kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,154
Jeshi la China limetangaza kuwa, kuendelea kuwa mbaya hali ya mambo kuhusiana na usalama wa bahari ya eneo, machafuko katika eneo la Asia na Bahari ya Pasifiki na kadhalika misimamo tata ya rais mpya wa Marekani, inalilazimu kujiandaa kuingia vita tarajiwa na Marekani kuliko wakati mwingine wowote.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa jeshi la China wa Army Daily imesema kuwa, kwa kuzingatia siasa na matamshi ya uhasama ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na Rais Donald Trump wa Marekani, Beijing imeamua kujitayarisha kukabiliana kijeshi na nchi hiyo.
Ripoti hiyo ya jeshi la China imefafanua kuwa, msimamo wa Washington wa kuweka ngao ya makombora ya THAD nchini Korea Kusini, kuongeza idadi ya askari wake katika maeneo ya mashariki na kusini mwa bahari za Uchina na kadhalika kuanzisha mlingano mpya barani Asia, ni siasa ambazo zinaweza kuwasha moto wa vita wakati wowote.
Hivi karibuni pia Rais Xi Jinping wa China na ambaye ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi ya nchi hiyo alinukuliwa akisema kuwa, askari wa taifa hilo lazima wajiimarishe kuliko wakati mwingine wowote ule, kauli ambayo imetafsiriwa na weledi wa mambo kuwa ni maandalizi ya kijeshi kwa ajili ya kuingia vitani na Marekani.
Katika kampeni za uchaguzi wa Marekani kwa mara kadhaa Trump alitoa matamshi ya uhasama dhidi ya Uchina kiasi cha kuifanya Beijing kumtaja rais huyo mpya wa Marekani kuwa mwenye nia mbaya dhidi ya China.
Makomando wa jeshi la Uchina wakiwa katika maandalizi
source: Radio tehran