China yalikubali rasmi Kanisa Katoliki

China yalikubali rasmi Kanisa Katoliki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
China imesema makubaliano ya muda yamefikiwa na uongozi wa Vatican juu ya kuteuliwa kwa maaskofu na kutafungua ukurasa mpya kati ya mahusiano ya China-Vatican yakimaliza miongo mingi ya kutofautiana.

Katika maoni yaliyowekwa katika tovuti yake, China imelitambua rasmi Jumapili, kanisa Katoliki, na kusema “kwa moyo mkunjufu imeafiki” mkataba uliosainiwa Jumamosi na kuahidi “kuendelea kufuata njia inayoafikiana na jamii ya kisoshalisti, chini ya uongozi wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CCP).

Lakini, idadi ya Wakatoliki milioni 12 wanaokadiriwa kuwapo nchini China, wamegawanyika juu ya mkataba huo, wakati kanisa lisilo rasmi likiwa linamfuata Kiongozi wa Kanisa Katoliki. Kadinali mstaafu wa Hong Kong Joseph Zen amekataa makubaliano hayo na kusema ni usaliti uliyofanywa na Vatican.

Brian Lucas ni Mkurugenzi wa taifa wa Taasisi ya Kikatoliki, ambayo ni Jumuiya ya misaada ya Wakatoliki ya Australia. Ameiambia VOA hili limekuwa suala gumu na maoni ya pande zote; wale wanaounga mkono makubaliano hayo na wale wanaokosoa wanachukulia kuwa ni jambo jepesi.

Vatican ambayo tayari imewatambua maaskofu kadhaa walio teuliwa na serikali ya China, wameuita mkataba huo ni wa kiuchungaji na siyo wa kisiasa.

Katika tamko lake, Vatican imesema kuwa mkataba huo “ni matunda ya maridhiano ya pande mbili ya hatua baada ya hatua,” na wanatarajia itapelekea kuwepo muungano wa Wakatoliki wote nchini China.


Vatican Defends Upcoming China Deal Against 'Drastic' Critics
 
Marko 16:15, Luka 14:23, Mathayo 28:19-20, Matendo 1:7-8 NB: Biblia ndio jibu, hakuna awezaye kuzuia neno la Mungu kuhubiriwa na hakika kila goti litapigwa Warumi 14:11 Bwana Yesu asifiwe sana. Mbarikiwe sana wana JF.
 
China inaenda kuanguka..
!
Mkuu wachina sio kama sisi serekali ndio inateu hao masikofu Mungu wa wachina ni serekali yao !
kucheza nao inatachukuwa miaka mingi sana labda adi Yesu arudi !!
 
Asilimia kubwa ya wachangiaji mnachangia msichokielewa, hata aliyeandika kichwa cha habari kaandika kishabiki, kichwa cha habari kilipaswa kuwa "Uchina na Vatcan wamekubaliana" maana kila mmoja ana vitu ambavyo mwenzie kavikubali kuvitekeleza, suala la kumchagua askofu mfano wamekubalina atachaguliwa na makanisa husika kwa kusaidiana na serikali halafu majina yatapelekwa kwa Papa kusibitishwa, kwahiyo unaona ni namna gani china bado inadhibiti kanisa hilo.
 
Mkuu wachina sio kama sisi serekali ndio inateu hao masikofu Mungu wa wachina ni serekali yao !
kucheza nao inatachukuwa miaka mingi sana labda adi Yesu arudi !!
Jesuit wamehusika hapo
 
Asilimia kubwa ya wachangiaji mnachangia msichokielewa, hata aliyeandika kichwa cha habari kaandika kishabiki, kichwa cha habari kilipaswa kuwa "Uchina na Vatcan wamekubaliana" maana kila mmoja ana vitu ambavyo mwenzie kavikubali kuvitekeleza, suala la kumchagua askofu mfano wamekubalina atachaguliwa na makanisa husika kwa kusaidiana na serikali halafu majina yatapelekwa kwa Papa kusibitishwa, kwahiyo unaona ni namna gani china bado inadhibiti kanisa hilo.
Kupenyeza injili huko si kitu kirahisi. Kanisa Katoliki limepenya sehemu nyingi ngumu kwa mbinu za baadhi ya makubaliano ambayo mwisho nchi hizo zimejikuta zikiruhusu ukristo bila kujua.

Huko uarabuni pia kuna kazi nzito inaendelea, ukiwa mfatiliaji wa jinsi kanisa linavyojipenyeza kwenye hizi nchi zisizotaka kusikia kabisa Ukristo utachoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom