooh, babbyyyyyyy nipe nipeeee ooooohhh chukuaaaa yoteeee yakoooo aaaasssshhhh ooooohhh aaaaaaah,” alitokwa na miguno wakati huo nilikuwa nikifanya naye mapenzi kwenye simu.
Je, ni nini kitaendelea?
Tukutane Jumatano mahali hapahapa.
#Like nyingi, komenti yako pamoja na Share nyingi ndizo zitafanya Chombezo hili liweze kufika mbali.