Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,005
- 9,872
Rais wa China Xi Jinping ameahidi kutuma barani Afrika dozi bilioni moja za chanjo ya Covid-19 ili kusaidia kuziba "pengo la chanjo". Rais alitoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wa kilele wa China na Afrika.
Kati ya bilioni moja, dozi milioni 600 zitatoka China moja kwa moja huku milioni 400 zitatoka kwa vyanzo vingine kama vile maeneo ya uzalishaji yatakayofadhiliwa. China tayari imekuwa ikitoa dozi kwa nchi za Afrika.
Ahadi ya hivi majuzi inakuja huku kukiwa na kuenea kwa aina mpya ya virusi kwa jina Omicron ambayo iligunduliwa kwa mara ya kwanza kusini mwa Afrika.
BBC Swahili