Chips za CCM-Mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chips za CCM-Mafisadi

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by eedoh05, Oct 5, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Maswali na Majibu Darasani:

  Mwalimu(Mtanzania Halisi
  : Leo tutajifunza hesabu za sehemu. Tunaanza na Juma. Enhe, Kiazi tukikikata katikati tunapata nini?(anakikata kiazi sehemu mbili zilizo sawa)
  Juma: Tunapata nusu ya kiazi.
  Mwalim(Mtanzania halisi): Sawa, Juma. Haya darasa mpigieni makofi. (makofi yanasikika,mwalimu anaichukua ile nusu sehemu anaikata sehemu mbili zilizo sawa) Je! hii ni sehemu gani ya kiazi Flora?
  Flora: Hiyo ni robo kiazi mwalimu.
  Mwalimu(Mtanzania halisi): Sawa kabisa, umepata.(mwalimu anaikata katikati ile robo).Sisiem hebu tuambie, hii robo nimeikata katikati; tunapata nini hapa? (Sisiem ndiye mwanafunzi mkubwa kwa umri na umbo pale darasa la 1)
  Sisiem:
  Chips iiiiiiii!
  Mwalimu(Mtanzania halisi)
  : (kwa mshangao mkubwa,huku akiwa ametoa macho kwa Sisiem) Duh! Kaazi kweli kweli! Ndio maana kila kitu mnakiona chips. Kweli kasungura ni kadogo!
   
 2. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  ccm wanaharibu kila sehemu
   
Loading...