Chidi Benz atoroka sober house, yadaiwa alikaa siku 28 tu

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Wakati wadau wa muziki wakifahamu kuwa msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chidi Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani,inadaiwa Chidi Benz alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa.

Akizungumza na Global Publishers meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura, amethibitisha kuondoka kwa Chidi akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu.“Ni siku 28 tu alikaa, lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Tumaini.

Aliomgeza, “Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maana siku moja meneja wake (Babu Tale) alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondokaa ling’ang’ania kuondoka naye. Sisi pamoja na Tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa,”Pia Global walimtafuta Chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.

Babu Tale alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema: “Sitaki kusikiliza wala kuzungumza lokote kuhusu Chidi, muda ukifika nitaongea ila kwa sasa niacheni tu.”

1464253898860.jpg
 
Maboss wameshamfanya sample lazima aendelee Na hali yake.Hiyo ni fedha ya mtu.Namaanisha "Ndondocha la unga".Namkumbuka marehemu Mr.Ebo"ukisema tusiuze unga ugali utasongwa na nini".
"unaharibu interview"
 
Ile ndio starehe ya mwisho unaambiwa ukijaribu tu uwezi kuacha Na ukiacha hayo madawa ya hospital lazima uteseke utafute unga tena labda uwe Na uwezo Wa ela Na usiwe Na matatizo yoyote ndio unaweza kuvumilia kwa muda unga ni hatari sana kwa jamii yetu
 
Mmeambiwa pia epukeni kuwasimanga au kuwatolea negativity watu waliotoka rehab,kufanya hivyo kunaweza kuchangia kuwarudisha kwenye matumizi ya madawa!Tuwasupport,ni binadamu wenzetu hata kama tuna chuki binafsi,sio wakati wake!
 
Back
Top Bottom