GE2025 Chid Benz: Inabidi watu watiki, wanaopiga mishale haihusiki na chama

GE2025 Chid Benz: Inabidi watu watiki, wanaopiga mishale haihusiki na chama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Rashid Makwiro almaarufu kama Chid Benz Msanii wa Bongo fleva ameonekana akiwa pamoja na Msanii Shetta ambaye pia ni Mgombea Ubunge CCM Kata ya Mchikichi wakiwa katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika leo Oktoba 22, 2025 jijini Dar es Salaam

Hapo awali Chid Benz aliwai kufanya mahojiano na shirika la habari la BBC ambapo alieleza kuwa anaogopa kujihusisha na vyama vya siasa kama ilivyokawaida kwa wasanii wengine

Soma pia GE2025 - Chid Benz: Naogopa kuchanganya siasa na sanaa yangu, nimetafutwa na Vyama vitatu kwenda kufanya Tamasha

Je ni nini kimempata Chid Benz kwa sasa? yule ambaye baadhi yetu tulimtazama kama msanii anayejitambua na kuwa na msimamo licha ya wenzake wengi kuingia kundini kwa Mama

 
Sasa kama chama kimefikia hatua ya kuwategemea mateja walio watengeza wao wenyewe, kuwaokoa! Hii ni dalili ya wazi kabisa ya jahazi kwenda kuzama hiyo tateje 29.
 
Kapona huyu au bado yupo kwenye dozi! 😁
Ameacha kulala mitaroni?
 
Je ni nini kimempata Chid Benz kwa sasa? yule ambaye baadhi yetu tulimtazama kama msanii anayejitambua na kuwa na msimamo licha ya wenzake wengi kuingia kundini kwa Mama
Msimamo sio kuwa neutral, msimamo ni kuchagua upande, sasa ameonyesha msimamo.

Ukisikia mtu anasema sitaki kujihusisha na siasa anamaanisha siasa za upinzani.

Ukisikia kiongozi anasema viongozi wa dini wasichanganye siasa na dini, hiyo siasa inayoongelewa hapo ni siasa za upinzani(kukosoa)
 
Back
Top Bottom