China yaomba kujenga kituo cha jeshi Rwanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

China yaomba kujenga kituo cha jeshi Rwanda

Discussion in 'International Forum' started by Mtu wa Pwani, Oct 25, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  China yaomba kujenga kituo cha jeshi Rwanda Send to a friend Monday, 25 October 2010 08:37 0diggsdigg

  BEIJING, China
  NCHI ya China na Rwanda wamekubaliana kushirikiana kikamilifu katika masuala ya kijeshi.
  Nchi hizo ambazo zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia kwa miongo kadhaa sasa ingawa ushirikiano wa kijeshi umeanza baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

  Habari zinasema kuwa, hatua hiyo imekuja baada ya Mawaziri wa Ulinzi wa nchi hizo mbili kukubaliana kwa kupanua wigo wa masuala ya kijeshi ndani ya nchi hizo.
  Wakizungumza mjini Beijing nchini China viongozi hao wamesema kuwa ushirikiano huo utapanuka zaidi na kuhusisha safari za mara kwa mara za maofisa wa kijeshi wa pande mbili hizo katika miji ya Kigali na Beijing.

  Habari zinasema kuwa katika makubaliano wa ushirikiano huo, China ilipendekeza kujenga kituo cha kijeshi nchini Rwanda.
  Aidha, kwa upande wa waziri wa Ulinzi wa Rwanda James Kaberebe ameitaja ziara yake nchini China kuwa yenye mafanikio makubwa.
  Rwanda wiki kadhaa zilizopita iliipinga ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusiana na
  matukio kuanzia mwaka wa 1993 hadi mwaka wa 2003.

  Ripoti hiyo ilikuwa inasema kuwa wanajeshi wa Rwanda wamehusika na mauaji ya kimbari wakati wa mapigano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
  Waziri wa sheria wa Rwanda, Tharcisse Karugarama, alisema Umoja wa wa Mataifa uliichoma kisu mgongoni Rwanda na haupaswi kuchapisha ripoti hiyo isiyokuwa na ukweli wowote.

  Rwanda inachangia maelfu ya wanajeshi katika kikosi cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
  Ripoti hiyo, ilisema kuwa maelfu ya Wahutu wakiwemo wanawake, watoto na wazee waliuawa na Jeshi la Rwanda lenye askari wengi wa kabila la Kitutsi.
  Ripoti hiyo vile vile inaorodhesha ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na vikosi vya nchi nyingine zilizoshiriki kilichokuja kujulikana kama ''Vita vya kwanza vya Afrika''.

  Ripoti kamili ya shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa itachapishwa hivi karibuni. Ingawaje mgogoro huo umemalizika rasmi, hali katika eneo la mashariki mwa Congo lililopakana na Rwanda bado ni ya wasiwasi.

  China yaomba kujenga kituo cha jeshi Rwanda
   
 2. bona

  bona JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  thread haijaonysha wazi kama china itawajengea rwanda au china itajenga kituo chake na rwanda iwe kama base tu kama inavyofanya marekani duniani kote!
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  East+cento afrika twafwa, ndani ya nchi ya huyu assin kuwa military base ya strong nation, majirani wajiandae.
   
Loading...