Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Kampuni mbili za China zimekubali kujenga kituo cha viwanda jijini Tanga kitakachogharimu mabilioni ya fedha zikiwa jitihada za kuunga mkono mpango wa serikali wa kuifanya Tanga kuwa jiji la viwanda.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Daud Mayeji, alisema kuwa tayari kampuni hizo zimeshaingia mkataba na kwamba ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuanza mara moja Juni mwaka huu.
Mayeji alisema chini ya mpango kituo hicho kutajengwa viwanda mbalimbali vidogo na vya kati sambamba na upanuzi wa bandari ya Tanga kuiongeza kina chake na chuo cha ufundi kwa ajili ya kupata wataalamu na mafundi wa kufanyakazi katika viwanda hivyo.
Hata hivyo, alisema kuwa mpango huo utalenga kwenye maeneo makuu mawili ya uwekezaji ambayo kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ni mikataba ya kufungua soko la zao la muhogo na ujenzi wa kiwanda kikubwa Afrika cha saruji na cha kioo.
“Tumeingia mikataba tayari na kampuni mbili ambayo ni makubwa kwa uwekezaji nchini China ambayo yatatumia mabilioni kwa ajili ya uwekezaji wa aina mbili, ule wa kiwanda cha saruji, kioo na mkataba wa zao la muhogo,” alisema Mayeji.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa chini ya mikataba hiyo kuna viwanda mbalimbali vitajengwa ikiwamo kuongeza kina Bandari ya Tanga, ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza malighafi itakayotumika katika mabomba yatakayosafirisha mafuta kutoka
Tanga hadi Uganda.
Alisema kuwa kwa makubaliano ya mikataba hiyo ni kwamba ujenzi wa kituo cha viwanda, viwanda vya saruji na kioo vinatarajiwa kuanza wakati wowote mwezi ujao baada ya kukamilika kwa maandalizi ya mchakato huo.
Chanzo: Nipashe