Chenji na karaha za konda

Chenji na karaha za konda

Nchi zingine unapopanda public bus (au commuter) unatakiwa huwe na change kamili. Kama huna utakachopata ni ticket ikionyesha kuwa unadai kiasi fulani cha pesa, na ukiuliza utaambiwa ukachukuwe change yako makao makuu ya hiyo kampuni.

Kuepusha usumbufu mwenyewe utatafuta change mapema.

Makonda wengi wa daladala wanakuwa wamehajiriwa, na matajiri wa hayo mabasi na huwa hawawapi change wanapo anza kazi asubuhi, usishangae hata pesa ya mafuta ya kuendeshea hayo mabasi ni jukumu la dereva na kondakta wa siku hiyo.

Ni jukumu la abiria kutafuta change kamili, na litaepusha usumbufu na matusi ya asubuhi subuhi.

Jiulize kwanza wewe ni konda umeanza kazi na huna hizo change na abiria kama wawili hivi anakwupa noti za elfu kumi kumi, utafanyaje?

Nakuunga mkono kabisa katika hili. Lakini pia kuna wale abiria ambao haweki nauli yake karibu hadi konda adai ndo ataanza kusukumana na abiria wengine katika harakati za kuitafuta hiyo nauli hivi kuna ugumu gani mtu kupanda daladala ukiwa na nauli yako mkononi au sehemu ya karibu?

Sometimes ndo mana tunafuatwa na vibaka wanatupora mabegi/ wallets maana mtu hadi afungue lipochi lote kibaka anaona simu, nyekundu anaziona n.k
 
nikisikia wakisema konda napata kichefu chefu kabisa maana yale makwapa ni balaaa...........
 
na matusi usiseme....pesa yako mwenye lakini unatukanwa kama kawa......
Jamani hawa makonda sijui wana nini,nakumbuka siku moja asubuhi nilitoa 5000 wakat naenda kazini akaanza kugomba nikamwuliza hivi unanigombezea nini je ningepanda halafu nikakwambia sina nauli ingekuwaje nakupa pesa na bado unanigombeza,alivyoona na mimi namjia juu akaniambia na utazunguka na hii gari mpaka chenji itakapo patikana nikamwambia sizunguki na nikifika kituo nachotakiwa kushuka nitashuka ukirudi utanikuta nakusubiri nikiwa na askari na utarudisha pesa zaidi ya hiyo uliotakiwa kunirudishia kusikia hivyo mbona alianza kutafuta chenji,na akapata na nikashuka kwenye kituo nilichotakiwa kushuka,wakati mwingine akiwa mbogo na sisi abiria tunapaswa kuwa wakali akiona hivyo atatafuta chenji lakini akikugombeza ukanyamaza anakuona wewe ni mnyonge wake.
 
kweli abiria wengine wamezidi...we mtu unatoka kwako asubuhi na mapema unafika kwenye gati unampa konda 10,000 sasa hapo si unataka ubaya kwa babaubaya? ustaarabu ni kitu cha muhimu sana kwenye jamii yoyote ile na sio kukomoana
 
Abiria tuache kulalamika na tukubali ukweli kwamba, Hao Makondakta na Madereva wa hivo Daladala wameajiliwa. Na kwamba mwisho wa siku (Jioni/usiku) wanapeleka gari na pesa kwa tajiri yao (Mwenye gari ama msimamizi). Siku inayofuata, wanachukua gari (Bila pesa, si walishakabidhi jana yeke, isitoshe wanapewa kiwango kwa siku), Hivo wanapochukua gari wanaanza hiyo siku bila pesa, sometimes hata mafuta ni yakutosha trip moja tu then wanajaza kutokana na pesa walizokusanya kwa abiria.

Huku kulalamika jamani hatuwatendei haki hata kidogo. Isitoshe huwa inafikia wakati wananunua chenji (mfano, Noti ya Tsh 1000 ananunua kwa change ya Tsh 900). Hesabu ya tajiri jioni iko pale pale, haijalishi kanunua change ama kamlipa mpiga debe.

Hutaki usumbufu, nenda na hela inayotosha nauli tu, vinginevyo jiandae na hizo kejeli na matusi. Sasa wewe unampa Tsh 10,000 asubuhi asubuhi, nauli Ths 300 jamani, unategemea nini? Mbona mchana huwa sio wakorofi? (Ni kwa sababu wameshafanya kazi ama maduka, vibanda n sehemu zingine za kupata change zinakuwepo).

Ni hayo tu.

lizy
 
Nakuunga mkono kabisa katika hili. Lakini pia kuna wale abiria ambao haweki nauli yake karibu hadi konda adai ndo ataanza kusukumana na abiria wengine katika harakati za kuitafuta hiyo nauli hivi kuna ugumu gani mtu kupanda daladala ukiwa na nauli yako mkononi au sehemu ya karibu?

Sometimes ndo mana tunafuatwa na vibaka wanatupora mabegi/ wallets maana mtu hadi afungue lipochi lote kibaka anaona simu, nyekundu anaziona n.k
Ah ah ah ah ah... umenikumbusha mdada mmoja, "alijitia kumkaripia konda wakati wa kutoa nauli kuwa pesa yake ipo mbali. Konda kamsubiri wakati wa kushuka mdada akajitia kasahau, kupiga hatua mbili konda kamshukia kuchuwa nauli. Mdada wa watu akatumia dakika kumi nzima kusaka nauli kwenye kipima joto chake... Mwisho mdada akamwambia konda... ai jamani si unisamehe tu... hela yenyewe ipo mbali jamani na mimi nina haraka... konda akamshupalia akamwambia ...una haraka una har1sha, towa pesa bana wacha kunirembulia mimacho kama kinyonga karamba ugoro hapa...mpaka mdada wa watu akatoa pesa uku uso kaukunja ...!"

Kwa ukweli kazi ya ukonda na dereva wa daladala, ni moja ya kazi ngumu sana, hawa jamaa wanapata ukichaa wa muda, kwa sababu ya kukosa usingizi wa kutosha, hawa jamaa wanalala nadhani masaa matatu tu... Wanaamka saa tisa za usiku na wanamaliza kazi saa sita usiku. Unafikiria watakuwa na akili nzuri kweli?
 
Abiria ndo mnachangia kuwafanya makonda wakorofi kwa nn usiweke nauli yako peupe au kuishika mkononi unataka mpaka konda adai mara kumi ndo utoe?
 
Ah ah ah ah ah... umenikumbusha mdada mmoja, "alijitia kumkaripia konda wakati wa kutoa nauli kuwa pesa yake ipo mbali. Konda kamsubiri wakati wa kushuka mdada akajitia kasahau, kupiga hatua mbili konda kamshukia kuchuwa nauli. Mdada wa watu akatumia dakika kumi nzima kusaka nauli kwenye kipima joto chake... Mwisho mdada akamwambia konda... ai jamani si unisamehe tu... hela yenyewe ipo mbali jamani na mimi nina haraka... konda akamshupalia akamwambia ...una haraka una har1sha, towa pesa bana wacha kunirembulia mimacho kama kinyonga karamba ugoro hapa...mpaka mdada wa watu akatoa pesa uku uso kaukunja ...!"

X-PASTER yaani umenichekesha hadi nimetoa machozi..... huyu konda matusi haya kajifunza au kabuni mwenyewe? Eti haraka unaharisha na kinyonga karamba ugoro duh .... huyu dada hatakaa asahau kamwe!
 
Tatizo la makonda walio wengi ni inferiority complex,inawafanya wawe jinsi walivyo.Usafirishaji ni biashara kama ilivyo duka na biashara nyingine.Wanapaswa kujua wanadili na watu direct hivyo wanatakiwa watumie kila strategy za kibiashara ikiwa pamoja na customer care.Kama ni konda makini kwa nini usiandae chenji zako jioni kabisa ili asubuhi usipate shida na ukizingatia unakuwa umeshajua tatizo la chenji lipo?

Na hii tabia huwa inaambukiza kwa sababu kijana akija kuanza kazi anakuwa mpole sana,lakini subiri baada ya wiki moja akianza kubadilisha mboga.

Tatizo hili la customer care sio kwa makonda tu, ni kwa watanzania wengi wanaofanya biashara na hata wale wanaofanya kazi ya kuhudumia jamii moja kwa moja.

Tubadilikeni wa TZ tuwe na mtizamo wa kibiashara zaidi na sio kuridhika na vimafanikio vidogo
 
Bangi si mchezo, abiria wote unawaona ka sisimizi!

All in all kazi ya konda ni ngumu sana usipime kabisa, wengine hamlipi hata nauli humu mnajikausha hasa kwenye daladala zetu za kusimama.

Mkuu Fidel wewe daladala zote za kutoka ubungo kwenda kimara/mbezi ni staff ndo maana unawatetea sana makonda bana!!.
 
.Kama ni konda makini kwa nini usiandae chenji zako jioni kabisa ili asubuhi usipate shida na ukizingatia unakuwa umeshajua tatizo la chenji lipo?

