China yajenga mtandao wa kwanza wa mawasiliano ya habari wa Quantum

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,625
32,756
China yajenga mtandao wa kwanza wa mawasiliano ya habari wa Quantum wa ardhi na setilaiti duniani Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha China kimetangaza kuwa timu ya utafiti ya China imefanikiwa kutimiza ugavi wa ufunguo wa siri (Secret-Key) wa Quantum wenye umbali wa kilomita 4600, ambayo ni alama ya uzinduzi wa mtandao wa kwanza wa mawasiliano ya habari wa Quantum wa ardhi na setilaiti duniani.

Mtandao huo unatumia teknolojia ya leza OKD na saitilaiti kuunganisha watumiaji, ambao unaweza kusambaa kwenye eneo kubwa zaidi na kuwa na utulivu na usalama zaidi kuliko mtandao wa zamani.

Wajuvi mtusaidie kujua huu mtandao unafanyafanyaje kazi
 
Wakati vyuo vya wenzetu vikikazana kufanya tafiti huku kwetu mambo ni tofauti, maprofesa wa vyuo vikuu wako wanangoja wapewe nafasi za kisiasa na kugombea ubunge!!

Mbaya zaidi tunataka viwanda, sijui hivyo viwanda vitatoka wapi kwa mtindo huu!
 
Unatuwekwa mada kana kwamba wote tumesoma Physics na tunayajua hayo.

Haya tuanze Quantum ni nini?
Duh! Swali langu limelenga kujua tu hiki walichokigundua kitakuwa kinafanya kazi kwenye simu, TV, au wapi na kwa namna gani?
 
Wanakuzoom hapo.....kama upo bongo huo mnara wenyewe inawezekana ni wa huawei
 
Mkuu kumbe uvumbuzi huu ni maswala ya internet? Asante sana
 
Wakati vyuo vya wenzetu vikikazana kufanya tafiti huku kwetu mambo ni tofauti, maprofesa wa vyuo vikuu wako wanangoja wapewe nafasi za kisiasa na kugombea ubunge!!

Mbaya zaidi tunataka viwanda, sijui hivyo viwanda vitatoka wapi kwa mtindo huu!
Ni kweli mkuu,

Badala watumie vitivo vyao kufanya tafiti pamoja na wanafunzi wao wamekalia siasa tu.

Sijui tunakwama wapi kama Taifa.
 
jack ma kwani kauwawa?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreā€¦