China yajibu mapigo-Yapandisha kodi kwa bidhaa za USA

jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
29,505
Points
2,000
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
29,505 2,000
China yalipiza kisasi kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani

China imesema leo kuwa itaongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani za thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni mosi, katika hatua ya kujibu duru ya karibuni ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China na mipango ya Marekani kuzilenga bidhaa zote zinazoingizwa nchini mwake kutoka China.

Tangazo hilo limekuja baada ya mazungumzo ya karibuni kabisa ya biashara kati ya Marekani na China kumalizika Ijumaa bila makubaliano, na baada ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China za thamani ya dola bilioni 200.

Licha ya hatua hiyo ya kulipiza kisasi, China imeonekana kutoa muda zaidi wa hadi Juni mosi. Ushuru mpya utazilenga bidhaa kadhaa za Marekani kuanzia asilimia tano hadi 25. Jibu la China limetangazwa mara tu baada ya Trump kuionya kutolipiza kisasi.

Awali, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Geng Shuang alisema kuwa China hitawahi kusalimu amri kwa shinikizo la kimataifa.

==================

China has decided to impose tariffs of 25 percent, 20 percent and 10 percent on certain U.S. products starting June 1, announced the Customs Tariff Commission of the State Council in a statement issued Monday.
The tariffs will be targeting U.S. goods worth 60 billion U.S. dollars, the statement said, adding that the products under five percent tariff cap would not be affected by this round of tariffs.

SOURCE: CGTN
 
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
1,357
Points
2,000
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
1,357 2,000
Wewe umesoma uchumi gani?, mnunuzi akikataa kununua bidhaa zako unayeumia ni wewe muuzaji soma 'US - china tariff war'
Kumbuka bidhaa karibia zote zinazotoka china kwenda marekani ni za wamarekani wenyewe na sidhani kama wataweza kuzipiga marufuku maana wakifanya hivyo itakua ni kuziua company zao wenyewe

Hapa tunazungumzia company kuanzia hp,dell,apple,textiles

Company kubwa zote za USA zinazalishia bidhaa zao china na bidhaa zikitoka china na kwenda usa zinahesabika kama imported goods ilhali ni bidhaa zao wenyewe wamarekani na zinawaletea faida vile vile wakina apple na wengineo na kadiri ushuru unavyozidi consumers wamarekani nao wanapata mzigo mkubwa vile na china nao watapunguza export

Hapa mkuu hakuna atakaye win kwenye hii battle,hapa nilimjibu jamaa kwa nini china amerespond tarrifs ndogo kwa USA ni kwa sababu tu hawa wana balance of trade isiyo sawa yani kuna mmoja anapeleka bidhaa nyingi kwa mwenzake kuliko mwingine
 
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
1,357
Points
2,000
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
1,357 2,000
Wewe umesoma uchumi gani?, mnunuzi akikataa kununua bidhaa zako unayeumia ni wewe muuzaji soma 'US - china tariff war'
Marekani hawezi kukataa kununua bidhaa zake mwenyewe

Kwa akili yako marekani na wamarekani wanaweza kukataa kununua apple products au hp computers au hata nguo za michezo zile nike?
 
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
1,357
Points
2,000
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
1,357 2,000
Mkuu huo Ni uchumi wa wapi, lazima huyo mwalimu wako alikufa kabla hujamaliza syllabus.

Mfano mdogo: Tanzania tunaingiza magari kutoka Japani, je tunapata mapato yeyote Kama nchi kwa maana ya Kodi na too zingine? Je Japan ikikataa kutuuzia au serikali ya Tanzania ikikataa kununua kutoka Japan Kuna hasara tutakayopata?

Naomba majibu
Itakua uchumi alifundishwa na mwalimu wa kemia
 
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2015
Messages
4,208
Points
2,000
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2015
4,208 2,000
Kuna watu bilioni moja kule alafu usizani china inaukubwa kama dar hadi bukoba hapana aisee kuna sehemu unaenda na ndege hata masaa manne hapa kwetu sehemu mbali ni saa moja tu kwa ndege
Purchasing power!
 
