Chiligati, Nape chupuchupu kuangukiwa jukwaa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Eliasa Ally, Iringa

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM), Bw. John Chiligati na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye wameponea chupuchupu kuangukia na
jukwaa walilokuwa wanatumia kwenye mkutano wao katika Kata ya Mgama mjini Iringa jana.

Mbali na viongozi hao walioko kwenye ziara ya kutambulisha Sekretarieti mpya ya chama hicho, viongozi wengine wa chama hicho Wilaya ya Iringa Vijijini, akiwamo Mkuu wa Wilaya, Bw. Asseri Msangi walifunikwa na jukwaa hilo.

Wengine waliofunikwa na jukwaa hilo, Katibu CCM wilaya ya Iringa Vijijini Ahamed Mkiri, Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Bi.
Delfina Mtavilalo; Mwenyekiti wa UWT mkoa, Bi. Zainabu Mwamwindi; Mwenyekiti wa CCM Iringa Mjini, Bw. Abeid Kiponza na mbunge wa Mimbo la Kalenga, Dkt. William Mgimwa.

Jukwaa hilo lilianguka muda mfupi tu ya baada ya Nape na Chiligati kuteremka kwenda kugawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.

Tukio hilo lilitokea jana saa 6:00 mchana, muda mfupi baada ya viongozi hao kuwasili eneo hilo wakitokea Chuo cha CCM cha Ihemi na kuwahutubia wananchi, na kisha kuwapokea wanachama 80 wapya ambao walidai kuwa wamehama kutoka upinzani.

DC Msangi alisema kuwa tangu awali aliona jukwaa hilo linayumba na aliwaambia viongozi wa CCM kuwa jukwaa ni bovu kabla ya kuangua wakajibu kuwa haliwezi kuanguka.

Mkutano huo ulitawaliwa na vioja, kwani awali, Diwani wa Kata ya Mgama, Bw. Disima Lupalla (CCM) alimgomea Bw. Chiligati alipoitwa kutambulishwa kwa wananchi, akisema hatambui ujio wa Chiligati na na wenzake kwenye kata hiyo kwa kuwa hawakumpa taarifa, jambo ambalo alidai ni dharau kubwa.

"Mimi kama kiongozi niliyechaguliwa na wananchi hususani wanachama wa CCM mmekuja kwenye kata yangu bila kunitaarifu, hizo ni dharau mmenidhalilisha mimi, wewe (Chiligati) sikutambui, sikuelewi na ujio wako kwenye kata yangu mimi nauona ni batili," alisema Bw. Lupalla kwa msisitizo hali iliyoshangazwa viongozi hao na wananchi.

Bw. Chiligati alimwacha diwani huyo ili kuwarudisha wananchi ambao walikuwa wanaendelea kushangazwa na tukio la kuanguka kwa jukwaa.

Katibu wa CCM kata ya Ulanda Bw. Gervas Ngakonda na diwani wa Viti Maalumu Kata ya Kiponzero, Bi. Laura Kilyenyi walilaani vikali ujenzi mbovu wa jukwaa hilo kwa kuwa Dkt. Mgimwa alitoa sh. 500,000 kwa ajili ya shughuli hiyo na limejengwa vibaya hadi kuhatarisha maisha ya viongozi hao.
 
Mbona Chama cha Maulaji (CCMAULAJI) nDIO zao, Ukifuatilia Utagundua Hilo Jukwaa limetolewa na ten Percent!! Katika Mazingira ya kawaida Vitu Vingi vya Chama Cha Maulaji ni Dili Tu Hakuna Utaalamu Unaotumika!!
 
kumbe laana ya Makamba a.k.a Yuda Iskalioti bado inafanya kazi, waandalie makazi hawa mzee!!
 
Back
Top Bottom