Chidy Benz Zungumza kwa Nukta

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,453
20,712
Mimi ni shabaki wa kipindi chako cha The Chidy Benz Show kinachochorushwa na Eatv.Kwa mda sasa nimekuwa nikifatilia show yako,ila kuna wakati huwa naikosa kutokana na majukumu ya kikazi.Mda nilioitazama na kukuona ukizungumza,kuna jambo ambalo si vibaya tukikukosoa ili ujirekebishe.Linahusu uzungumzaji wako.Ukianza kuzungumzia jambo fulani unazungumza kama unabwabwaja bila nukta.Uzungumzaji wako wa hovyo hovyo unapelekea ushindwe kueleweka kirahisi.Unapoteza point ya msingi ya jambo unalozungumzia.Pia tabia yako ya kuvuta sigara mbele ya camera sio jambo zuri.Waungwana wanakuona mshamba.Unawafundisha nini vijana na watoto wanaotazama show yako?.Wale wanao unda zile sigara wanakulipa?.Umeingia nao mkataba wa kutangaza bidhaa yao katika show yako?.Kama sivyo basi uache kuvuta sigara mbele ya camera zinazo shoot show yako.Au ingia mkataba wa kibiashara na waundaji wa sigara ili utakapo anza kuugua maradhi yanayo sababishwa na uvutaji,uwe na pesa ya kutosha kujitibu.tembelea hapa upate elimu kidogo kuhusu madhara yatokanayo na uvutaji sigara:Madhara ya kuvuta sigara - Wikipedia, kamusi elezo huru.
 
Hayo ya Sigara tuyaweke kando,
Inawezekana hapo ndio kapunguza kabisa otherwise ungemuona na "kijiti cha Arusha".
Nizungumzie kuhusu kuweka nukta, jamaa ni Rapa, na kawaida ya Rapa ni kuongea kasi, so kawaida tu mkuu!!
 
kwanza show yenyewe sijui ina malengo gani.watanzania kwa kuiga tu wana alama nyingi
 
Jamani Chid benz show ni maisha halisi ya huyo jamaa,so anayoyafanya ndo maisha yake,k2 kingine sababu kafanya chid wa2 wanadis kipind hakina maana angefanya m2 wa mbele 2ngeona safi 2pende vya kwe2 that's all!
 
Back
Top Bottom