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
1,357
Points
2,000
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
1,357 2,000
Trump anachofanya Ni.kulinda soko la viwanda vya ndani mchina anatishia soko la viwanda vya ndani.Mchina soko lake la ndani hana shida ya kulinda wachina hupenda vyao yeye anahangaika na exports tu.Soko la viwanda vyake vya ndani Hana tatizo.Je Vita hi hasa anaumia Nani? Jibu Ni.mmarekani wa kawaida sababu vitu vya China vizuri alikuwa akivipata Bei nafuu kuliko vinavyozalishwa marekani sababu China Kuna low cost of production wakati marekani Kuna high cost of production .Hivyo Bei za bidhaa za China kuwa chini.
Sema kitachomkwamisha ni kwamba viwanda vingi vikubwa vya marekani vipo china labda akitaka awe sawa hivyo viwanda ni kuvirudisha nyumbani ila kuzidi kuongeza tarrifs ni kuwaumiza tu consumers wa marekani na vile vile nilisikia kwamba marekani inataka kuhamimishia viwanda vyake india na ikifanya hivyo yatakua ni yale yale tu yani karuka mkoja na kakita nyesi maana na india nayo itaendelea na ita acquire technology na USA tena itaanza kuona wivu kama ilivyo kwa china

Hapa solution ni kuhamishia viwanda vyote virudi kwao na hapo ndio waanze kushindana kufanya biashara na kwa jinsi usa ilivyo soko la ushindani kwao litakua gumu sana bidhaa zao ni ghali sana kama watazalisha wenyewe.
 
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
1,357
Points
2,000
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
1,357 2,000
Kwenye hii Vita wote wanaumia ila atakaeumia zaidi ni China sababu China anauza sana Marekani kuliko Marekani anavyouza China hapa tunaweza sema Marekani ni mnunuzi ilhali China ni muuzaji. Mnunuzi akikataa kununua bidhaa hapa atakaethirika zaidi ni muuzaji sababu mnunuzi anaweza kwenda kununua hizo bidhaa mahali pengine tofauti na muuzaji ambae itakua ngumu kwa yeye kupata solo lingine kama lile kwanza.

Kwenye hili tifu China ataishiwa silaha mapema sababu yeye hanunui sana toka Marekani wakati Marekani wana silaha nyingi ikiwemo bado kuna $350bn ya bidhaa hazijaongezewa ushuru.
Kingine Trump akiongeza ushuru kwenye bidhaa za China atafanya bidhaa za Marekani ziwe competitive na zile za China sababu zote zitakua bei moja au za China zitakua ghali zaidi kuliko zile za Marekani.

China akisema adevalue fedha yake hii pia ina madhara kwake ikiwemo kuongezeka kwa Deni lake la taifa au Marekani inaweza tena ushuru kwenye hizo bidhaa za Uchina kulipiza kisasi

China labda aamue kudump treasuries bond za US,hii nayo bado itamwathiri yeye kuliko US japo wote wanaumia sana. Na akiamua kuzidump ataenda kuziwekeza tena wapi?!
Kudump treasury ni last resort kabisa na sidhani kama china watafanya hivyo kwa sasa na ikitokea wamefanya italeta impact kubwa sana kwa pande zote na usa ki ukweli haita kopesheka kabisa na nchi nyingi zita dump us treasury.
 
hindustan

hindustan

Senior Member
Joined
Oct 15, 2014
Messages
158
Points
250
hindustan

hindustan

Senior Member
Joined Oct 15, 2014
158 250
Kwanza nashukuru kwa kukiri wembe unakata kotekote.

Hapa we umeangalia upande mmoja tu. Hebu aangalie stock market Leo imepoteza 600points baada ya China tu kutamka. Calculate hizo point Ni sawa na billion ngapi?

Pili China hataki Vita hiyo ya biashara maana yeye ananufaika na soko la Marekani zaidi kuliko America.

