Rosti la viazi mbatata na nyama

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,706
MAHITAJI

1.Viazi mbatata kilo moja

2.Nyama ya ng'ombe kilo moja

3.Nyanya maji kubwa nane

4.Tomato paste vijiko viwili vya chakula

5.Vitunguu maji viwili

6.Karoti kubwa moja

7.Kitunguu saum kilichosagwa kijiko kimoja cha chakula

8.Binzari nyembamba ya unga nusu kijiko cha chai

9.Tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja cha chakula

10.Pilipilimanga ya unga nusu kijiko cha chai

11.Paprika kijiko kimoja cha chai

12.Pilipili mbichi iliyosagwa kiasi

13.Mchuzi mix au garam masala kijiko kimoja cha chakula

14.Limao moja

15.Mafuta ya kupikia

16.Chumvi

MAPISHI

1.Katakata nyama katika vipande tia tangawizi na chumvi kamulia kipande cha limao changanya, ichemshe hadi iive bakisha supu kiasi

2.Saga nyanya kupata rojo

3.Kataka vitunguu maji na karoti katika vipande vipande

4.Tia mafuta katika sufuria, acha yapate moto tia vitunguu maji koroga hadi vibadirike rangi viwe kama vya kijani mpauko, kisha tia vitunguu saum koroga kidogo hadi usikie harufu, visiungue, tia binzari ya nyembamba koroga vyema.

5.Tia rojo la nyanya na chumvi kiasi kisha koroga na funika, acha hadi nyanya ziive vizuri

6.Tia humo nyama,viazi na vipande vya karoti na tomato paste koroga vyema

7.Funika acha vichemke kiasi, funua nyunyuzia mchuzi mix au garam masala, unga wa pilipilimanga, paprika,pilipili mbichi,kamulia kipande cha limao kilichobaki,tia supu iliyobaki kidogo kisha koroga, punguza moto acha chakula kichemke taratibu hadi maji yapungue na ibakie rosti zito.

8.Epua chakula kipo tayari

Andaa juisi au soda baridii na chakula hiki kisha jenga mwili

FB_IMG_1668232411706.jpg
 
Ha ha haa,inashangaza kama usemavyo nama ina mafuta tayari Mkuu...
Eee mafuta ya kwenye nyama yanatosha kabisa ,kujaza mafuta mengi sio nzuri kwa afya ,sio ubahili,nyama inapoiva unaiacha na supu kidogo ambayo ndio utachanganya,Sasa futa la nini tena
 
Itabidi niwe nakula kwa mamalishe,chakula kile kingine tu Cha usiku ndio nitakula ,sita kwa sita,hakuna Cha mafuta
Hicho mbona utakimbia mwenyewe,nikikuzoea siyo kwa mkesha huo.Kaz itakushinda,kibaruani utatimuliwa kwa kosa la kusinzia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom