Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,067
- 34,829
UTUMWA mwingine wa ajabu sana, viburi vya makondakta vimewafanya watu sasa wanapotoka kazini kabla ya kufika nyumbani waanze kuchenji kwenye maduka ya jirani noti zao. Unajua kwa nini? Wanaogopa matusi ya makondakta asubuhi, bila hiyana makonda wengi wamekuwa wanatoa matusi kwa watu wanaotoa manoti kama Ntenze au wekundu wa Msimbazi.
Unakumbuka Nteze John alikuwa mchezaji wa Pamba na Simba miaka ya 90 akilisakata kabumbu nambari 10 hadi noti ya Sh 10,000 ikabatizwa jina la Nteze.
Wasiofahamu msamiati huo wawaulize wanahabari ni mabingwa wa kuutumia. Wanautumia wakati gani, sina jibu lakini Nteze ni moja ya lugha zao kubwa wanazozitumia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wanayo misamiati mingi mara kiasi cha vumbi, changarawe na kiasi cha lami, nisiendelee mbele wasije wakaona nawasakama bure. Sasa ukitaka kujua hasira ya konda wakati wa asubuhi wewe mpe hiyo Nteze au tu mpe nusu Nteze uone, atakakusakama hadi siku utaianza vibaya.
Akikusamehe sana atakusonya bila kificho. Ataanza kwa nini utoe fedha kubwa asubuhi hii, yaani wewe unapotoka nyumbani kwa nini usijiandae kuchenji fedha yako au unataka kupanda bure.
Maneno kama hayo yatamtoka kondakta kana kwamba una ugomvi naye. Mara nyingi anatafuta sapoti ya abiria wengine. Sasa ukute abiria wasio na ustaarabu nao watadakia, aha! Watu wengine bwana wasumbufu kweli asubuhi yote hii kwa nini atoe Nteze.
Fedha yako na nauli umetoa, lakini matusi yanakuandama. Juzi kwa macho yangu nimemshuhudia abiria aliyekuwa anashukia kituo cha Kongo akitoa noti ya Sh 5000, konda akakataa kumrudishia chenji yake kwa madai kuwa hakuwa nayo. Kaka twende hadi mwisho wa safari ndo nitachenji wewe unatoa noti unafikiria mimi nitatoa wapi chenji asubuhi hii.
Kijana akawa mpole, akawa hana budi akaendelea na safari aliyolazimishwa hadi Mnazi Mmoja. Konda akachenji kijana akaanza safari ya kupiga mguu kurudi Kariakoo. Hiyo ndio biashara ya usafiri wa Bongo ni karaha tupu! Hebu tujiulize hivi nani mwenye jukumu la kutafuta chenji ni la abiria au la kondakta. Sio kwamba nawapendelea abiria lakini jukumu lake ni kutoa nauli.
Kondakta anajua fika kuna abiria watatoa Nteze ni jukumu lao kuwa na chenji. Abiria anyongwe kama hana nauli lakini sio atoke kazini kachoka aanze tena kutafuta chenji, huo ni utumwa na unyanyasaji. Abiria kataeni kuburuzwa na makondakta wachacharike kuhakikisha wanakuwa na chenji.
http://www.habarileo.co.tz/safu/?n=3320