Ziondaughter:

Je unaweza kutuambia hawa makonda waandae vipi hizo change in advance? Kumbuka mwisho wa siku/kazi wanakabidhi pesa kwa Tajiri/mwenye gari/Msimamizi. Sasa sijui waandae hizo change kutoka wapi labda?
 
UTUMWA mwingine wa ajabu sana, viburi vya makondakta vimewafanya watu sasa wanapotoka kazini kabla ya kufika nyumbani waanze kuchenji kwenye maduka ya jirani noti zao. Unajua kwa nini? Wanaogopa matusi ya makondakta asubuhi, bila hiyana makonda wengi wamekuwa wanatoa matusi kwa watu wanaotoa manoti kama Ntenze au wekundu wa Msimbazi.

Unakumbuka Nteze John alikuwa mchezaji wa Pamba na Simba miaka ya 90 akilisakata kabumbu nambari 10 hadi noti ya Sh 10,000 ikabatizwa jina la Nteze.

Wasiofahamu msamiati huo wawaulize wanahabari ni mabingwa wa kuutumia. Wanautumia wakati gani, sina jibu lakini Nteze ni moja ya lugha zao kubwa wanazozitumia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Wanayo misamiati mingi mara kiasi cha vumbi, changarawe na kiasi cha lami, nisiendelee mbele wasije wakaona nawasakama bure. Sasa ukitaka kujua hasira ya konda wakati wa asubuhi wewe mpe hiyo Nteze au tu mpe nusu Nteze uone, atakakusakama hadi siku utaianza vibaya.

Akikusamehe sana atakusonya bila kificho. Ataanza ‘kwa nini utoe fedha kubwa asubuhi hii, yaani wewe unapotoka nyumbani kwa nini usijiandae kuchenji fedha yako au unataka kupanda bure”.

Maneno kama hayo yatamtoka kondakta kana kwamba una ugomvi naye. Mara nyingi anatafuta sapoti ya abiria wengine. Sasa ukute abiria wasio na ustaarabu nao watadakia, aha! Watu wengine bwana wasumbufu kweli asubuhi yote hii kwa nini atoe Nteze.

Fedha yako na nauli umetoa, lakini matusi yanakuandama. Juzi kwa macho yangu nimemshuhudia abiria aliyekuwa anashukia kituo cha Kongo akitoa noti ya Sh 5000, konda akakataa kumrudishia chenji yake kwa madai kuwa hakuwa nayo. “Kaka twende hadi mwisho wa safari ndo nitachenji wewe unatoa noti unafikiria mimi nitatoa wapi chenji asubuhi hii.”

Kijana akawa mpole, akawa hana budi akaendelea na safari aliyolazimishwa hadi Mnazi Mmoja. Konda akachenji kijana akaanza safari ya kupiga mguu kurudi Kariakoo. Hiyo ndio biashara ya usafiri wa Bongo ni karaha tupu! Hebu tujiulize hivi nani mwenye jukumu la kutafuta chenji ni la abiria au la kondakta. Sio kwamba nawapendelea abiria lakini jukumu lake ni kutoa nauli.

Kondakta anajua fika kuna abiria watatoa Nteze ni jukumu lao kuwa na chenji. Abiria anyongwe kama hana nauli lakini sio atoke kazini kachoka aanze tena kutafuta chenji, huo ni utumwa na unyanyasaji. Abiria kataeni kuburuzwa na makondakta wachacharike kuhakikisha wanakuwa na chenji.
http://www.habarileo.co.tz/safu/?n=3320

Ndugu MziziMkavu shukran sana kwa kutupasha habari kuhusu Kero za makonda asubuhi asubuhi.

Yafuatao ni mchango kwa ufupi kuhusu suala hilo.

Mimi kama mpenda usawa awali ya yote napenda kusema kuwalaumu makonda pekee yao itakuwa kuto watendea Haki na ni kuwa vunjia Heshima.

Haki itatendeka tukiangalia pande zote za sarafu kisha kutoa hukumu sahihi.

Nionavyo mimi binafsi ni Ma-Konda na Ma-Abiria asubuhi asubuhi watoao Stenzi na Denzi wote ni wenye kulaumiwa sio makonda pekee yao.

Nasema hivi kwa sababu Makonda kutoweka chenji kwa ajili ya abiria ya kwanza na pili hadi wa tatu ni wenye kulaumiwa.

Na Ma abiria kutokwenda na chenji 10300 pia wanastahili lamawama na fundisho.

Nataraji kwa ufupi huu nitaeleweka kwa undani kama sivyo tuendelee kujadiliana hadi kufika kilele cha hitimisho.

Wenu katika Utu
Mpenzi wa Islam.
 
Back
Top Bottom