China na Marekani zalegeza masharti ya kibiashara

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
China na Marekani zimeridhia kulegeza masharti ya kibiashara huku China ikisema itapitia upya na kuidhinisha maombi ya usafirishaji wa bidhaa yatakayoendana na kanuni zilizopo.

Marekani nayo ikiondoa hatua kali za kibiashara ilizoiwekea China.

Awali Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kutiwa saini mkataba wa kibiashara kati ya nchi yake na China na kugusia kwamba unajumuisha usafirishaji wa smaku na madini adimu kutoka Beijing kwenda Washington.

Tangu Trump aanzishe vita vya biashara na China mwezi Februrari, mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani yamekuwa katika mvutano wa kupandishiana ushuru ambao umevuruga masoko ya dunia.

Kwengineko Trump pia amedokeza kuwa huenda kukawa pia na makubaliano makubwa ya kibiashara kati ya taifa hilo na India.
 
Wakubwa hao wanajuana
 
Back
Top Bottom