Chinese Taxi Driver in Bongo?

Chinese Taxi Driver in Bongo?

J4 King hivi sio kwamba kuna maeneo twaweza kuruhusu wawekezaji na mengine hapana??
yaani kwetu mabo yanfanywa holeholela....hata tax driver awe mchina??? haya sisi tufanye nini sasa?? tunabaki kumangamanga ndani ya nchi yetu!!!
huyo anayesema huduma yao nafuu hebu atuthibitishie basi...

asa uhv said it ....hapa si kw amaslahi ya taifa mkubwa....pity!

Mkuu nilishawahi ona wachina wakisukuma mkokoteni mitaa ya bunge mkokoteni ulikuwa na kreti na mabox. Mie na watu niliokuwa nao tulishindwa kuelewa ilikuwa ni 'usafiri' nafuu au ndio 'wawekezaji' walikuwa kazini!
 
This is a wake up call for everybody! Tuache kulalamika na kutumia fursa zilizopo, although i have to say kufanya competition na wachina especially kwenye biashara, tena ya vitu vinavyotoka kwao is rather difficult. Kuna nguo za watoto jamaa wanauza 2000-2500 , nguo ambayo ungeinunua kwenye duka la mbongo kwa 8000 minimum. so akili kichwani, tumieni hizo fursa kama hizo kwa kufanya biashara hata mikoani ambako hawajafika, that is just one example coz i think they are here to stay, seeing the kind of leadership we have.
 
Inabidi watanzania waamke, anayetaka kujua dunia inakwenda wapi ajaribu kusoma historia ya dunia kutoka katikati ya 1800 hadi hivi leo. Upepo wa mabadiliko yanayotokea leo dunia ni ya kawaida na yametarajiwa toka wakati huo. Dunia imeshafikia kuwa katika ngazi moja kama vile kijiji kwa hiyo kama tuna-resist mabadiliko tutalia kilio mbwa na kusaga meno. Tunachotakiwa si kulalamika, la hasha tuangalie na sisi tutabadilikaje kuendana na hali halisi ya mabadiliko.

Endapo mimi ninafanya kazi mwezi mzima, nitahitaji at the end of the day nifanye saving, ikiwa dukani kwa mchina anauza nguo kwa 2500/= na kwa mbongo 8000/=, sihitaji rocket science kuona ni wapi nitapa nafuu, na hii ndiyo faida ya utandawazi, wabongo wawe wabunifu kwani biashara zao zitazidi kudoda. Endapo Taxi ya mchina inatoa huduma nzuri na kwa bei nafuu, nina sababu gani ya kwenda kukamuliwa pesa nyingi kwa mbongo mwenzangu? Dunia inasonga mbele kwenye soko huria na haitarudi nyuma. China yenyewe kama nchi imeona kuwa isipofanya mabadiliko itaachwa nyuma, leo hii China ni tishio katika anga za kiuchumi wa dunia.
 
aaaaaaaaaaaaah nimemuona si mweupe hivi eeeh,mfupi kidogo eeeeh ananywele za kichina,kiswahili kama kawaaaaaaa?
 
yeah..ndo hivyo WAchina walivyo.. Ubaya mmoja wakiingia mahali hawatoki. Wanabaki hapo forever. Angalia ishu ya Angola..inasemekana kuna Wachina zaidi ya milioni mbili. Taani kama mkoa wa arusha, kilimanjaro na tanga yaani. Nawashangaa Uhamiaji wako wapi. Utashangaa kuona Uhamiaji wanabania passport ili watu wasiende nje lakini cha ajabu wachina wako hapa kwetu bila ya hata visa. Lazima Watanzania tufunguke macho na kuona hili kwamba ni jambo la hatari kwa maisha ya baadae..Uhamiajiiiiiiiiiiiiiiii amkeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii... Ondoeni wamachinga wachina upeeeeeeeeeeeeeeeeeesi
 
Kabla hatujaanza yale yalitokea hivi majuzi South Africa tujichunguze wenyewe, Leo tunawasema wachina Kesho wanaingia rasmi Wakenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Ikiwa tutaendelea kuvuta miguu tunapopewa kazi...inachukua nusu saa kuletewa kinywaji mezani unapoagiza, maofisi mahospitali kazi haziendi kwa gharama mteja anayolipia, muda si mrefu tutawakuta wafagia barabara si watanzania.
 
I recently had a conversation na shop owner hapo Kariakoo, Mtaa wa Swahili. Jamaa wanadai wachina wanaua biashara ya knobs za draws na vitasa. Mimi mwenyewe nimeshuhudia duka moja hapo Kariakoo – adjacent to Swahili street, but near where they sell electrical goods. Jamaa bei zao ziko chini kishenzi, yani huwezi kushindana nao. I didn't buy from them kwasababu najua wabongo wanahitaji biashara yangu. But with those kind of prices, I don't know how long I can hold my breath ...😕

How are Chines by the way????😕
Yani siku hizi ni wao na wahindi wameivamia nchi hii hapa kwetu sie nio wavivu au?😕

are we degrading ourselves??😕 ni kitu gani sie hatuwezi fanyaaa jamani watu toka mashariki ya mbali waja fanya kazi ambazo sie hata huko kwao ukifanya is a big scandal, wao wakija Bongo they're free to do anything they want.

Sheria za wahamiaji hazitulindi wazawa😕

Inabidi watanzania waamke, anayetaka kujua dunia inakwenda wapi ajaribu kusoma historia ya dunia kutoka katikati ya 1800 hadi hivi leo. Upepo wa mabadiliko yanayotokea leo dunia ni ya kawaida na yametarajiwa toka wakati huo. Dunia imeshafikia kuwa katika ngazi moja kama vile kijiji kwa hiyo kama tuna-resist mabadiliko tutalia kilio mbwa na kusaga meno. Tunachotakiwa si kulalamika, la hasha tuangalie na sisi tutabadilikaje kuendana na hali halisi ya mabadiliko.

Endapo mimi ninafanya kazi mwezi mzima, nitahitaji at the end of the day nifanye saving, ikiwa dukani kwa mchina anauza nguo kwa 2500/= na kwa mbongo 8000/=, sihitaji rocket science kuona ni wapi nitapa nafuu, na hii ndiyo faida ya utandawazi, wabongo wawe wabunifu kwani biashara zao zitazidi kudoda. Endapo Taxi ya mchina inatoa huduma nzuri na kwa bei nafuu, nina sababu gani ya kwenda kukamuliwa pesa nyingi kwa mbongo mwenzangu? Dunia inasonga mbele kwenye soko huria na haitarudi nyuma. China yenyewe kama nchi imeona kuwa isipofanya mabadiliko itaachwa nyuma, leo hii China ni tishio katika anga za kiuchumi wa dunia.
Nakubaliana nawe. Swala la msingi sana umeeleza.

Ila sasa, unataka tufungue milango raia wa kigeni waingie nchini wafanye kazi watakayo? Nipe majina ya nchi zinazofanya huo upuuzi.

Wenzetu wana-incourage foreign workers waende kufidia pengo la uhaba wa skilled labor kwenye maeneo maalum, mfano madaktari. Tunahitaji manesi na madaktari zaidi ili tuishi kwa afya. Tunahitaji waalimu ...kuna maeneo mengi tu.

We don't need unskilled labor as we already have enough of those. Perhaps we should think about moving some of our unskilled labor to China; that would be cool - itapunguza msongamano kwenye magereza yetu.
Tunahitaji kuchuja Chinese criminals wanaokimbia mkono wa sheria huko watokako.

Foreigners waje, wafanye kazi kwenye makampuni ya watanzania, sio waanzishe makampuni yao. Au kama ni makampuni yao (mfano kwenye construction) sheria iwalazimishe wafanye kazi jointly na locals.

Usimamizi wa sheria zilizopo ni hovyo. Wafanyakazi serikalini na taasisi zake wamekuwa mstari wa mbele kuingia ushirika na wageni kufanya mambo kinyume na sheria. Magogo kiasi gani yametoroshwa? Nyara kiasi gani wamekomba? ...You name it!

Mfano mdogo tu kuhusu sheria:
In Malaysia: Foreign workers can only work for five years
SOURCE: http://whiteglove.com.my/index.php?option=com_content&task=view&id=197&Itemid=47

Picture that! Jiulize kwa nini wenzetu wameweka sheria ya namna hiyo.
 
Kabla hatujaanza yale yalitokea hivi majuzi South Africa tujichunguze wenyewe, Leo tunawasema wachina Kesho wanaingia rasmi Wakenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Ikiwa tutaendelea kuvuta miguu tunapopewa kazi...inachukua nusu saa kuletewa kinywaji mezani unapoagiza, maofisi mahospitali kazi haziendi kwa gharama mteja anayolipia, muda si mrefu tutawakuta wafagia barabara si watanzania.

Tatizo ni viongozi wetu ni wanafki sana waliona kutowanufahisha watanzania wenzao ili wao wafaidi wakijua kwamba wao ni viongozi na wanatakiwa kuutumikia umma na sio kujineemesha sasa wanazipindisha sheria ili waneemeke kuliko raia au wananchi wanao waongoza. yani hapa wananchi ndio tuamke sasa la sivyo tutakuja kuuzwa ndani ya nchi yetu hapa.

...

We don't need unskilled labor as we already have enough of those. Perhaps we should think about moving some of our unskilled labor to China; that would be cool - itapunguza msongamano kwenye magereza yetu.
Tunahitaji kuchuja Chinese criminals wanaokimbia mkono wa sheria huko watokako.
......
Well put!
 
the thing that suprises me the mast it is very easy for chienise to get a permit to work in our country thn why cant we get a permit t work or get a got in theirr country?
 
Whoever is serious concerning what we are here asking about i've got an e-mail on my id kik me wether personal mail or message about the number of that tax um going to work on it even if um not un official of the same now we are too jalala i can say. Afteral um not not happy with my TRL let us be serious.
 
Nakubaliana nawe. Swala la msingi sana umeeleza.

Ila sasa, unataka tufungue milango raia wa kigeni waingie nchini wafanye kazi watakayo? Nipe majina ya nchi zinazofanya huo upuuzi.

Wenzetu wana-incourage foreign workers waende kufidia pengo la uhaba wa skilled labor kwenye maeneo maalum, mfano madaktari. Tunahitaji manesi na madaktari zaidi ili tuishi kwa afya. Tunahitaji waalimu ...kuna maeneo mengi tu.

We don't need unskilled labor as we already have enough of those. Perhaps we should think about moving some of our unskilled labor to China; that would be cool - itapunguza msongamano kwenye magereza yetu.
Tunahitaji kuchuja Chinese criminals wanaokimbia mkono wa sheria huko watokako.

Foreigners waje, wafanye kazi kwenye makampuni ya watanzania, sio waanzishe makampuni yao. Au kama ni makampuni yao (mfano kwenye construction) sheria iwalazimishe wafanye kazi jointly na locals.

Usimamizi wa sheria zilizopo ni hovyo. Wafanyakazi serikalini na taasisi zake wamekuwa mstari wa mbele kuingia ushirika na wageni kufanya mambo kinyume na sheria. Magogo kiasi gani yametoroshwa? Nyara kiasi gani wamekomba? ...You name it!

Mfano mdogo tu kuhusu sheria:
In Malaysia: Foreign workers can only work for five years
SOURCE: http://whiteglove.com.my/index.php?option=com_content&task=view&id=197&Itemid=47

Picture that! Jiulize kwa nini wenzetu wameweka sheria ya namna hiyo.

I agree with you kuwa sheria zilizopo/ziwekwe kwa ajili ya kuwalinda watanzania.

Lakini naomba kutoa onyo kuwa wimbi la mabadiliko duniani hatuwezi kulizuia kwa kuweka sheria, the real forces ndiyo zitakazoamua nini kifanyike.

Tunapojifananisha na sehemu zingine kama vile Malaysia, jaribu kuangalia wamalaysia ni wachapa kazi kiasi gani? Je uchumi wao uko vipi? Nafikiria Malaysia sio nchi ya kujifananishia na sisi kwani wao wanauchumi mzuri kwahiyo wanaweza kudictate some terms za mabadiliko lakini pia siyo zote.

Kitu cha msingi ni kuelewa kuwa Tanzania kama nchi haina ubavu wowote wa kuzuia mabadiliko yanayotokea hapa duniani. Kwa hiyo basi, tuondoke kwenye upande wa kufikiria everything will be ok kwa kuweka sheria za kuwazuia, badala yake tuumize vichwa ni kwa jinsi gani tutatumia hizo fursa za utandawazi kwa ajili ya kujijenga kiuchumi zaidi.

Dunia haina huruma, kila mtu ni lazima ahangaike na huko tunakokwenda wahangaikaji ndiyo watazidi kuingia Tanzania tena kwa uhalali kabisa na kutuacha sisi tunaweka sheria za kuwazuia bila ya mafanikio.

Sera za WTO zinataka kuifikisha dunia mahali ambapo kila mtu awe na fursa sawa ya kufanya biashara yeyote mahali popote pale duniani bila ya kujali utaifa wake. Kama waliweza kutuleta mfumo wa vyama vingi unadhani hili litawashinda? Tutafute nafasi zetu mapema badala ya kulalamika, malalamishi hayatasikilizwa once mfumo tusioutaka utakapokuwa unafanya kazi zake in full swing. Hakuna cha Rais, Bunge wala serikali itakayoweza kuzuia, sana sana ndiyo itakayokuwa inahimiza wananchi wakubaliane na mfumo huo.

"Kama huchukui hatua sasa basi utakuja kujuta baadae"
 
Je tatizo la msingi hapa ni nini? Je ni huyu taxi driver mchina au ofisa wa serikali aliyemruhusu kufanya hiyo biashara? Je tukiwafukuza wachina na wageni wengine wote tatizo litakuwa limekwisha? Kumbuka kwamba Dar-es-salaam ina watu wengine wengi toka nje ya nchi wakiwemo wakenya, waganda, waingereza, wacongo, wanigeria nk.

Mimi nadhani tatizo la Tanzania ni watanzania wenyewe hii inajumuisha watawala wetu na sisi watawaliwa. Soko HURIA lina taratibu zake na Serikali inatakiwa kusimamia soko hili kwa mujibu Katiba, sheria, sera na taratibu zinazoeleweka ili liweze kuleta manufaa kwa wananchi.

Kwa bahati mbaya badala ya kuanzisha soko HURIA viongozi wetu, kwa sababu zao binafsi za kifisadi, walianzisha soko HOLELA lisilokuwa na sheria wala taratibu zinazoeleweka na wala msimamizi.

Huwezi kuwa na Katiba ya nchi inayohuribi msingi wa UJAMAA halafu ukaendesha mambo kwa utaratibu wa SOKO HURIA. Huu ni mkanganyoko wa kisera na unatoa ombwe la watu kufanya mambo wanayotaka kwa faida zao wenyewe. Hivi sasa kwenye Ujamaa hatupo, kwenye Ubepari hatupo, kwenye Soko Huria hatupo - yaani tupotupo tu.

Ni lini mara ya mwisho tulimsikia kiongozi akiongelea masuala ya UKOLONI MAMBOLEO hapa Tanzania? Je ina maana ukoloni mamboleo umekwisha dunia hii? Je huu unaoitwa utandawazi siku hizi siyo ule ukoloni mamboleo ila ikiwa na sura na mavazi mengine? Tumejiandaa vipi kusimamia raslimali zetu kama nchi katika huu mfumo unaotawaliwa na ukoloni mamboleo?

Ninavyoelewa ukoloni mamboleo ni mbaya kuliko ukoloni mkongwe kwani umewageuza watawala wetu kuwa MAKUWADI wa raslimali za nchi katika soko huria.

Mimi binafsi sipingi ujio wa wafanyakazi wataalamu toka nje ya nchi ili mradi tu wazingatie sheria, taratibu na sera za nchi ambazo ama hazipo kwa sasa au zipo lakini zinaweza kubadilishwa kwa kitu kidogo. Hawa wageni ni muhimu hasa kama sehemu wanazokuja kufanya kazi zina upungufu mkubwa wa utaalam na uzoefu na kuna utaratibu wa kuwafundisha wataalamu wa nyumbani ili baadaye tusihitajike kuleta watu toka nje.
 
Tata,
Mawazo yako mazuri ila ninasikitika kusema kuwa unachokiongelea hakipo sasa hivi duniani. Wageni watakuja Tanzania kama kuna vitu vya kuwavutia kutengeneza faida zaidi na zaidi. Hii habari unayosema kuwa kwani hatuweki sheria za kuwafnya wafuate taratibu kama unavyozifikiria wewe, hilo ni jambo 'tata' kwani serikali yako ni signatory katika mikataba kadha wa kadha ikiwemo hiyo ya kufungua milango ya biashara huria. Dunia inaendeshwa kama shughuli zinavyoendeshwa mtaani sidhani kama unaweza kuwakataza wakazi wa mtaa wa pili wasipite au kutumia mtaa wenu.

Hawa wageni ni muhimu hasa kama sehemu wanazokuja kufanya kazi zina upungufu mkubwa wa utaalam na uzoefu na kuna utaratibu wa kuwafundisha wataalamu wa nyumbani ili baadaye tusihitajike kuleta watu toka nje

Hicho ulichoandika hapo juu unaongelea msaada kutoka serikali moja kwenda nyingine. Sasa hivi hata hao wanaotoa msaada wawakilishi wao (wabunge) wanataka wananchi wao wafaidikie na misaada hiyo. Kwa hiyo kinachofanywa ni kuwekeza kwa malengo ya kupata faida na wala siyo kukufundishia watu wako.

Misaada ambayo haina masharti magumu ambayo watakufundishia watu wako ni ile kukabiliana na uharibifu wa mazingira ya dunia kwani ukiimarisha hapa na wao wanakuwa salama.
 
Back
Top Bottom