Chibok: Miaka Miwili Baadaye

My God...
 
Sio unafki. Kiufupi ni kwamba ukiona vita yoyote taifa la kimagharibi limejikita jua kuna maslahi.
Mdogo wangu huniambia kila siku no free lunch. Ndio haya sasa. Adui si wa kwako hayupo nchini mwako ila unatumia mateknolojia ya hali ya juu na gharama kubwa kumuangamiza. Dini imekuwa mwanvuli tu. Ila ndani yake ni ushetani mtupu.
 
"DINI IMEKUA MWAMVULI TU,AMBAO NDANI YAKE NI USHETANI MTUPU"
 
Hii ni sinema tu na ukweli wa ili tukio upo Washington DC
 
Nchi yoyote yenye malighafi ambayo ni hitaji kuu kwa mataifa ya magharibi au mabeberu....hiyo nchi haitakaa ibaki salama hata siku moja......sote tunafahamu kuwa Nigeria ni miongoni mwa nchi zinazodhalisha mafuta kwa wingi duniani.....kuiacha Nigeria itulie kwao kunamaanisha kuwa ni kuiacha Nigeria ijipatie maendeleo na hivyo kujitegemea....jambo ambalo ni sumu kwa mataifa ya magharibi....hivyo kikundi cha kigaidi cha boko haram ni kimewekwa mahususi kuihadaa dunia na kuipa serikali ya Nigeria kazi ya kufanya huku ikiacha kushughulika na masuala ya msingi kama taifa....kwa mfano kwa sasa hivi serikali inalazimika kupunguza bajeti kwenye huduma za kijamii kwa ajili ya kutunisha msuli wa bajeti ya ulinzi kwa ajili ya usalama......wakati huo huo serikali inalazimika kuomba mpaka misaada ya kijeshi kutoka kwa mataifa anayodhani kuwa ni rafiki kumbe ni unafiki.......

Ni mpuuzi pekee anayeweza kuamini kuwa serikali na washirika wake wanashindwa kufanya operesheni ya hata week moja ya kuwakomboa hao wasichana kwa muda wote huo.....kipi kinachoshindikana kufanyika kwa jambo hilo.....ukitazama kwa makini huwezi kupata sababu ya msingi ya serikali na washirika wake wanaojiita kuwa ni watetezi wakuu wa haki za binadamu.......

Ikiwa serikali ya Nigeria ndio inadhibiti mipaka yote ya nchii hiyo....hao wapiganaji wa BOKO HARAM wanapata wapi silaha kali kiasi cha kuiogopesha serikali ya Nigeria....au tuseme wapiganaji wa boko haram ni mazimwi wasioonekana kwa macho....??

Kusema imekuwa ni changamoto kubwa kupata taarifa sahihi katika dunia hii iliyojaa propaganda na unafiki wa hali ya juu....lakini jambo la kujivunia ni kuwa muumba ametupa ubongo na ufahamu wa kuweza kuchambua na kutafakari kila habari inayotufikia.....

DUNIA ITAKUWA MAHALI SALAMA KWA KUISHI KAMA KILA TAIFA LITAISHI KATIKA UHALISIA NA KUACHA UNAFIKI......
 
Aksante..
 

Visa vya uharamia pwani ya Somalia vimepungua
Maharamia saba kutoka Somalia wamefungwa jela na mahakama nchini Ufaransa baada ya kupatikana na makosa ya kuteka boti na kuua mmiliki wake mwaka 2011.

Maharamia hao wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka sita na 15 jela.

Waliteka boti la Christian na Evelyne Colombo kwenye Ghuba ya Aden.

Wawili hao walikuwa kwenye safari ya kutalii dunia.

Christian aliuawa na mwili wake kutupwa baharini, naye mkewe akashikiliwa mateka kwa saa 48 kabla ya kuokolewa na wanajeshi wa Uhispania.

Maharamia wawili waliotambuliwa kama Farhan Abdisalamn Hassan na Ahmed Abdullahi Akid, na ambao walidaiwa kuhusika katika kuwatafuta na kuwapa kazi maharamia, walifungwa jela miaka 15.

