Chips nyama 8000 Singida Hotelini

Sasa mtu mwenye kisukari ndiyo hatakiwi kabisa kula kula hovyo njiani, bora atoke home na Chakula chake..
 
Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
Nunua biskuti na juice ya Azam mixer, apple
, chungwa/ndizi...
 
Tumia akili.

Sio kila safari mtu anatokea nyumbani.

Safari zingine unatokea mkoani kikazi (mfano Musoma/Rukwa), unarudi zako Dar es Salaam.

Unatoka Musoma/Rukwa saa kumi usiku, unafika Dar 11 alfajiri au kesho yake kabisa
Kwani huko mikoani hakuna hotels? Mfano Kigoma pale kuna fast food restaurants unaweza nunua Usiku na wakakufungia vizuri tuu..
 
Pale Moro ukipanda ABC UPPER CLASS BUS wana hotel yao pale Kingoluwira instwa Carte Hotel, yaani vyakula ni bei mbaya sanaaa..
 
Unaruhusiwa kula ndani ya Bus huku safari ikiendelea na ma Bus mengi yana dust bin
Mbona?? Hata kwenye hizo hotel zao utasikia tunasimama dakika 10 tujisaidie, na tuchukue chakula na kurudi kwenye Bus..
 
Pale Moro ukipanda ABC UPPER CLASS BUS wana hotel yao pale Kingoluwira instwa Carte Hotel, yaani vyakula ni bei mbaya sanaaa..
Napajua pale sasa ni kheri ya pale mazingira ni mazuri na ni pa safi sanaaa..uje upande shabib ili waka jutupe hapo ninapo sema utajionea mazingira ni machafuuuu wali maharagwe unauziwa 5000 can you imagine ? Bahati mbaya siku piga picha
 
Mmmh mayayiii tena.... air conditioner iwepo aisee
😆😆 Kuna mwamba alinunua mayai na mahindi ya kuchemsha pale Chalinze akala mayai na mahindi yake, aisee Ruvu hakumaliza mwambaa akaomba msaada kwa konda akajisaidie nahisi alikutwa na MHARISHOOO maana basi ilipo simama alitoka resi kuelekea vichakani
 
Unazani ni rahisi hivyo safari ya masaa kumi unakula tu vitu vya baridi tu mimi kwangu wala huwa sijutii kununua chakula hicho hotelini kwa bei kubwa kutokana na mazingira kikubwa watu tujifunze kujipanga tunavyosafiri ata kama utabeba chakula chako safari ikiwa ndefu tumbo huwa linagoma kuendelea kupokea chakula cha baridi
Chips za hivi usafi sifuri kabisa... Ila mazoea bwana yaani kweli mtu anashindwa kutoka home na skonzi/slesi 2 za mkate, mayai ya kuchemsha 2, chungwa/ndizi na juice/soda kweli?? Tena safari yenyewe Dar to Dodoma
 
Sijui una maanisha nini kwa chakula cha baridi, nowadays kuna vi container vizuri tuu vidogo ambavyo vipande vya kuku 2 au nyama finyango 5 zilizoko kwenye foil unaziweka ndani ya kikontaina na muda wa kula bado vinakuwa fresh kabisa. Tatizo hatuna hayo mazoea sisi, niliwahi kufanya kazi na mzungu mmoja kwenye NGO fulani for 3 years sikuwahi kumuona kantini au akiagiza chakula sijui chips au nini. Kwenye begi lake la laptop ana maji yake, coffee mug, na kikontena kidogo cha chakula from home. Cha ajabu ni kwamba huyo mzungu salary yake ni kubwa mnooo kutushinda siye woootee mpaka mkurugenzi mkuu but siye ndiyo tunaongoza kuagiza chips kuku, biriani, makange etc... Na tukiishiwa huwa tunaenda kumkopa yeye pesa, basi huwa anacheka sana jinsi ambavyo hatuna bajeti na nidhamu ya pesa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…