Cheyo: Magufuli ni Rais aliyesubiriwa tangu Tanzania ipate Uhuru

Yupo kwenye waiting list ya kupata ajira serikalini, tukiwaambia ajira ngumu hamsikii ona sasa,
 
haya ni matusi sasa...so Nyerere,Mwinyi,Mkapa and JK did nothing?
Kasema kweli. Ujue nini?
Utawala wa Nyerere na Waziri mkuu wake Sokoine walifanya operesheni wahujumu uchumi kidhati kabisa.
Na iIiungwa mkono sana na watu wa chini kama ilivyosasa. Ila kwa hila na wanavyoweza kucheza na "mazingira", Sokoine hakuishi, wala hakushuhudia mwisho wa kesi hizo. Nyerere akabaki peke yake. Wakapekua na kucheza na makaratasi ambayo nyie mnasema ni sheria, tena kwakushirikiana na haohao wakubwa serikalini ambao walikuwa "against"na "Ikulu" ikaja kuonekana baadae kuwa operesheni ama matamko ya serikali bila baraka za bunge kutengeneza sheria, si chochote si lolote.
Wakaanza kuiburuza serikali mahakamani, wengi kuigaragaza na kudai fidia. Sheria ya uhujumu uchumi haikung'ata, maana haikutungwa kabla,bali ilitungwa baada ya operesheni kufanyika.
Sasa kuanzia hapo watawala wote waliofuata walilaani ufisadi lkn hakuna hatua yoyote mahususi iliyochukuliwa kukomesha. Labda kwa kuhofia dhahama iliyopelekea serikali kushindwa ktk awamu ya kwanza. Mfano Mwinyi alianzisha kaulimbiu ya "Fagio la chuma", Mkapa "Uwazi na ukweli".Awamu iliyopita sikumbuki kauli mbiu yake. Lkn kama nilivyokwisha kusema hapakuwa na dhamira ya kweli ya kudili na uozo huo.
Hivi sasa serikali tunaiangalia machoni na kuona kuwa ina dhamira ya kweli, sababu wameanza na kutunga sheria kwanza, na kuandaa "timu" mahususi ya kuhangaikia hao mafisadi.
Kama rais alivyokuwa anawaasa Mapolisi wakamataji,waandika mashitaka, waendesha mashitaka,mawakili na mahakimu kama wakiendeleza longolongo zao kuchezea sheria kwa manufaa yao binafsi, basi tunashauri serikali ikodi hiyo kada ya sheria mahsusi kuja kudili na nahakama hiyo tu,kama uadilifu wa wazalendo utakuwa ni sifuri kwa dhamira hii adhimu ya Serikali.
 
Kachelewa sana kusema hayo kwani alitegemewa kufanya hivyo kitambo kirefu sana...huyo ndiye Cheyo, so true to form!
 
Mkuu, tatizo letu kubwa si wanaokosoa au kupinga. Hatuwezi kuishi katika dunia bila kuwa na wakosoaji au watu wanaopinga, hata kama utaona unayoyafanya ni mazuri kwa asilimia 100%. Umesoma habari za mwanasayansi wa kale anayeitwa Gallileo Gallilei? unajua kwamba alikuwa "mpinzani" wa kwanza juu ya imani kwamba jua ndilo linalozunguka dunia? unajua kwamba baada ya kuchapisha imani yake hiyo, alihukumiwa kifo?? Je unajua kwamba mawazo yake hayo ya "upinzani" ndicho kilichothibitishwa kuwa kweli miaka mingi baadaye? Tuwe makini tunaposikia haya mambo. Hicho unachokiita "Upinzani" (Mawazo mbadala au ukosoaji) ndiyo chanzo kikubwa cha maendeleo ya dunia hii. Ogopa sana watu wanaoogopa au kuchukia kukosolewa au kupingwa.....
Kwa ukweli huu ni mjinga pekeee atakae yapuuza

Lakini tuangalie histolia ya falao pia alipinga agizo la Mungu

Magufuli anapaswa kusahihisha kauli yake, lakini aweke japo hata masharti nafuu ili wapinzani wake waweze kutoa michango yao katika majukwaa na watanzania waelewe kipi kinaendelea

Mafanikio yake ni kutenda vema aruhusu hii mikutano ila isiathiri utendaje wake kama anafanya vema watanzania watachuja wao wenyewe.

Ikitokea atarekebisha hapa naamini atakuwa amekata kiu na achukulie hili kama udhaifu wake na tutamuelewa tu kama binadam wengine
 
Kasema kweli. Ujue nini?
Utawala wa Nyerere na Waziri mkuu wake Sokoine walifanya operesheni wahujumu uchumi kidhati kabisa.
Na iIiungwa mkono sana na watu wa chini kama ilivyosasa. Ila kwa hila na wanavyoweza kucheza na "mazingira", Sokoine hakuishi, wala hakushuhudia mwisho wa kesi hizo. Nyerere akabaki peke yake. Wakapekua na kucheza na makaratasi ambayo nyie mnasema ni sheria, tena kwakushirikiana na haohao wakubwa serikalini ambao walikuwa "against"na "Ikulu" ikaja kuonekana baadae kuwa operesheni ama matamko ya serikali bila baraka za bunge kutengeneza sheria, si chochote si lolote.
Wakaanza kuiburuza serikali mahakamani, wengi kuigaragaza na kudai fidia. Sheria ya uhujumu uchumi haikung'ata, maana haikutungwa kabla,bali ilitungwa baada ya operesheni kufanyika.
Sasa kuanzia hapo watawala wote waliofuata walilaani ufisadi lkn hakuna hatua yoyote mahususi iliyochukuliwa kukomesha. Labda kwa kuhofia dhahama iliyopelekea serikali kushindwa ktk awamu ya kwanza. Mfano Mwinyi alianzisha kaulimbiu ya "Fagio la chuma", Mkapa "Uwazi na ukweli".Awamu iliyopita sikumbuki kauli mbiu yake. Lkn kama nilivyokwisha kusema hapakuwa na dhamira ya kweli ya kudili na uozo huo.
Hivi sasa serikali tunaiangalia machoni na kuona kuwa ina dhamira ya kweli, sababu wameanza na kutunga sheria kwanza, na kuandaa "timu" mahususi ya kuhangaikia hao mafisadi.
Kama rais alivyokuwa anawaasa Mapolisi wakamataji,waandika mashitaka, waendesha mashitaka,mawakili na mahakimu kama wakiendeleza longolongo zao kuchezea sheria kwa manufaa yao binafsi, basi tunashauri serikali ikodi hiyo kada ya sheria mahsusi kuja kudili na nahakama hiyo tu,kama uadilifu wa wazalendo utakuwa ni sifuri kwa dhamira hii adhimu ya Serikali.
hata hao waliitangulia kuna mema mengi wameyafanya....tuyatambue,japo lazima wana mapungufu yao
 
Waliyoyafanya kweli ni mengi,ila mada yetu pendwa ni mapambano dhidi ya rushwa.
Nimeelezea jinsi awamu ya kwanza ilivyochukua hatua za dhati kupambana na iliposhindwa, tawala tatu zilizofuata, fisadi alionekana mtu mwenye akili,aliheshimika,kuogopeka na hakuna hatua ama mkakati madhubuti uliochukuliwa kukomesha mafisadi.
Kwakuwa tunabadilishana mawazo, ukiacha mambo mengine, naomba unikumbushe awamu ya Mwinyi,Mkapa na Kikwete, uoneshe mchakato mahususi uliofanywa kitaifa kukomesha mafisadi .
 
Back
Top Bottom