Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
- Thread starter
- #41
NIFANYE NA MIMI KAKA DICK-32
JUMA HIZA
Age:18+
ILIPOISHIA.....
Kazi kubwa iliyokuwa imebakia kwa wakati ule ilikuwa ni kutafuta njia ya ziada ya kuweza kumuingilia Evadia mpaka akubali kunisaidia nia yangu ya kutoa filamu na muigizaji huyo ambaye alikuwa na urafiki naye. Ilikuwa ni kazi ngumu mno lakini niliamini kufanikiwa katika hilo.
SONGA NAYO......
Ulikuwa ni mwanzo wangu wa kuonyesha mapenzi ya dhati niliyokuwa nayo kwa Evadia, nilikuwa nikionyesha kumpenda sana kiasi kwamba kuna kipindi alikuwa akishangaa upendo ule ulikuwa unatokea wapi hasa. Kila siku sikuacha kumtafuta, nilikuwa nikimtumia ujumbe mfupi na hata pale alipoonekana kuwa kimya kwa kutonijibu ujumbe wangu niliamua kumpigia na hapo tuliweza kuzungumza mambo mengi sana kuhusiana na mapenzi yetu. Alionekana kuniamini kwa kila kitu na hiyo ndiyo ilikuwa ngao yangu kubwa ya kutimiza lengo langu kwa wakati ule.
“Baby halafu kuna kitu nataka kukuambia,” aliniambia Evadia siku moja tulipokuwa dukani kwake.
“Kitu gani?”nilimuuliza.
“Nataka uje ujitambulishe kwa wazazi wangu,” aliniambia kisha nikabaki nimeshikwa na butwaa kwa muda halafu nikajilazimisha kutoa tabasamu, nilikuwa nikitabasamu tabasamu la uwongo, sikuwa nikitegemea kama Evadia angeweza kuniambia maneno yale kwa wakati ule.
“Nini?” aliniuliza mara baada ya kuniona nikitabasamu.
“Hamna kwahiyo unataka twende lini?”
“Hata kesho mpenzi siunajua jinsi ninavyokupenda?”
“Ndiyo nafahamu ila tusifanye kesho unaonaje tukapanga siku nzuri ambayo nitaweza kwenda kujitambulisha kwa wazazi wako?”
“Sawa nimekuelewa mpenzi naamini wewe ndiyo mume wangu mtarajiwa.”
“Hata mimi naamini wewe ndiyo mke wangu wa maisha,” nilimwambia kisha tukakumbatiana.
Mapenzi yangu na Evadia yaliendelea kupamba moto kila siku, nilijitahidi sana kumfanya azidi kuwa karibu yangu kiasi kwamba hata nitakapofikia hatua ya kumueleza nia yangu asiweze kunikatalia, niliamini kulikuwa na ugumu katika kulitimiza hilo na ndiyo sababu iliyonifanya nizidi kuwa mpole.
****
Penzi la Precious bado halikufutika kichwani mwangu niliendelea kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi lakini mapenzi yetu yalikuwa ni ya kujiiba. Nilifahamu fika kuwa Precious alikuwa ni mke wa mtu, mke wa mwanaume ambaye alikuwa akipambana usiku na mchana kutafuta riziki ili aweze kuihudumia familia yake.
Kwa muda mrefu wa ndoa yake hakuwa amebahatika kupata mtoto na hii ndiyo sababu iliyomfanya apunguze mapenzi kwa mume wake. Alikuwa akiniambia mambo mengi sana na jinsi ambavyo ndugu wa mume wake walivyokuwa wakimuandama kwa maneno yaliyokuwa yakizidi kumuweka katika wakati wa maumivu kila siku, alikuwa akitamani sana kupata mtoto katika ndoa yake lakini hakubahatika.
“Ndoa yangu inanitesa sana, natesekea Dick natamani mpaka kufa,” aliniambia Precious huku machozi yakimdondoka, alikuwa akilia kwa uchungu mno.
“Hapana hutakiwi kusema hivyo unakufuru,” nilimwambia huku nikijaribu kumbembeleza, alikuwa akibubujikwa na machozi kwa wakati huo, sikutaka kuyaacha machozi yake yaendlee kumtoka mbele yangu, niliamua kumfuta.
“Dick ndugu wa mume wangu wananinyanyapaa sana kila siku ugomvi hauishi ndani ya nyumba.”
“Kwani unaishi nao pamoja?”
“Ndiyo baada ya kuona sijampatia kaka yao mtoto wameamua kunifuata na lengo lao kubwa wanataka niachike.”
“Mh! Kweli hilo ni tatizo.”
“Dick naumia sana, naumia sana,” aliniambia kwa sauti iliyogubikwa na wimbi la masikitiko makubwa.
Kila nilipokuwa namtazama alizidi kuonekana kuwa mtu mwenye shida, sura yake ya masikitiko ilizidi kunidhihirishia wazi kuwa kulikuwa na kitu alichokuwa anakihitaji kwa wakati ule, sikutaka kujifanya ajuza wa kufahamu kila kitu, niliamua kuwa mkimya nikimpa nafasi ya kutaka kujielezea na kama yalivyokuwa mawazo yangu aliniita kwa sauti ya chini huku uso wake akiwa ameuelekeza chini kisha nikamuitikia huku nikiyapa wasaa masikio yangu yaweze kumsikiliza.
“Naomba unisaidie kitu kimoja,” aliniambia.
“Kitu gani?” nilimuuliza.
“Naomba unipatie mtoto sina tatizo lolote mimi katika kizazi changu, tatizo lipo kwa mume wangu naomba unipe ujauzito na ninakuahidi ile ahadi yangu ya kukupa nyumba pamoja na mtaji wa kutoa vitabu vyako nitakupa, naomba unisaidie niondokane na fedhea hii inayoniandama katika maisha yangu,” aliniambia Precious.
Je, ni nini kitaendelea?
Usikose sehemu ijayo ya Chombezo hili mahali hapahapa.