Tatu usiishie kuangalia import/export tu uchumi wa China ukidorora dunia nzima itayumba including amerika.

Hebu fanya marejeo
Factors affecting demand and supply including Elasticityof demand and supply

Trade barriers regimes and it's effects

kisha fanya marejeo ya valuation and devaluation of currencies and it's effects.

stock markets.... Kisha assess mchezo wa Trump na China.

ungekuwa mchezo mzuri nchi zote za Ulaya zingempa support Trump.

pia jiulize Nani mkopeshaji mkubwa duniani kwa Sasa?
Chief unamwaga nondo ambazo mtu asieujua uchumi anaweza kutokukuelewa...

Wote wataloose kwenye hii vita yao ya kiuchumi ila tatizo wengi wetu tumejaa ushabiki zaidi kuliko uhalisia
 
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2015
Messages
4,208
Points
2,000
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2015
4,208 2,000
China ndio nchi yenye purchasing power parity (PPP) kubwa kuliko nchi yeyote ile duniani.
Nimegoogle nikaona nikataka niyaondoe niliyoandika lakini umakonda ukaniingia na sikubali china haiwezi bila export!
 
13 mega pixel

13 mega pixel

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Messages
6,110
Points
2,000
13 mega pixel

13 mega pixel

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2013
6,110 2,000
Maana yake hapo atakaye athirika zaidi ni mchina maana anamtegemea zaidi mmarekanikuliko mmarekanian avomtegemea mchina
Wanaoumia zaidi ni wananchi wa marekani, kwa kuwa watapata bidhaa zile zile ambazo zinatengeneza china kwa gharama kubwa, production cost ya bidhaa per unit kwa marekani na china ni tofauti sana, china more cheap na matajiri wa US wamegoma kurudisha viwanda ndani kwa sababu ya gharama kubwa za uzalishaji, Marekani anaongeza tariff kwenye hadi malighafi za uzalishaji wkati mwenyewe hana uwezo wa kupata hizo malighafi kwa viwanda vya ndani...marekani hawezi kuepuka bidhaa za china
 
K

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Messages
2,092
Points
2,000
K

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2008
2,092 2,000
Kwenye hii Vita wote wanaumia ila atakaeumia zaidi ni China sababu China anauza sana Marekani kuliko Marekani anavyouza China hapa tunaweza sema Marekani ni mnunuzi ilhali China ni muuzaji. Mnunuzi akikataa kununua bidhaa hapa atakaethirika zaidi ni muuzaji sababu mnunuzi anaweza kwenda kununua hizo bidhaa mahali pengine tofauti na muuzaji ambae itakua ngumu kwa yeye kupata solo lingine kama lile kwanza.

Kwenye hili tifu China ataishiwa silaha mapema sababu yeye hanunui sana toka Marekani wakati Marekani wana silaha nyingi ikiwemo bado kuna $350bn ya bidhaa hazijaongezewa ushuru.
Kingine Trump akiongeza ushuru kwenye bidhaa za China atafanya bidhaa za Marekani ziwe competitive na zile za China sababu zote zitakua bei moja au za China zitakua ghali zaidi kuliko zile za Marekani.

China akisema adevalue fedha yake hii pia ina madhara kwake ikiwemo kuongezeka kwa Deni lake la taifa au Marekani inaweza tena ushuru kwenye hizo bidhaa za Uchina kulipiza kisasi

China labda aamue kudump treasuries bond za US,hii nayo bado itamwathiri yeye kuliko US japo wote wanaumia sana. Na akiamua kuzidump ataenda kuziwekeza tena wapi?!
Kumbuka pia wawekezaji wakubwa China Ni wamarekani ambao wanapeleka nyumbani ile faida wapatayo huko China.

Lakini pia Marekani hawezi kupata mbadala wa bidhaa zake zitokazo China. Mfani Apple, Hp, etc products Ni za kimarekani zinazozalishwa China, kusema zitakosa soko sehemu ingine duniani Ni uongo lakini mbadala wake kwa wamarekani pia haupo.

Hapa ndipo utaona Kila mmoja anamuhitaji mwenzake na maumivu kwa mmoja Ni maumivu kwa wote.

Hivyo Ni zero sum game
 
GreatSeal

GreatSeal

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,003
Points
2,000
GreatSeal

GreatSeal

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,003 2,000
Hapa china kwa vyovyote vile lazima asalim amri hamna jinsi
Kwenye hii Vita wote wanaumia ila atakaeumia zaidi ni China sababu China anauza sana Marekani kuliko Marekani anavyouza China hapa tunaweza sema Marekani ni mnunuzi ilhali China ni muuzaji. Mnunuzi akikataa kununua bidhaa hapa atakaethirika zaidi ni muuzaji sababu mnunuzi anaweza kwenda kununua hizo bidhaa mahali pengine tofauti na muuzaji ambae itakua ngumu kwa yeye kupata solo lingine kama lile kwanza.

Kwenye hili tifu China ataishiwa silaha mapema sababu yeye hanunui sana toka Marekani wakati Marekani wana silaha nyingi ikiwemo bado kuna $350bn ya bidhaa hazijaongezewa ushuru.
Kingine Trump akiongeza ushuru kwenye bidhaa za China atafanya bidhaa za Marekani ziwe competitive na zile za China sababu zote zitakua bei moja au za China zitakua ghali zaidi kuliko zile za Marekani.

China akisema adevalue fedha yake hii pia ina madhara kwake ikiwemo kuongezeka kwa Deni lake la taifa au Marekani inaweza tena ushuru kwenye hizo bidhaa za Uchina kulipiza kisasi

China labda aamue kudump treasuries bond za US,hii nayo bado itamwathiri yeye kuliko US japo wote wanaumia sana. Na akiamua kuzidump ataenda kuziwekeza tena wapi?!
 
ze kokuyo

ze kokuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Messages
6,405
Points
2,000
ze kokuyo

ze kokuyo

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2014
6,405 2,000
Kudump treasury ni last resort kabisa na sidhani kama china watafanya hivyo kwa sasa na ikitokea wamefanya italeta impact kubwa sana kwa pande zote na usa ki ukweli haita kopesheka kabisa na nchi nyingi zita dump us treasury.
Marekani hakopi,ila nchi zinanunua Deni lake. Hata Urusi inamiliki sehemu ya Deni la Marekani. Wanaoongoza ni China na Japan
 
ze kokuyo

ze kokuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Messages
6,405
Points
2,000
ze kokuyo

ze kokuyo

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2014
6,405 2,000
Kumbuka pia wawekezaji wakubwa China Ni wamarekani ambao wanapeleka nyumbani ile faida wapatayo huko China.

Lakini pia Marekani hawezi kupata mbadala wa bidhaa zake zitokazo China. Mfani Apple, Hp, etc products Ni za kimarekani zinazozalishwa China, kusema zitakosa soko sehemu ingine duniani Ni uongo lakini mbadala wake kwa wamarekani pia haupo.

Hapa ndipo utaona Kila mmoja anamuhitaji mwenzake na maumivu kwa mmoja Ni maumivu kwa wote.

Hivyo Ni zero sum game
Mbadala wa mnunuzi ni mkubwa ukilinganisha na wa muuzaji.
Hizo bidhaa zinazozalishwa China wawekezaji wakiona hawapati faida wanaweza kuamua kuhamisha viwanda vyao kwenye nchi nyingine za karibu Kama vile India, Indonesia,Taiwan,nk zikaenda Marekani.
Je kwa China?!
 
Ozzanne Issakwisa

Ozzanne Issakwisa

Verified Member
Joined
Mar 7, 2016
Messages
250
Points
250
Ozzanne Issakwisa

Ozzanne Issakwisa

Verified Member
Joined Mar 7, 2016
250 250
Kukiwa na vita ya kibiashara kati ya nchi mbili, kwa kutunishiana misuri kama ifanyavyo USA na China, basi asilimia kubwa yule ambaye amekuwa akiuza zaidi kwa mwenzake ndiye ataathirika zaidi.

