Cheti cha corona ni pesa tu kila kona

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,562
11,625
Inasikitisha sana katika kipindi hiki kigumu cha uchumi duniani kila mmoja amepanga kumminya mwenzake bila uhakika wala faida ya kinachofanyika.

Mwanzoni niliona tangazo la wizara ya afya lililohimiza wasafiri kuhakikisha kuwa wanapata cheti cha usafi wa corona kabla kuondoka nchini na ikatolewa hesabu ya kila kundi la wasafiri kulipa kulingana na utaifa wao.

Na mimi juzi nilipotaka kuanza safari kwa utii nikaingia kwenye hamkani japo uchumi umenipiga chenga.Nikafika hospitali ya Amana na kwa haraka kabisa nikafikishwa kwenye kitengo cha kuchukua sampuli kukiwa na mtu inaonekana amewekwa maalum kuharakisha shughuli bila kupitia urasimu wa foleni moja kwa moja kutoka ofisi ya mganga mkuu.

Gharama ya kuchuliwa sampuli ni tsh.25000.Ilipofika usiku nikatumiwa ujumbe na namba ya kulipia dola 50 kwa thamani ya Tanzania siku ile ni 117,000.Nikalipa haraka benki ya Nmb halafu nikafanya mawasiliano na aliyenitumia ujumbe akanielekeza pa kwenda kufuata majibu yangu moja kwa moja kwenye maabara ya Taifa maeneo ya Mabibo kesho yake.

Kufika kule nikakuta watu wengi wamewekwa kwenye viti kusubiri lakini wengine wanaingia chumba cha uchapishaji wa vyeti na kutoka kabla yetu tuliofika mwanzo.Halafu likaja gari aina ya costa na wazungu na wachina watupu baada muda si mrefu wakaondoka wote.

Hatimae wengine tukakosa subira tukawa tunajazana kwenye chumba cha uchapishaji tukihofia kuja kuachwa na ndege na cheti kuisha muda wake.

Huko ndani hakuna anayeogopa korona si wasafiri wala wahudumu hii ni dalili kuwa corona hasa haipo kihivyo.
Cheti chenyewe ni karatasi nyeupe yenye nembo ya Jamhuri juu lakini saini ni ya fotokopi na hakuna muhuri wa maana yeyote anaweza akatengeneza.Nilipouliza nikaambiwa mihuri mengine ni huko uwanja wa ndege.

Nilidhani nikifika uwanjani nitakuta majina yametangulia kwa maafisa na ambaye hana hiki cheti hatoki.Kumbe wala shirika la ndege hawana haja nacho na hata maafisa wa afya hawalazimishi.Nilichoulizwa wakati napanda ngazi ya kuelekea uhamiaji na kuingia kwenye ndege ni jee unacho cheti nikasema ndio,Jamaa kama mgambo akasema nimpatie akatoa muhuri kama wa mitaani akapiga na wino wa bluu na wengine wengi hasa wazungu hata hawakuonesha.

Matatizo yakanikuta nilipofika Istanbul.Tayari nimefika kwenye lango la kuingia kwenye ndege kuelekea niendako wakataka cheti kingine cha korona na hiki cha kwetu wala hawana taarifa nacho.Wanataka kipimo cha kupima damu na kifua ambacho kitadumu kwa masaa 24 tangu kiandikwe.

Ndege ikaniacha na pesa sina na mamlaka ya uwanja hawataki mtu abaki ndani.Na kwa vile vipimo ni nje mjini lazima msafiri atoke atafute pa kwenda kwa gharama zake bila kujali shida zitakazompata.Hakuna wifi wala nini kuwasiliana na nyumbani wanisaidie pesa.

Hatimae nikatoka na kukaa hoteli ambayo wenyewe lazima uwalipe dola 150 kwa siku tatu mbele na kipimo nacho ni dola 150 pia.Hospitali inayopima ipo mbali na uwanja wa ndege na hoteli safari ya kwenda ni dola 40 na kurudi dola 40.Yaani kila mmoja anachuma pesa bila huruma kutokana na shida ya corona.

Kama ningejuwa mapema wala nisingepoteza pesa zangu Amana na Mabibo nikapata nguvu ya kufanya vipimo pale Istanbul.Kwa sababu cheti kile hakina maana yoyote,Hakitambuliki na shirika lolote la kimataifa na wala hakuna kilipojazwa kwenye mtandao.Kwa lugha ya kiengereza sisi tunaosafiri kwenye nchi za lugha nyengine kwanini wajipe tabu kutafsiri na kutafuta nani aliyekisaini.

Hata kama hicho kipimo cha koo na pua kinachofanyika Tanzania kingekuwa kweli kina umuhimu basi hata mimi ningekuwa afisa wa afya nchi nyengine nisingekitazama.

Kwa hivyo watanzania wanakula pesa za corona na waturuki pia na pengine kwenye viwanja vyengine vikubwa vya kubadili ndege.Unyonyaji tu.!
 
Kama wanao uhakika imkwisha na haipo tena sasa wanapima nini si washuke tu saini kwenye hivyo vyeti ?, Au itakuwa imekuja tena na huyo anayepimwa ?
 
Rushwa kuisha hakiwezekani kwa tanzania hii..hakuna kiongozi mwenye ubavu wa kulisimamia hilo..zaidi ya porojo za majukwaani tu..

#MaendeleoHayanaChama
 
Asante mkuu kwa taarifa maaana na mimi ni msafiri mtalajiwa Nilikua nawaza haya sasa nitajipanga
 
Asante mkuu kwa taarifa maaana na mimi ni msafiri mtalajiwa Nilikua nawaza haya sasa nitajipanga
Hata mimi ningepata uzoefu wa abiria mwengine wala nisingeingia hasara kumbe safari ni ndefu sana.
 
Hi, jamani naombeni maelezo kdg.mimi nmepimia Corona kgm town hospital ya mkoa vipimo huwa vinasafirishwa maabara ya taifa.na nimelipia 40 nikatumiwa conton no.na maabara ya taifa nikalipia nikapimwa Sasa nshu nikwamba majbu unapewa maada ya masaa 72 yaan cku tatu.ila Mimi siku ya tatu ilikuwa jmos sikupewa nikiuliza naambiwa subiri tunatuma hadi leo hi cjapewa naangaika na kujaribu ratiba.jmn nifanyaje?
 
Back
Top Bottom