China kuzindua ndege yenye uwezo wa kukwepa RADA

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,692
China imeonesha ndege yake mpya ya kivita yenye uwezo mkubwa wa kukwepa rada na kushambulia maeneo magumu kufikika.

Ndege hiyo iliyopewa jina la Wing Loong II imetengenezwa kwa teknlojia ambayo inaifanya kuwa ngumu kuonekana kwenye rada au vifaa vingine vya kunasa ndege.

Ina uwezo wa kubeba kilo 400 pamoja na kuunganishiwa aina mbalimbali za makombora yatakayoiwezesha kufanya mashambulizi, na itakuwa inaongozwa na rubani mmoja ambaye atakuwa ardhini akitumia rimoti.

Nchi hiyo imeionesha ndege hiyo kwenye kipande cha video, na imeelezwa kuwa ndege hiyo imekusudiwa kwa ajili ya soko lake la nje la silaha.

Aidha, hatua hiyo ya kuionesha ndege hiyo imekuwa wakati ambapo China iko katika mpango wa kuiuzia Pakistani ndege 48 zisizo na marubani zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu.

The Indian Express imeripoti kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kusafiri angani kwa saa 20 bila kuongeza mafuta.

Msanifu mkuu wa ndege hiyo, Li Qidong amekaririwa na Xinhua akieleza kuwa ndege hiyo ya kivita ina uwezo wa kutua kwa dharura katika hali ambayo haikutarajiwa ikichagua yenyewe viwanja vya ndege vilivyo salama.

SISI NGOJA TUPAMBANE NA UPINZANI
231A5057wliiPARIS-800x445.jpeg
1704032_-_main.jpeg
 
mkuu comment yako haijaendana na uzi wako aisee,ila ungeshauri tu nini tufanye na sisi tuonekane katika ulimwengu wa technologia hizi ndgu,
 
Hizo rada za kukwepa walizotengeneza wa China wenyewe au nchi zingine. Technology inatofautia wanachokifanya China wezao wamekifanya zaidi ya miaka 10 iliyopita.
 
Siyo lazma Na sisi tuwe wagunduz, lazma kuwe na wagunduz+wanunuzi sasa nchi zote tukishughulika na ugunduzi mambo mengine yatafanywa na akina nan!!? Nchi yetu ina mambo meng ya kufanya isitoshe bado tulikuwa tumelala jiwe katuamsha tupo tunanawa uso wengne tunasugua meno kuna wachache wako bafuni wanaoga sasa ikitokea mtu tayar akawa jikoni anafanya yeke tutamshangaa sana....hatua kwa hatua huko tutafika
 
Hizi mbona mmarekani yupo nazo mda mrefu sana tu.. ndio zilizovamia makazi ya osama kule Pakistan. Tena zakwao zilikuwa ni chopper
 
wabongo tupo inst tunashindana kupost picha na kuangalia umbe, kweli tunasafairi ndefu
 
Kwenye armor industry china hana jipya yeye ni kukopi na kununua teknolojia.
Hivi vijamaa bana shida kweli.Lakini wansema hata ucopy vipi huwezi tengeneza kilicho sawa na original,sababu siri zake wanazijua wao.
 
China imeonesha ndege yake mpya ya kivita yenye uwezo mkubwa wa kukwepa rada na kushambulia maeneo magumu kufikika.

Ndege hiyo iliyopewa jina la Wing Loong II imetengenezwa kwa teknlojia ambayo inaifanya kuwa ngumu kuonekana kwenye rada au vifaa vingine vya kunasa ndege.

Ina uwezo wa kubeba kilo 400 pamoja na kuunganishiwa aina mbalimbali za makombora yatakayoiwezesha kufanya mashambulizi, na itakuwa inaongozwa na rubani mmoja ambaye atakuwa ardhini akitumia rimoti.

Nchi hiyo imeionesha ndege hiyo kwenye kipande cha video, na imeelezwa kuwa ndege hiyo imekusudiwa kwa ajili ya soko lake la nje la silaha.

Aidha, hatua hiyo ya kuionesha ndege hiyo imekuwa wakati ambapo China iko katika mpango wa kuiuzia Pakistani ndege 48 zisizo na marubani zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu.

The Indian Express imeripoti kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kusafiri angani kwa saa 20 bila kuongeza mafuta.

Msanifu mkuu wa ndege hiyo, Li Qidong amekaririwa na Xinhua akieleza kuwa ndege hiyo ya kivita ina uwezo wa kutua kwa dharura katika hali ambayo haikutarajiwa ikichagua yenyewe viwanja vya ndege vilivyo salama.

SISI NGOJA TUPAMBANE NA UPINZANI View attachment 904067View attachment 904068
Great leap forward.....hongera once best friend of Tanganyika.
 
HII NI DRONE
 
Back
Top Bottom