Chicken jalfrezi na wali wa kukaanga

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,568
16,907
Mahitaji


Kwa ajili ya chicken jalfrezi

Kuku 1 mkate vipande vipande

Curry powder 1 teaspoon

Uzile wa unga (bizari ya pilau) 1 teaspoon

Bizari ya manjano 1/2

Plain yogurt (sio lazma)

Chicken masala upendayo ukikosa tumia tandoor 1/2 teaspoon

Limau 1

Vitunguu maji 4

Nyanya 4 zisage

Nyama ya kopo 2 tablespoon

Kitunguu saumu 1 teaspoon

Hiliki punje 4

Tangawizi 1 teaspoon

Pilipili manga 1 teaspoon

Chumvi kiasi

Viazi (potatoes) 5

Pilipili mboga 1- ukipata ya red fanya nusu red na nusu green


Namna ya kutaarisha chicken jalfrezi

Mueke kuku bizari,chumvi,limao na pilipili manga....mwache akolee walau 30 minutes

Weka sufuria jikoni

Mimina mafuta kidogo

Weka viungo masala,bizari ya pilau,curry powder na hiliki

Kaanga kwa dakika 1

Weka vitunguu maji kaanga kwa dakika 5

Weka saumu na tangawizi

Kaanga vianze kua laini kidogo

Weka kuku,koroga vizuri

Funika kwa ufuniko acha ichemke kwa maji ya kuku mwenyewe

Weka viazi acha viwive kidogo tu

Mimina nyanya,yogurt na pipili mboga

Subir viwive then upua

Weka mezani tayaar kwa kuliwa
 
****WALI WA KUKAANGA***

Karot 2 zipare

1/2 teaspoon ya saumu

Wali uliokwisha pikwa kg 1

Mayai 2-3 yafunje na uyachanganye

Zabibu kavu kiasi upendacho (sio lazima)

Namna ya kutaasrisha

Weka mafuta kidogo sana kwenye sufuria

Yakishapata moto weka saumu kaanga kwa dakika 1

Weka yai na kaanga huku wakoroga ili liwe vipande vipande....

Toa mayai weka kwenye bakuli...

Weka tena kwenye sufuria mafuta kidogo

Kaanga karot zikaribia kuwiva weka zabibu kaanga vizuri

Weka mayai na wali uloikwisha pikwa

Changanya kwa muda wa dakika 5

Epua na weka mezani

Tayaar kwa kuliwa
 
****karibuni***
 

Attachments

  • 20140616_213237.jpg
    20140616_213237.jpg
    257.5 KB · Views: 306
  • 20140616_213347.jpg
    20140616_213347.jpg
    276.5 KB · Views: 305
  • 20140616_223136.jpg
    20140616_223136.jpg
    257 KB · Views: 308
Njia nzuri sana hii ya kupasha kiporo cha wali.
farkhina, asante umenifundisha kuongeza matumizi ya mtindi ili nipunguze kutumia nazi. Mtindi naweka kwenye sosi ya biriani tu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom