CHINA kumtunuku nishani ya juu ya urafiki Dkt. Salim Ahmed Salim

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
1569222205788.png

Octoba 1, 2019 kutakuwa na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuzaliwa taifa la Jamhuri ya Watu wa China. Maadhimisho hayo yamepewa uzito mkubwa na yatajumuisha matukio mbalimbali ikiwemo Gwaride kubwa ambalo halijawaji kutokea hapa China.

Vilevile wataonesha hatua kubwa waliyopiga ndani ya kipindi cha miaka 70 katika sayansi na teknolojia pamoja na nguvu za kijeshi. Katika ku revisit safari yao ya miaka 70 wameutambua mchango wa Tanzania katika maeneo mawili. Moja- mchango wa kuwawezesha kupatiwa kiti katika Umoja wa Mataifa na pili fursa waliyopata kutekeleza mradi wa kwanza wa ujenzi wa Reli nje ya nchi (TAZARA).

kutambua mchango wa Tanzania kuwawezesha kuingia UN- Rais wa China Mhe Xi Jinping atamtunuku Mhe Dr. Salim Ahmed Salim Nishani ya Juu ya Urafiki ya taifa la China. Dr Salim atakuwa Mwafrika wa kwanza kupatiwa nishani hiyo na mtu wa tatu kutoka nje ya China kupatiwa nishani hiyo.

Wengine waliokwishapatiwa nishani hiyo ni Rais wa Urusi Mhe Vladmir Putin- kutokana na mchango wa mkubwa wa Urusi kwa taifa la China katika miaka 1949-1970… waliwapa mikopo nafuu, mitaji, teknolojia na ufundi iliyowawezesha kupiga hatua.

Pia nishani hiyo amewahi kupewa Kiongozi wa Khazakstan Mhe DescriptionNursultan Äbishuly Nazarbayev kutokana na ujirani mwema na ushirikiano mkubwa katika nyanja za ulinzi na uchumi. Khazakstan inapakana na China (mpaka wao una urefu wa kilomita 1,782.75). Mizigo ya China inayosafirishwa kwenda Ulaya kwa treni, lazima ipitie Khazakstan- hiyo nchi hiyo ni strategic country kwa China.

Kwa upande wa mchango wa Reli ya TAZARA wachina wanaichukulia kuwa ni alama ya urafiki kati ya China na Bara la Afrika. Hivyo katika kutambua urafiki huo- viongozi wa taasisi za China-Tanzania Friendship Association na Tanzania Zambia Friendship Association wamealikwa kuhudhuria sherehe za miaka 70 na pia watashiriki katika gwaride rasmi la Nchi Rafiki wa kweli wa China katika kipindi cha miaka 70. Kutoka Afrika ni nchi mbili tu- Tanzania na Zambia.
 
La ukweli hapo ni kusaidiwa kupata kiti cha kudumu katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. La TAZARA iliwasaidia katika biashara ya shaba.
 
Namuona malaika mkuu akitaka hiyo nishani apewe yeye maana kila pongezi anataka apewe yeye
View attachment 1214006

Tuliiibiwa sana madini wakati Reli ya tazara inajengwa

Ugali Maharagwe umeharibu akili za watanzania
 
Chanzo kingine kinaonesha watu 6 toka nje ya Uchina wamewahi kupewa tuzo ya heshima miongoni mwao ni Dr. Salim A. Salim.

...Six foreigners were awarded the Friendship Medal for their great contributions to supporting China's socialist modernization, promoting exchanges and cooperation between China and foreign countries and safeguarding world peace.
They are Cuba's Raul Castro Ruz, Thai Princess Maha Chakri Sirindhorn, Tanzania's Salim Ahmed Salim, Russia's Galina Kulikova, France's Jean-Pierre Raffarin and Canada's Isabel Crook....

kutambua mchango wa Tanzania kuwawezesha kuingia UN- Rais wa China Mhe Xi Jinping atamtunuku Mhe Dr. Salim Ahmed Salim Nishani ya Juu ya Urafiki ya taifa la China. Dr Salim atakuwa Mwafrika wa kwanza kupatiwa nishani hiyo na mtu wa tatu kutoka nje ya China kupatiwa nishani hiyo.

Walikuwa wapi siku zote hizi, leo ndio wanakumbuka hili wakati Salim mgonjwa kitandani?
 
Ukiachilia mbali kupigia debe china waingie UN,DR Salim alisimama kidete kuhakikisha china inapewa kura veto
 
Huyu mzee kwa aliyoyafanya kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla,anastahiki kuheshimiwa zaidi ya heshima aliyonayo sasa. Kwa tuliokuwa tunafuatilia mambo tangu miaka ya 1970 watanielewa.
Punguza uongo, ameifanyia nini Tanzania zaidi ya kulitumikia tumbo lake na familia yake?!

Sio kila umaarufu wa mtu unamanufaa kwa nchi ya Tanzania.

Kaifanyia nini Tanzania to be specific, kama utapenda kujibu?!
 
Mchango wa salum ni mkubwa sana, bahati mbaya nchi zetu hatuna siku ya kuwaenzi watangulizi wetu na michango yao kwa nchi yetu, ni muhimu Kuwa Na siku ya mashujaa wa ujenzi wa uchumi wetu hata kuanzisha vipindi namashuleni watoto wetu wajue tuliko toka, Salum ukisikia masimulizi yake mwenyewe jinsi alivyokuwa anawajibika kwenye nafasi yake ya ubalozi huko China na mchango wake kwa ujenzi wa Reli ya Uhuru yaani Tazara, utajifunza umuhimu wa Kuwa na mabalozi makini kwa Maendeleo ya nchi yetu, China walijitolea kujenga reli ya Tazara tukiwa maskini Sana, lakini watu kama Salim mchango wao ni wakukumbukwa daima.Ushawishi wao kwa viongozi wawakati ule ulikuwa mkubwa, Mwalimu Nyerere alikuwa na watu makini Sana, Salim alikuwa kijana Sana nadhani ndiye aliyekuwa balozi mdogo kuliko wote walikuwa China kwa wakati huo, pia hata Tanzania alikuwa ndiye balozi mdogo kuliko wawakilishi wengine kwenye balozi zetu.
 
Yes, Time to celebrate baada ya kazi ngumu ya kulijenga Taifa lenu...hongereni sana wachina. Dunia imeshaanza kuwaelewa..ni muda wa nyie kutembea kifua mbele ...hata watoto wetu sasa tunawafunza kukijua kichina, tunaona fursa mbele.
 
Salim Ahmed Salim. Mwanafunzi mwaminifu wa JK Nyerere.
Mungu amtunze na kumjaria kila lililo jema
Unaweza kusema kijana wa Nyerere na mwanafunzi wa A.M.Babu gwiji la siasa kuwahi kutokea Afrika,na ndie muasisi wa uhusiano wetu na China
 
Waafrika viumbe wa ajabu sana, wakati hao wachina wanashrehekea maendeleo na kuvishana nishani za kufanikiwa katika nyanja ya teknolojia, sisi tunaenda kuvishwa nishani ambayo kwetu inaonekana kama ni ishara ya kushindwa.

Reli wamejenga wao, sisi ilikuwa ni kuiendesha tu na kuiboresha, lakini ajabu hata hilo limetushinda.
Hiyo nishani ni tusi walah!
 
Siku hizi Kina Mama hawabebi Mimba za kina Salim Ahmed Salim na kina Baba XY zao hazina Kina Salim

Kila tukijikunja tunatoa kina Harmorapa
 
Back
Top Bottom