China wazindua daraja refu lililotengenezwa kwa vioo

China wazindua daraja refu lililotengenezwa kwa vioo

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,982
China imezindua daraja la vioo linalounganisha vilele viwili vya milima katika eneo la Zhangjiajie kwenye Jimbo la Hunan.

Daraja hilo limeundwa kwa vipande 99 vya vioo vigumu, lakini ambavyo unaweza kujiangalia na kujiona ulivyo. Pia lina mita 430 (yaani kama viwanja vinne na kidogo vya mpira-urefu). Usanifu wake umefanywa na mtalaamu wa usanifu wa miundombinu wa Israel, Haim Dotanna.

Watu 8,000 tu wanaruhusiwa kupita kila siku katika daraja hilo na ni watu 600 pekee watavuka kwa wakati mmoja, ingawa watu 800 wanaweza kupita kwa wakati mmoja. Ni marufuku kupiga piga unapopita au kuwa karibu na daraja hilo na 'selfie' haziruhusiwi (ingawa wakati linazinduliwa waliruhusu selfie).

Pia huruhusiwi kupita na viatu vya 'kokoko' au vyovyote vyenye chuma na ukifika darajani hapo unavalishwa viatu maalumu vya kuvukia, vyako unaweza kwenye mkoba au begi.

Kupita katika daraja hilo ni kwa malipo na unafanya 'booking' mapema kwa kutoa dola 15.94 za Marekani.

WhatsApp Image 2016-08-21 at 7.21.57 AM.jpeg
WhatsApp Image 2016-08-21 at 7.21.49 AM.jpeg
WhatsApp Image 2016-08-21 at 7.21.49 AM(1).jpeg
 
Wa

Wanazalisha nini hao Cdm? CCM imejenga kwa nguvu za wana nchi wote tangu enzi za chama tawala. Majengo, viwanja vya michezo, hqs wote tulichangia.
Ruzuku na misaada mnayopata kutoka kwa wahisani mnafanyia kazi gani.
Miaka 24 bila hata jengo moja la ofisi kuu. Ifike mahali muone aibu.
Ndo maana baadhi ya watu wanawaita saccos
 
Kwetu bado tunahangaika na MATUNDO ya vyoo kwa wanafunzi wetu pamoja kaulimbiu ya nchi ya viwanda
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Kuna jamaa zetu wanaitwa cdm, kwa miaka 24 tangu waanze hawajawahi kuwa hata na jengo moja la ofisi.
Nadhan wakichukua nchi watakodi majengo yawe ikulu.
We ,ccm zaidi ya miaka 50 ktk utawala wenu hamjafanya lolote la maana
 
Kutangulia si kufika, wacha kwanza sisi tuzindue mafunzo ya polisi kupambana na UKUTA. Halafu tutajenga kama hilo la kwenda zenj.
 
Back
Top Bottom