Chezea muosha magari wewe

Chezea muosha magari wewe

Pole ila baadhi ya yenu nyinyi mabinti mmekaa kudanganyika tu
 
Kila mmoja na mbinu zake za mafanikio. Na ili akupate ilimbidi aendane na moyo wako unavyoerekea. Vumilia tu huku ukimtafuta na Mungu wako
 
Yaani kuna mdada kanitumia meseji juzi anataka ushauri nimebaki nimeduwaa sina la kusema kabisa. Ninachoweza kusema ni kuwa sasa nina uhakika wa ule msemo wa wahenga kuwa Kupenda Upofu. Hebu na nyinyi hebu someni wenyewe mi nakaa pembeni.

Anko habari yako,
Vipi mzima? Anko huu ni mwezi wa nne toka nimeolewa, yaani tayari najilaumu sana kuhusu ndoa hii. Kiukweli najuta sana. Kabla ya kunioa mume wangu alikuwa anakuja kwangu kila siku na gari jingine, akanambia kazi yake ni dalali wa magari, na akaniahidi kuwa na mimi ataninunulia gari ili nisiwe na tatizo la usafiri. Niliongeza mapenzi kwake ili asijekusahau kunipa gari. Uchumba wetu ulichukua miezi mitatu kisha tukaoana katika ndoa ambayo mpenzi wangu alisema tufanye kakitu kadogo tu kakisiri tusiharibu pesa. Ndugu zangu walininunia lakini mimi sikujali. Kwa kuwa nilikuwa na chumba kizuri katikati ya mji, ilionekana maisha tuanze kwetu maana mume wangu akisema alikuwa akiishi na mama yake nje ya mji, aliyekuwa akimkataza asipange chumba.

Huwezi kuamini Anko, si juzijuzi tu ndio nimegundua kumbe nilikuwa nadanganywa siku zote, kumbe mume wangu kazi yake ni kuosha magari, hana udalali wala nini. Kuna kijiwe chao kando yam to wanaosha magari mchana kutwa sasa akiachiwa aoshe gari basi ndio huzunguka nalo na ndipo alipoweza kunidanganya nikaingia kingi. Kwanini alinidanganya vile? Si angenieleza tu ukweli nijue?

Ntaendeleaje kumuamini sasa? Mbaya zaidi mi nimemaliza chuo kikuu na nimegundua kuwa jamaa hakumaliza hata fom tu, Anko what do I do? Wenzangu walikuwa wananicheka nilikuwa siwaelewi. Nilikuwa kila siku napiga picha niko kwenye gari tofauti nazituma instagram, jamani watu wakigundua si ndio watanichamba mwaka mzima? Ndugu zangu walinionya kuwa wanamuona jamaa tapeli nikagombana nao sana, narudije kwetu? Anko nipe ushauri.

Hata mimi sijui nimwambieje huyu mdada, hivi alikuwa fala kiasi gani hakuona kuwa anatapeliwa?
Ulipoona magari akili yako ikatafakari kuhusu pesa ukafunga kabisa uwezo wako wa kufikiri wa ki graduate sasa leo umeujua ukweli ndo unakuja kutuomba ushauri. Angekuambia ukweli ungemkataa...Ukomeeeee unalo hilo babuuu.. Na bahati hajakudungaa na mimba....
 
Unanikumbusha mwalimu Jackson alimdanganya Martha ni mfamsia kumbe ni mwalimu Wa dhule ya msingi kagogwa Hahahahahaha akala mzigo
 
Awe mpole tu..... Hivi 20% yule aliyewahi kuimba wimbo wa TAMAA MBAYA yuko wapi siku hizi??
 
Siku zote wanawake hawasikii ukweli, usijiroge Kuwa mkweli kwa mwanamke, hawezi kukuelewa hata siku moja..... Masikio ya mwanamke husikia uongo,, na ukiwa muongo mwanamke hijisikia raaaaha kama vile unamwimbia kwa zeze.... Jamaa amewasoma tabia zao, na atakua anawaburuza saaana. UONGO +KUJIAMINI.. Mke hachomoi.
 
Ngoja na mie nkaoshe magari au nikawe fundi magari maana ntakuwa na drive mikoko eday.
Ntawamegaje wa kila rika na kila aina wa vyuo na waofisini. Aishi milele aliyetengeneza magari!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom