Chile miners' rescue underway!!!!

AP_CHILE_RESCUE_CAPSULE.grid-3x2.jpg

bora nimepata ufafanuzi hapa kuhusu hii capsule. Na hii ni teknolojia ya jeshi la maji la chile
 
Bado wanasema couple of hours. Wanaweka mitambo sawa. Tutasinzia sasa
 
Sio muda mrefu sana Miner wa kwanza atatoka nje,Inachukua dk 15 - 20 kufika kwenye level ya ardhi,kutoka walipo mpaka juu ni feet 2300.Kutokana na makubaliano yao wataanza kutoka walio na nguvu,Miners wote wamelishwa Fluid food.Miner wote 33 wameangaliwa na Daktari ambaye alipelekwa huko chini,inasemekana imeamuliwa watoke usiku kwa sababu hali ya mwanga ingeweza kuwaharibu macho.Miner mkubwa ana Miaka 63 na kijana kuliko wote ana miaka 19.Hao watu wamekuwa ardhini kwa takriban siku 69.Inasemekana huko chini ni joto kali (90c) na kuna uwezekano mkubwa walio wengi wakawa na tatizo la kuchubuka ngozi.Mara tu wakifika Nje watakimbizwa Hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Chombo maalumu cha kuwachukua (Phoenix) kina uwezo wa kuchukua mtu mmoja at time,atakuwa anapata Oxygen na atavaa seti ya mawasiliano ili awe anawasiliana na waokoaji.Miner akishaingia ktk Phoenix tu kutapigwa king'ora kuashiria kwamba anakuja nje,itachukua dk 15 - 20 kufika juu.Bado kuna wasiwasi mkubwa kama uokoaji utawatoa Miners wote 33 salama.Kuna wasiwasi wa kuanguka kwa sehemu kubwa ya udongo na kuwafukia.Ukiacha Timu ya Uokoaji na mitambo watu wengine wako eneo la mbali na sehemu Miners watakapotokea.Zoezi zima la uokoaji litachukua 48 hrs.Watu wengi wa Mji wa Copiapo ikiwa pamoja na Rais wa Chile wapo katika eneo la Uokoaji.

Mwenyezi Mungu awabariki Miners wote 33 watoke salama!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom