China: Mwananchi ajichorea alama za barabarani

China: Mwananchi ajichorea alama za barabarani

Bahati furaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
3,077
Reaction score
1,439
Mtu mmoja raia wa China amepigwa faini baada ya kupatikana katika kamera akipaka rangi ishara mpya za barabarani ili kurahisisha safari yake kuwa rahisi.

Gazeti la Modern Express limeripoti kwamba mtu mwenye umri wa miaka 28 kwa jina Surnamed Cai, alipigwa faini ya Yuan 1000 mashariki mwa mji wa Lianyungang mkoani Jiangsu .

Alipatikana katika kamera mnamo mwezi Septemba 27 akiwa na mkebe wa rangi akipaka mistari mipya katika barabara ili kubadilisha mwelekeo wa trafiki na kuwaambia maafisa wa polisi kwamba alichukua hatua hiyo ili kupunguza tatizo la milolongo mirefu ya magari swala ambalo limekuwa likimchelewesha kila siku anapoelekea kazini.

Niliona kwamba barabara iliokuwa ikielekea moja kwa moja ilikuwa na mlolongo mrefu wa magari , huku barabara inayoelekea upande wa kushoto ikiwa na nafasi kubwa., aliambia maafisa wa polisi.

Nilidhani kubadilisha ishara hizo za babarabara kutarahisisha usafiri wangu kuelekea kazini.

Maafisa wa idara ya trafiki waliambia gazeti hilo kwamba walidhani kwamba tabia ya bwana Cai ilikuwa hatari na kwamba ingesababisha ajali.

Tayari wametuma wafanyikazi kuhadilisha ishara hizo za trafiki.

Hii sio mara ywa kwanza kwamba raia ametumia ujuzi wake wa sanaa kuweka ishara zao za barabara.

Mnamo mwezi Mei ,dereva mmoja mashariki mwa mji wa Zhejiang alipigwa faini baada ya kamera kumpata akichora eneo lake la kuegesha gari kwa kutumia chaki.

WA DAR, UBUNIFU HUO.
 
Aiseee ni nooma huyo angekua bongo angepeta no CCTV no what
 
Na huku kwetu hamna kamera ngoja vile vibao vya 30,40 na 50 nikacheze navyo....ole wake trafiki anisimamishe
 
Ungenogesha na picha bac
Najua thamani ya picha mkuu.
Wakatimwingine ukiona habari iliyostahili kuwa na picha haina basi chukulia labda alietoa post/taarifa amekumbwa na magumu fulani katika hilo.

trafic sign.jpg


Jamaa huyo hapo anaongezeaa njia ya kunyoosha.
 
Duh! Uchina Kila kitu kinaenda kichinachina
 
Back
Top Bottom