Hukumu ya Dowans imetoka wakati Muafaka ambao kampeni za mwisho zinafanyika igunga, Wapiga kura wa igunga tambueni kuwa ubovu na ufisadi wa CCM na Rostam Azizi ndio uliopelekea taifa hili lilazimike kulipa mabilioni haya, Tarehe 2 October iwe siku ya kuwapa Chadema ushindi ili kuowaongezea nguvu bungeni waweze kupambana na udhalimu huu na hatimae iwe ndio ishara ya kuwaondoa magamba 2015. Watanzania tunahitaji mabadiliko, tumenyonywa vya kutosha na tusipoamua sasa tutaangamiza taifa hili. Umaskini unazidi, maisha yanazidi kuwa magumu, hakuna anaejali hatma ya umaskini huu, wenzetu wametumia nguvu ya umma kuleta mabadiliko na kuondoa utawala dhalimu duniani, tanzania kwa nini tusifanye hivyo?
nawakilisha
nawakilisha