China yakanusha kuipeleleza AU

China yakanusha kuipeleleza AU

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
Serikali ya China imekanusha kuwa ripoti iliyotelewa na gazeti binafsi la Ufaransa la Le Monde kuwa imekuwa ikifanya upelelezi dhidi ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) yaliopo jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Taarifa hiyo ilidai kuwa kwa muda wa miaka 5, habari kutoka jengo la AU, lililojengwa na Wachina, zilikuwa zikipelekwa jijini Shanghai usiku wa manane.

Balozi wa China katika Umoja wa Afrika, Kuang Weili, alitaja ripoti hio kuwa "isiyo na mantiki" na "ya kupotosha."

Pia alitia shaka kwenye siku ripoti hio ilitolewa, ambapo ilitolewa siku moja kabla ya viongozi wa Afrika kuanza mkutano wao wa mwaka katika makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Jengo hilo lenye gorofa 20 liligharimu dola za Marekani milioni 200 na limekuwa makazi ya bodi hiyo ya Bara la Afrika tangu mwaka 2012.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hao WAFARANSA Nao ili waonekane wema ndio wanasema ya wenzao? Wao na ile France Afrique bado mpaka leo wanayo, ila nyani haoni....

Afrika tutaijenga wenyewe au tutaibomoa wenyewe !!!
 
Yaani Mtu akujengee na akukabidhi tu hivihivi, thubutu.

Ila Waafrica kazi tunayo, sasa hapo kinachoendelea ni malumbano kati ya France na China, sie tupo Mtu kati, tunageuka kwa France akiongea, tunageuka kwa China akiongea, sidhani hata kama tuna cha kuchangia.
 
Serikali ya China imekanusha kuwa ripoti iliyotelewa na gazeti binafsi la Ufaransa la Le Monde kuwa imekuwa ikifanya upelelezi dhidi ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) yaliopo jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Taarifa hiyo ilidai kuwa kwa muda wa miaka 5, habari kutoka jengo la AU, lililojengwa na Wachina, zilikuwa zikipelekwa jijini Shanghai usiku wa manane.

Balozi wa China katika Umoja wa Afrika, Kuang Weili, alitaja ripoti hio kuwa "isiyo na mantiki" na "ya kupotosha."

Pia alitia shaka kwenye siku ripoti hio ilitolewa, ambapo ilitolewa siku moja kabla ya viongozi wa Afrika kuanza mkutano wao wa mwaka katika makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Jengo hilo lenye gorofa 20 liligharimu dola za Marekani milioni 200 na limekuwa makazi ya bodi hiyo ya Bara la Afrika tangu mwaka 2012.

Chanzo: BBC Swahili
Huyo alotoa ripoti aliipataje bila kupeleleza?
 
Yaani Mtu akujengee na akukabidhi tu hivihivi, thubutu.

Ila Waafrica kazi tunayo, sasa hapo kinachoendelea ni malumbano kati ya France na China, sie tupo Mtu kati, tunageuka kwa France akiongea, tunageuka kwa China akiongea, sidhani hata kama tuna cha kuchangia.
Mazuzu kabisa sisi. Ila viongozi wetu ndio mazuzu kuliko sisi
 
Hawawezi kukubali kamwe na AU hawato washutumu kwa kufanya udukuzi.
Lakini chini ya Cybersecurity team kutoka Algeria hawatoweza kudukua tena. Hii ni baada ya server walizofunga wachina kubadilishwa.
 
Yaani Mtu akujengee na akukabidhi tu hivihivi, thubutu.

Ila Waafrica kazi tunayo, sasa hapo kinachoendelea ni malumbano kati ya France na China, sie tupo Mtu kati, tunageuka kwa France akiongea, tunageuka kwa China akiongea, sidhani hata kama tuna cha kuchangia.

Umasikini mbaya sana.
 
hizi ni propaganda za kuichafua china kwa kuichonganisha na africa baada ya kuona china inakuja kwa kasi katika uwekezaji africa
 
Mazuzu kabisa sisi. Ila viongozi wetu ndio mazuzu kuliko sisi
Sisi ni mazuzu kuliko viongozi wetu. Sababu mtu asiye zuzu kamwe hatokubali kutawaliwa achilia mbali kuongozwa na zuzu.
Waafrika wengi ni first class zuzus
 
Fatilieni vizuri China ilishawahi kuipa Ofisi ya Bunge la Tanzania msaada wa computer kadhaa na zilipokelewa na Anna Makinda.

No free lunch in Shithole land.
 
Back
Top Bottom