China: Dawa mpya tuliyotengeneza ina uwezo wa kuzima janga la Corona 'bila kuhitaji chanjo'

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
China: Dawa mpya tuliyotengeza ina uwezo wa kuzima janga la corona 'bila kuhitaji chanjo'

Maabara moja nchini China ambayo imekuwa ikitengeza dawa ya kutibu maradhi ya Covid-19 yanayosababishwa na virusi vya corona imesema, inaamini dawa hiyo iliyotengeza ina uwezo wa kuzima janga la maradhi hayo liliyoikumba dunia nzima bila kuhitaji chanjo

Watafiti nchini China wanasema, dawa hiyo ya kidonge inayofanyiwa majaribio katika Chuo Kikuu cha Beijing ina uwezo sio tu wa kuwaponesha kwa muda mfupi zaidi watu wanaougua ugonjwa huo lakini pia inatoa kinga ya muda mfupi pia dhidi ya kirusi cha corona

Sunney Xie, mkurugenzi wa kituo cha Ubunifu cha Chuo Kikuu cha Beijing amesema, dawa hiyo imekuwa na mafanikio katika hatua ya majaribio kwa mnyama

Xie amesema, timu yake imekuwa ikifanya kazi kutwa kucha kutafuta kingamwili kwa ajili ya tiba ya ugonjwa wa Covid-19.
Ameongeza kuwa, anatumai dawa hiyo itakuwa tayari kwa matumizi baadaye mwaka huu na kuweza kupatikana kwa wakati endapo mripuko mpya wa virusi vya corona utazuka katika msimu wa baridi.

Mtaalamu huyo wa tiba nchini China amebainisha kuwa, matumaini yaliyopo ni kwamba dawa hiyo iliyotengezwa nchini humo itaweza kuwa tiba ya kitaalamu itakayositisha janga la dunia nzima la ugonjwa wa Covid-19.

Ripoti ya utengezaji dawa hiyo isiyo na hitajio la utumizi wa chanjo ya corona imetolewa, wakati kampuni ya bioteknolojia ya Moderna nchini Marekani imetangaza kuwa imefanyia majaribio kwa mafanikio chanjo iliyotengeneza kwa ajili ya kinga ya ugonjwa wa Covid-19.

Taarifa ya kampuni hiyo ya teknolojia ya tiba imeeleza kuwa, majaribio ya dawa hiyo aina ya mRNA-1273 waliyofanyiwa watu wanane waliojitolea yalikuwa na taathira sawa kwa kinga za mwili za watu hao wazima na za watu wengine walioambukiwa virusi vya corona.

Hivi sasa kuna miradi zaidi ya mia moja ya utengezaji chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 inayofanyika katika nchi mbali mbali duniani.../
 
Wana picha yao inaitwa Viral Factor! Ukiingalia utawaelewa vizuri sana yaani kuna limjamaa linajisifu kabisa litatajirika duniani baada ya kusambaza virus na Tiba anayo yeye pekee! Tuendeleee kujifukiza tuu,Aliyetuweza sisi waaAfrika ni yule wa Ukimwi tuu. Labda waje kutengeneza virus huku ila km wanatengeneza kwao....Mchuma janga hula na wakwao.
 
Back
Top Bottom