Dark Angel
JF-Expert Member
- Sep 12, 2013
- 212
- 220
Refresh zipo mkuu...Hizo caption zipo wapi?
Lakini inawezekanaje katika dunia ya sasa kwamba hakuna msichana hata mmoja alieweza kuokolewa?
Miaka miwili iyopita wiki kama hii , wasichana 267 walitekwa nyara kutoka shuleni kwao na wanamgambo wa Boko Haram .
Suala lililolaaniwa vikali kimataifa na kuchochea kampeni ya mitandao ya kijamii iliyojulikana kama #bringbackourgirls na kuweka wazi udhalimu unaotekelezwa na makundi ya uasi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Shule ya Chibok ilivyobakia sasa
Zaidi ya vijana 200 wa kike hawajapatikana hadi leo .
Katika ripoti hii maalum mwandishi wa BBC Martin Patience alisafiri hadi Chibok kuongea na familia za wasichana na kutembelea shule ambako walitekwa nyara.
Msitu hapa ni mkubwa .. na ni rahisi sana kwa wanamgambo wa Boko Haram kuvamia msafara wowote wa magari ya kijeshi
Barabara ya kuelekea Chibok imejaa vikwazo na hatari hata hivyo tulisafiri katika msafara wa magari ya kijeshi tukipitia vijiji vilivyotelekezwa .. kimoja baada ya kingine
Taswira
Kile kinachoonekana kama msikiti unaonekana kupigwa risasi kila mahali , Paa lake limeng'olewa ,
Hiki kilikuwa ni kijiji ambacho huenda kilikua ni makaazi ya makumi kadhaa familia , lakini kwa sasa hakuna mtu anayeishi hapa na vichaka vimemea tena kijijini hapa
Msitu hapa ni mkubwa .. na ni rahisi sana kwa wanamgambo wa Boko Haram kuvamia msafara wowote wa magari ya kijeshi
Msikiti wa Chibok
Saa tatu baadae tuliwasili Chibok mahala kulikokuwa zamani soko maarufu la mji ambao kwa sasa halisikiki.
CHIBOK
Lakini wakati huo Boko Haram walipokuja kuwateka mamia ya wasichana wa eneo hili walibaki na kumbukumbu za kutisha za usiku huo …..
Wazazi hapa wamebakia kusubiri majibu ya wapi waliko watoto wao.
Miongoni mwao ni Mariam Abubakar.
Mwanaye Han Satu alikua na umri wa miaka 17 alipotekwa … alipenda mitindo
Msafara wa jeshi la Nigeria
''Msichana wangu likua mchapakazi . Alipenda utani na alipenda mavazi.''
''Muda mfupi tu kabla ya kuchukuliwa alikua ameniomba nimnunulie mashine ya kushona nguo''alisema Myrama Abubakar.
Mbele ya nyumba yake ya matope Maryama alivuta nguo alizoacha binti yake .
Alichukua vazi alilolipenda na kuliweka kwenye magoti yake .
Chibok
''Hii ni gauni aliyotakiwa kuvaa kwenye harusi ya rafiki yake siku moja baada ya kumaliza mitihani .
Lakini mitihani haikufanyika . Nitaitunza gauni hii mpaka atakaporudi alisema mzazi huyo.
Na baade nilizungumza na Binta AbuBakar mama yake Maryam ambaye sasa angekua na miaka 19 -
Kundi la waandishi wa habari
''Kabla ya kwenda shuleni siku ile alikua anafanya kazi katika duka angu la chakula . Aliweza kufanya mauzo ya dola hamsini! alikua mzuri sana kuwavutia wateja , alikua mfanyabiashara hodari . Hizii ndizo nyakati za mwisho nilizokua naye.
Naomba binti yangu arejee akiwa hai . Lakini kama haitakua hivyo natumai roho yake italala kwa amani . Natumai kumbu kumbu za kutisha alizoziona wakati alipotekwa yatakua ndio mateso yake ya mwisho ,alisema bi AbuBakar.
Mwanaye Han Satu alikua na umri wa miaka 17 alipotekwa … alipenda mitindo
Miaka miwili baadaye hakuna taarifa kuhusu waliko wasichana wa Chibok - Labda wako Chad ama Cameroon - kuna uwezekano mkubwa wengi wao walilazimishwa kuolewa na wapiganaji.
Maisha yanaendelea kurejea taratibu katika hali ya kawaida mjini Chibok na usalama unaimarika.
Lakini inawezekanaje katika dunia ya sasa kwamba hakuna msichana hata mmoja alieweza kuokolewa?
Kuna vitu vinatokea Duniani ambavyo vinashangaza.
Huwa najiuliza huo msitu ambao Boko Haram wanaweza kuingia lakini jeshi la nchi lenye resources zote linashindwa kuingia, ni aibu.
Ni rahisi kusoma hii Habari ya hawa mabinti na kuona ni kawaida kwa sababu si ndugu wala jamaa zetu, ila wenye watoto wao wanapitia kipindi kigumu sana.
Pamoja mkuuSawa, tupo pamoja.
Ndio maoni yao tenav,mkuuWatu weupe nao michosho tu , Pori la Chibok eti Msitu.
Siamini kuwa Hawa jamaa wameshindwa kupatikana. Unless kuna jambo lingine tusilolijua wana ulimwengu.Nogeria haina wanajeshi?waende kama vile vitani kuwakomboa!
Haya mambo yanaumiza kichwa,yupi mpigania imani yupi n muasi na gaidi wote wanachanganya snTatizo higaidimbo limejikita kwenye imani za watu. Kwamba kinachopiganiwa ni imani na si uasi hivo kumjua adui ni kazi ukizingatia eneo hilo majority ni wa imani hiyo
Wakati mwingine huiona Marekan km chanzo cha matatizo mengi sana barani africaWakuu:
Mimi nailaumu Marekani. Ni juzi tu wametoa taarifa ya kutamba eti wanapeleka wataalam wa kijeshi 800 pamoja na vifaa vya kisasa vyenye kutumia utaalam wa hali ya juu (drones)nchini Uganda ili kumsaka Josef Kony.
Sasa Kony ni mtu mmoja wanatumia gharama kubwa kwa nini wasitumie gharama hizo kuwatafuta hao wasichana wetu 200? ambao hadi sasa hawajulikani walipo. HUO NI UNAFIKI.
Jwtz...Hawa boko haram wenyewe ndo maharam....
ukiangalia walio tekwa na kuumizwa ni wa dini yao sasa kama sio uharamu huo ni nini? Ni Mungu yupi wanampigania kama sio ushetani tu..... wawachukue JWTZ wakasafishe huo msitu....