Chenge,Werema: Tume imedanganya kiasi kilichopo kwenye mchanga, wajivua lawama

Umeliona Tanzania Daima tu Mtanzania hujaliona

Kwa akili hizo ndio tutashindwa kuibiwa kweli?
Tanzania daima =mbowe

Mtanzania =Rostam Aziz/Lowassa/Bashe.

Sasa ata waki report izo habari uwezi kushangaa au kujiuliza kuna nini hapo?

Na cha kuongezea kwanini waende kuwauliza na kuwaoji wanasheria ambao wanahukakasi na ndio wanatuhumiwa kutuingiza kwenye mikataba mibovu?

Na kwanini wapinge report ya wataalamu wa madini wakati wao ni wataalamu wa sheria na walijuaje tume ilidanganya? Ukiangalia hapo utaona ule msemo jiwe limepigwa gizani na watajitokeza wengi tu.

Ningekubaliana na ukosoaji wa chenge na werema kama report ingekuwa ya kisheria ndio uko utaalamu wao waliobobea.
 
View attachment 515116 View attachment 515111 Haya mambo ni kuyatazama kwa umakini sana.Wazungu huwa hawaibi "kijingajinga",wanaiba kwa umakini sana,tena wanakuibia kwa wizi wa "kisheria" ulioupitisha mwenyewe bungeni.

Unaposema mikataba ya madini yote,basi unamzungumzia Andrew Chenge na Mzee Mwakalukwa!!Hawa lazima maoni yao uwe makini nayo sana,maana wamekula sana 10% za hawa wawekezaji wakati wa kuandaa na ku-sign mikataba hii.

1998,wakati bunge la kina JPM,Chenge,Mkapa na JK wakipitisha sheria za madini kwa hati ya dharura,Tundu Lissu alikuwa "korokoroni" kwa kuipinga miswaada hiyo,CCM walipitisha mikataba hii kwa uwingi wao na kura za "NDIOOOOOOO"

Hivi mdivyo walivyofanya kwenye mikataba ya mafuta na gesi...Mpaka leo licha ya kuuwa watu na kupeleka jeshi Mtwara,hakuna lolote la maana kuhusiana na gesi.

Hii ni "Political Milage" ya kina Polepole na team yao,lakini itakumbana na upinzani wa ndani ya mfumo na chama.Huwezi laumu wizi wa madini bila kumkamata Chenge,Mkapa na Yona.Lissu aliwaambia miaka na miaka wakafumba macho

Mzungu sio mjinga kiasi hiki...Licha ya Chief Mangungo kutojua kusoma wala kuandika,bado Wajerumani chini ya Carl Peters walimsainisha "mkataba" wa kuuza himaya yake...ili waichukue "kwa uhalali wa mkataba"...Kama 1880's Mzungu alituibia kwa "mkataba",unafikiri leo ataiba "kijingajinga"??

Mikataba hii itawasomba kina Mwandosya enzi akiwa Katibu Mkuu Nishati,kina Chenge kama wanasheria na wasimamiaji wa mikataba...Kama ni wizi,basi hawa CCM na kina Polepole wawe wakwanza kuanza kufumua toka ndani ya chama chao...Vinginevyo ni yaleyale ya kutujaza hasira ili wapate ahueni ya kisiasa!!Tutafakari kwa pamoja!!!

Chenge ni mwizi number moja. Mkono wa Chenge uko kwenye Huu mchanga. Nashangaa mpaka Sasa yuko bungeni. Chenge hafanyi kazi kwa niaba ya Watanzania. Chenge yuko UPANDE wa ACACIA. Sasa hivi atatuambia anawashahuri namna ya kupigana na Watanzania kama alivyofanya kwenye account ya Escrow. MAAJABU bado yuko bungeni Tanzania imekwisha, inalala kitanda kimoja na maadui wake eti wanasheria. Rais Magufuli ana maadui wengi wanaomuzunguka, lazima afunguwe macho na masikio.
 
Kweli nimeamini sasa hata Chenge mzee wa mapesa ni kipenzi cha watu!!!!!!!!! Tanzania kweli imeendelea.
Adui namba moja wa watanzania ni serikali yenyewe. Chenge ana makosa yake kama walivyo mamber wengine wengi tu wa serikali kwa miaka mingi iliyopita. Ila tusimbebeshe zigo lote hili la issue ya madini as if alikuwa anafanya peke yake. Kama watawala wangekuwa na nia ya dhati kuhakikisha rasilimali zinatunufaisha wote then Mzee Chenge asingekuwa na influence yoyote. Tatizo nchi nyingi za Kiafrika vyama vya siasa vinavyotawala hugeuka magenge ya uporaji, huku wakiishi kama familia, kama ndugu wanaounganishwa na kitu kimoja kikubwa, kujilimbikizia mali kwa gharama yoyote. JPM anaonyesha nia lakini mikakati na namna ya kujenga teamwork kufika huko inamchanganya sana, aina ya wanaomzunguka na aina yake ya utawala itakuwa changamoto kubwa sana kufika tuendako.
 
ahaaaa..... Andrew Chenge kaua hapa
''Rais ameshatoa maoni yake , kuna marais wawili hapa?, Nani alikwambia nilikua mwanasheria mkuu wa serikali? Mbona nyie wagonjwa gonjwa kidogo? Mnaonekana kuwa na ugonjwa.
 
Nina uhakika Tume ya JPM ya Makinikia imemdanganya sana Rais na Watanzania. Nina ushahidi ufuatao:

1. Wamewaaminisha watanzania kuwa kwenye kila kontena moja tunapoteza 1 Trillion shilings badala ya 300m walizosema Acacia. Hapa wanacheza na akili zetu na za JPM kwa kutaja figure hiyo kubwa wakati wanajua wazi kuwa hayo makinikia hayakushuka kutoka mbinguni. Kuna mtaji wa awali ulitumika yaani capex, kuna gharama za uzalishaji yaani opex na za usafirishaji. Chetu ni 4% ya hiyo 1Trillion ambayo ni 4Billion tu. Ili kuleta mtikisiko wa bongo zetu wakaona waseme tunapoteza 1Trillion kwa kila kontena badala ya kusema 4Billion. Lengo lao ilikuwa nini?

2. Mfumo waliotumia kukokotoa thamani ya madini ni wa uongo, maana wame assume kuwa recovery ni 100% kitu ambacho hakiwezekani. Hata kiwanda cha sukari hakina recovery ya 100% kwenye miwa iweje madini! Kwa teknolojia ipi utapata hiyo kitu?

3. Sampling method waliyoitumia inatia mashaka, ndio maana taarifa yao haiwekwi wazi ili sisi wajuzi wa sampling tuwakosoe. Aidha Lab ya GST waliyoitumia haina ISO hivyo haikubaliki kimataifa. Utamuitaje mtu mwizi kwa lab results za GST? Watuambie lab ipi zaidi ya GST waliyotumia yenye ISO. Vinginevyo ni kudanganya umma na kuiweka nchi kwenye hatari ya kushitakiwa kimataifa.

4. Hawakujipa muda kuhoji unalali wa resuts zao. Walipaswa kujiuliza maswali yafuatayo na kujijibu, je kwa results hizi ni kweli kuwa Acacia ni mzalishaji namba moja wa dhahabu duniani? Kama ndio, kwa nini wanaficha ukweli huo kwani si ingewasaidia kuongeza hata bei ya share zao kwenye soko? Je haya madini ya ziada tuliyoyaona zaidi ya dhahabu, shaba na fedha wanayoripoti serikalini je yanaweza kuchambuliwa kwa gharama gani na faida ikawepo au haiwezekani? Je wao Acacia wanalipwa hayo madini kama sio kwa nini wanakubali kupoteza fedha hiyo? Je kama wanalipwa, hiyo fedha ya ziada inaingia kwenye akaunti gani ambayo sisi hatuijui na je inawezekana hata USA na Canada hawaijui? Je serikali kupitia TRA na TMAA wanavyokagua financiàl records za Acacia huwa hawayaoni hayo mafedha ya ziada? Je hizi findings zetu ziko in line na taarifa za explorations na Feasibility study za migodi hiyo au tumegundua kitu kipya? Nina uhakika wangejiuliza maswali hayo wangedrop hizo findings za uongo na kuokoa nchi kwenye aibu hii.

5. Tume hawakuchukua tahadhali kutoa conclusion hizo ambazo zinaituhumu Acacia kuwa ni wezi na watendaji ni wazembe. Hatari iliyopo ni impact yake kwenye jamii na kwa watuhumiwa. Ona sasa share za Acacia zimeporomoka na watendaji wamesimamishwa kazi na wanachunguzwa bila hata kusubiri ukweli halisi kujulikana. Hii ni pigo kubwa kwa watu hao. Ndio maana naunga mkono hoja ya serikali kuyanunua makontena hayo na kuyapeleka kwa marafiki zetu china kuyachakata ili tuone kama hayo madini aloyoyasema Prof Mruma yatapatikana. Yaani Tume itaumbuka mchana kweupe na serikali itapata hasara kwa kuaminishwa na hawa maprofesa waliopika data ili kupata vyeo.

Nashauri JPM awaite hao wajumbe wa tume wathibitishe mapema ukweli wa hizo data zao ili ikija kutokea tofauti wanyongwe. Ni maoni yangu, Msema Kweli Mpenzi wa Mungu.
 
Acha kupotosha hao ni wezi watanzania aliyeturoga kafa mnatetea acacia sasa.pathetic
 
Jamani nisameheni, naombeni kujua professional ya change,

Tafiti hupingwa Kwa Tafiti sasa yeye kafanya tafiti gani hadi aje apinge hiyo tafiti? Naona Kuna watu wanamsapot chenge duuh watanzania wengine sijui vichwani mwao kuna vitu gan
Dr.Mwele alipingwa kwa tafiti ipi?
 
Mahakamani mtatushinda ila wananchi tunashindwa hata kuwapopoa kwa mawe wahaini hawa?
Tukishindwa basi jichawi, mshana jr, MziziMkavu na Bujibuji tukikaa kama kamati ya ufundi twaweza fanya jambo
Mkuu Bujibuji,kwa nini kamati yenu ya ufundi msianze kuiroga CCM ipotee ili tuwe na uhakika wa kuwa na Taifa bora kwa kizazi na kizazi kuliko kuwaroga Acacia then kesho maCCM yanaendeleza u KKK zao kwenye maswala ya msingi?
 
Adui namba moja wa watanzania ni serikali yenyewe. Chenge ana makosa yake kama walivyo mamber wengine wengi tu wa serikali kwa miaka mingi iliyopita. Ila tusimbebeshe zigo lote hili la issue ya madini as if alikuwa anafanya peke yake. Kama watawala wangekuwa na nia ya dhati kuhakikisha rasilimali zinatunufaisha wote then Mzee Chenge asingekuwa na influence yoyote. Tatizo nchi nyingi za Kiafrika vyama vya siasa vinavyotawala hugeuka magenge ya uporaji, huku wakiishi kama familia, kama ndugu wanaounganishwa na kitu kimoja kikubwa, kujilimbikizia mali kwa gharama yoyote. JPM anaonyesha nia lakini mikakati na namna ya kujenga teamwork kufika huko inamchanganya sana, aina ya wanaomzunguka na aina yake ya utawala itakuwa changamoto kubwa sana kufika tuendako.

Hebu nieleze, huyu mtu anayeitwa serikari ni nani? Na Anafafaje? Anakaa wapi? Serikali ni group la watu wanaochaguliwa kuunda serikali na Chenge alikuwa mmojawapo, alikuwa kati ya wana sheria. Pana ushahidi mkubwa nafasi yake ameitumia vibaya kujitajirisha mwenyewe kwa shida za Watanzania. Hakuna mtu anamuonea Chenge, Chenge anawaonea Watanzania kuzungumza nao kwa dharau na kutuona hatujui kitu. Usimuonee huruma Chenge, jionee huruma wewe mwenyewe. Chenge ni Mabutu Seseko ana mabilioni ya Watanzania nchi za nje, muulize kupata wapi hawezi kukuambia. Kazitowa mifukoni mwa Watanzania.
 
Ule ni mwenge au sanamu!!!
Kuwashwa na kukimbizwa kwa huo mwenge wenu si bure.....kuna kitu.
Kuwe na kitu au kusiwe, do not limit THE ALMIGHTY SOVEREIGN CREATOR kwa ki piece cha kimoto! Mwenye Enzi Mungu ni mkuu sana!
 