Farhan Mohamoud Abchir, aliyekuwa hajatimiza umwi wa miaka 18 wakati huo na ambaye alianza kuugua ugonjwa wa kuchanganyikiwa kiakili akiwa gerezani kwa mujibu wa wakili wake, amepewa kifungo cha miaka sita jela.

Mwendesha mashtaka alikuwa amependekeza wafungwe miaka 22.



Wanajeshi wa EU walitumwa kukabiliana na maharamia
Christian na Evelyne walkuwa wameuza mali yao yote kabla ya kuanza safari hiyo.

Waliondoka bandari ya Aden nchini Yemen mapema Septemba 2011 wakielekea Oman boti yao ilipovamiwa na maharamia hao.

Visa vya uharamia vilipungua sana pwani ya Somalia hasa baada ya majeshi ya Ulaya kuingilia kati.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hakuna meli yoyote kubwa iliyotekwa ikilinganishwa na meli 47 zilizotekwa mwaka 2010, visa vilipokuwa juu zaidi.

Chanzo: BBC Swahili
 
Kumbuka wakati wa Jonathan alijikuta hata makamanda wake tena wa ngazi za hui kabisa ni waaminifu kwa BOKO HARAM.

Siku dunia ikiacha kuhubiri unafki na kuhubiri ukweli hasa misikitini mambo hayo yatapata tiba lakini si kwa hali ya sasa

I remember reading a leaked report about Nigerian Army commanders who were allegedly briefing Boko Haram militia about the plans and tactics, as a result Boko haram is always ahead of army.
Its shame for people who show allegiance to killers simply because they are fellow Muslims.
 
Kwa mzazi mkuu haihitaji awe mwanao inaumiza sana tena sana
 
Mbona boko haramu walisema wasichana wote wameolewa na wapiganaji wao, kwa hiyo wale mabinti wamenogewa na michi kwa hiyo hawana mpango wa kurejea makwao
Wameolewa kwa idhini ya nani? Wale bado wadogo anayetoa idhini ya kuoa ni bokoharam au wazazi?
 
Nogeria haina wanajeshi?waende kama vile vitani kuwakomboa!
Ni vigumu sana kupambana na magaidi kuliko kupigana jeshi kwa jeshi, hawa huvaa kiraia na wengine wapo uraiani au hata jeshini, mnapopanga kuvamia eneo flani walioko jeshini huwasiliana na wenzio. Hii ni vita ngumu sana
 
Ni vigumu sana kupambana na magaidi kuliko kupigana jeshi kwa jeshi, hawa huvaa kiraia na wengine wapo uraiani au hata jeshini, mnapopanga kuvamia eneo flani walioko jeshini huwasiliana na wenzio. Hii ni vita ngumu sana
jwtz baba lao! but hatutaki kuingilia yasije kutukuta ya kenya na alsgbab bure..Tumezoea amani.Watajua la kufanya
 
Hii inauma sana, kumbuka jeshi likiwavamia hawa boko kwa lengo la kuwaokoa ni hatari sana kwa usalama wa mateka
 
Ni vigumu sana kupambana na magaidi kuliko kupigana jeshi kwa jeshi, hawa huvaa kiraia na wengine wapo uraiani au hata jeshini, mnapopanga kuvamia eneo flani walioko jeshini huwasiliana na wenzio. Hii ni vita ngumu sana
Jeshi ni taasisi iliyokamilika sana kimfumo. Ukikuta jeshi lina mamluki hilo ni jeshi dhaifu na bovu kabisa. Tukubali tu kuwa jeshi la Nigeria ni dhaifu.
 
Tena usitaje jambo hilo kabsaa, usa wenyewe wemegwaya wenye tech ya juu sana jwtz ingefanya nini?
mmhhh! natania tu...Ila hawa watu hawa wajinga sana!
Et elimu ya magharib ni haram wakat magari,mabumo,bunduki,simu vyote vimetokana na hiyo elimu ya magharibi.wanataka nn haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…