China yasaidia Afrika kuingia katika zama za kidijitali

China yasaidia Afrika kuingia katika zama za kidijitali

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
169
Reaction score
287
3781300760a552e87f6c8d2318085564.png
Katika enzi ambapo utandawazi na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda yanapokutana, mageuzi ya kidijitali yamekuwa nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo. Kwa bara la Afrika, mageuzi ya kidijitali si kama tu ni fursa ya kihistoria ya kutimiza maendeleo endelevu, bali pia ni njia kuu ya kutekeleza Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na mifumo ya ushirikiano wa hali ya juu ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia moja, na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, pande hizo mbili zimeendelea kupanua ushirikiano katika uwanja wa kidijitali. Kuanzia kuharakisha ujenzi wa miundombinu ya kidijitali, hadi kujenga majukwaa ya huduma za biashara ya mtandaoni na kutoa mafunzo kwa watu wenye vipaji, China inazisaidia nchi za Afrika kuziba pengo la kidijitali, ili kutimiza maendeleo endelevu.

Kwa muda mrefu, miundombinu dhaifu imezuia maendeleo ya uchumi wa kidijitali barani Afrika, lakini ushirikiano kati ya makampuni ya China na washirika wao wa Afrika unabadilisha hali hii. Mwezi Novemba mwaka jana, ujenzi wa kebo ya 2Africa iliyoko chini ya bahari, uliotekelezwa na kampuni ya China Mobile International Limited pamoja na mashirika mengine ya kimataifa, ulikamilika. Kebo hiyo yenye urefu zaidi ya kilomita 45,000, itaunganisha Afrika na zaidi ya nchi na maeneo 33 katika Mashariki ya Kati, Ulaya, na Asia. Inakadiriwa kuwa kebo hiyo itachangia faida takriban dola bilioni 36.9 za Kimarekani kwa Afrika, na kutoa msingi imara kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa kidijitali wa bara hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni nyingi za teknolojia za China zimeanzisha ushirikiano na nchi za Afrika. Kampuni hizo, si kama tu zimeleta teknolojia mpya na vifaa vipya vinavyowezesha matumizi ya vifaa vya kidijitali barani Afrika, bali pia zimeleta seti kamili ya “suluhisho za Kichina” katika kuharakisha kuanza kwa “zama ya kidijitali” barani humo.

Mwaka jana, Kampuni ya Huawei ya China ilitangaza uzinduzi rasmi wa Kituo cha Huawei Cloud huko Cairo, mji mkuu wa Misri, na kutoa zaidi ya aina 200 za huduma, ikiwa ni pamoja na majukwaa ya AI, na data kubwa. Baadaye kampuni hiyo pia inapanga kutambulisha teknolojia nyingine mpya zikiwemo modeli ya akili bandia, modeli ya lugha kubwa ya Kiarabu, na mfumo wa kanzidata kwa Misri.

Mbali na miradi hiyo ya “hali ya juu”, kampuni za China pia zinazingatia ngazi ya mashina ili kuwasaidia watu wa kawaida barani Afrika kunufaika na teknolojia za kisasa.

Hivi sasa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na miundombinu duni, watu wengi bado wanatumia mtandao wa 2G wa mawasiliano ya habari, na hata baadhi ya watu wanakosa huduma ya umeme. Katika miaka ya hivi karibuni, Kampuni ya Zhongteng ya China imejenga au inajenga miradi 22 ya umeme ya nishati mpya katika nchi mbalimbali barani Afrika, zikwemo Niger, Ethiopia, Nigeria, na Tanzania, na kuboresha kwa kiasi kikubwa kiwango cha upatikanaji wa umeme katika vijiji vya mbali, na kunufaisha zaidi ya watu milioni 30. Kampuni ya ZTE ya China imesaidia Misri kuongeza kasi ya mtandao kwa zaidi ya mara kumi, na kuwawezesha idadi kubwa ya Wamisri kutumia mtandao wa kasi ya juu.
 
Back
Top Bottom