I presume they are very aware of what is the practice...Kwanini watu wana draw conclusion hizo bila kwanza kujiuliza? Hawa tume wamecheki mchanga uliokuwepo kwenye containers. Na wametoa angalizo kuwa scanner haina nguvu kiasi cha kuweza ku ona the content. Kwanini basi wasijiulize je huu mchanga unafanana na ule unaochimbwa au la? What if it was amongst many ways ya kutorosha madini? Kwani hawawezi kuchanganya gold yenyewe na mchanga kwa njia zao huku wakijidai ni concentrate wkati humo kuna dhahabu ambayo siyo amalgamates? Then wanakimbilia kusema ooh mchanga hauna hiyo concetrates etc? La pili; Je wanaposema any of commercial value what does that infer? Hawajiulizi maswali kama hayo wanakimbilia ku conclude bila ku deduce kama tume ilivyofanya...Tume ilienda kuchunguza contents zilizomo kwenye container siyo what is contained in the mgodi ambacho hakijachimbwa...Unless I did not understand their ToR...Kama hadidu za rejea ni kilichomo huwezi kutumia sample nyingine zaidi ya ile iliyokuwa packed kutolea conclusion, wao wana base kwenye nini kufikia hiyo conclusion kuwa tume imedanganya? Walienda kupima hizo content za kwenye containers? Hii tu inatufanya tu suspect kwamba wanajua kinachoendelea ndiyo maana wanapata confidence ya ku conclude Rais anadanganywa...

Hakuna facts ambazo zinasimama zenyewe bila kuweka objectives and when the objective change hizo facts haziwezi endelea ku hold water...Hadidu za rejea ndiyo ilikuwa frame ya uchunguzi huo. Hawa hawakuwa wanafanya utafiti wa what is the level of gold and other minerals concentrations kwenye rocks iliyopo kwenye migodi tuliyonayo kitu ambacho wengi ndicho wanachoki base katika arguments zao. Hawa walikuwa wana determine contents na extents za hizo contents katika defined packages kama zinafanana na declarations zilizofanywa na hao walio fanya the same proceedures wanayofanya wao.
Nakubaliana na wewe mkuu wengi wanajua tume ilienda kuchunguza madini hadi ya ardhini
 
Werema na Chenge wanatoa argument za kimaskini sana sijui walifikaje hapo walipo nashangaa au mtu akianza kuwa mzee akili zinapungua?Chenge na Werema wamesoma combination either History, Geography na Language au vinginevyo ambapo ni fully art hakuna hata chembe chembe ya 1+2 sasa leo waliosoma (8/2*3+2-1)=13 yaani BODMAS mnabishana nao kweli nchi hii wakati nnaitafuna mlizani hatutakuja kujumlisha na kutoa? tulieni dawa iwaingie Mhe.Rais endelea kubomoa ukuta tu

Chenge sio mzee, ni mwizi. Mwizi hamushiki mwizi mwenzie. Chenge ana historian ya kuwaibia Watanzania. Chenge ni tajiri mkubwa, tajiri bila ya kufanya kazi. Chenge yuko kwenye kila janga kwa wizi Tanzania. Kwenye rada, Escrow, na wizi wa kila aina. Chenge ni mufano wa Mabutu Seseko wa Tanzania. Chenge anajuwa wizi wote unaotokea hapa kwetu, cha ajabu bado anapiga suit, na bado yuko bungeni. Nashangaa katiba yetu ina inaruhusu watu wenye mikono michafu wenye sifa za wizi wanakuwa Viongozi wetu. Chenge kwenye nchi zenye kupenda haki leo hii Chenge angekuwa anafundisha sheria gerezani.
 
Chenge sio mzee, ni mwizi. Mwizi hamushiki mwizi mwenzie. Chenge ana historian ya kuwaibia Watanzania. Chenge ni tajiri mkubwa, tajiri bila ya kufanya kazi. Chenge yuko kwenye kila janga kwa wizi Tanzania. Kwenye rada, Escrow, na wizi wa kila aina. Chenge ni mufano wa Mabutu Seseko wa Tanzania. Chenge anajuwa wizi wote unaotokea hapa kwetu, cha ajabu bado anapiga suit, na bado yuko bungeni. Nashangaa katiba yetu ina inaruhusu watu wenye mikono michafu wenye sifa za wizi wanakuwa Viongozi wetu. Chenge kwenye nchi zenye kupenda haki leo hii Chenge angekuwa anafundisha sheria gerezani.
Hakika wewe unamjua chenge alitakiwa kuwa Segerea anafundisha sheria
 
Nawashangaa wasiomjua, ukizungumzia mikataba hovyo ya madini nchi hii unamzungumzia chenge!
Lakini maCCM mnampitisha kuwa mbunge kila muhula,na mkampa uenyekiti wa bunge. Nani alaumiwe? Mwananchi wa kawaida ambaye ameaminishwa kuwa Chenge ni fisadi mkubwa lakini wenye mamlaka hawampeleki kwenye mahakama ya mafisadi zaidi ya kumuongezea mavyeo au yule mtu mwenye mamlaka na uwezo wa kumuwajibisha lakini hafanyi hilo?
 
Back
Top Bottom