Wabobezi wanasema USA ni mwagizaji mkuu wa bidhaa toka China. Pia hawahawa wataalamu wanasema pamoja na US kukaza msuri kwa China na kisha China kulipiza, bado dollar ya Kimarekani inazidi kupata nguvu. China hawezi kaza sana msuri kwa sababu yeye si mnunuzi mkubwa toka USA.

Wataalamu wanasema ingawa China inaweza kuathiri mauzo ya kampuni za USA zilizopo ndani ya China kama Apple na GM, bado iPhone zinazouzwa China zinazidi zile zinazouzwa USA na kampuni ya magari GM inauza magari zaidi nchini China kuliko USA.

Wataalamu waliomo humu labda watatujuvya zaidi.

China yalipiza kisasi kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani

China imesema leo kuwa itaongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani za thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni mosi, katika hatua ya kujibu duru ya karibuni ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China na mipango ya Marekani kuzilenga bidhaa zote zinazoingizwa nchini mwake kutoka China.

Tangazo hilo limekuja baada ya mazungumzo ya karibuni kabisa ya biashara kati ya Marekani na China kumalizika Ijumaa bila makubaliano, na baada ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China za thamani ya dola bilioni 200.

Licha ya hatua hiyo ya kulipiza kisasi, China imeonekana kutoa muda zaidi wa hadi Juni mosi. Ushuru mpya utazilenga bidhaa kadhaa za Marekani kuanzia asilimia tano hadi 25. Jibu la China limetangazwa mara tu baada ya Trump kuionya kutolipiza kisasi.

Awali, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Geng Shuang alisema kuwa China hitawahi kusalimu amri kwa shinikizo la kimataifa.

==================

China has decided to impose tariffs of 25 percent, 20 percent and 10 percent on certain U.S. products starting June 1, announced the Customs Tariff Commission of the State Council in a statement issued Monday.
The tariffs will be targeting U.S. goods worth 60 billion U.S. dollars, the statement said, adding that the products under five percent tariff cap would not be affected by this round of tariffs.

SOURCE: CGTN
 
mbalaka

mbalaka

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Messages
597
Points
1,000
mbalaka

mbalaka

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2017
597 1,000
Unajua china inapeleka bidhaa za thamani kiasi gani USA na USA inapeleka kiasi gani china?

Unataka china nao waweke hizo tarrifs za billion 200 na wakati hawajafika huko kwenye uthamani wa hizo bidhaa
Soko kubwa la mchina ni USA, So mchina anamhitaji zaid mmarekani kuliko mmrakani anavyomhitaji mchina.

Nope:
wote wataumia lakni mchina ataumia zaidi kuliko atakavyoumia USA.
 
mbalaka

mbalaka

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Messages
597
Points
1,000
mbalaka

mbalaka

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2017
597 1,000
Nyie hamjui Trump na matajiri wengine wanatafuta Global recession ili wapige pesa, wanajitahidi kuanzisha Vita na Venezuela au Iran kinachowashinda ni sababu ya kuweza kuvamia hizo nchi, na unaona mafuta yamepanda bei hiyo siyo bahati mbaya wakati mafuta yalipoteremka bei Uchumi wa Saudia na UAE ulitetereka hadi wakaachana na project kubwa. Jamaa wamemkamata Trump kaiwekea Iran na Venezuela vikwazo ili wao wauze mafuta kwa bei ya juu.
Ishu ya China na USA, mchina ataathirika lakini hatoumia jamaa wanajua kuvumilia katika shida, nachokiona kunakitu Trump anakitaka huko China haswa fursa kubwa za biashara.
Hii comment yko imenifikirisha zaidi.
 
Forum statistics

Threads 1,296,486
Members 498,655
Posts 31,249,917
Top