watu wanatembea na chequrbooks mifukoni mazee. pia na banks zote wanawekwa watu standby kuchota hela yoyote itakayotakwa na cour. afterall court sansana ikukandaniza ni vijisenti tu, hakuna fine ya kumletea tumbo la kuhara mtu kama chenge katika mahakama zetu.
hivi hukumu yake imesomwa ? kahukumiwa hiyo fine au hiyo fine ni ya nini?
kama seria imefuatwa, hakuna shida. ila sijui kama kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kutakuwa na consequenses gani hasa kwenye ubunge wake. mtujuze jamani mnaofahamu
Sasa kosa la Chenge liko wapi hapo? Kama ameambiwa nenda jela au lipa laki saba na yeye anayo laki saba mfukoni akailipa si ndo anapeta tena au! Unless afunguliwe mashitaka mengine ya kuvuliwa Ubunge kwa kuwa amekutikana na hatia kwenye mahakama (ambayo sijui kama kuna sheria inayomkataza kuwa mbunge kwa kupewa hukumu kama hiyo)
Hii faini ya Laki saba kwa roho za watu wawili ndipo nnapokwazika na hizi sheria za Tanzania.
Hukumu ya kutoa laki saba pia ni kwa sababau amekuwa kigogo tu kwan mtaani kwetu mtu akigongwa na gari hata kama dereva ndio mwenye makosa utaona mwisho wa siku faini elfu ishirini au jela miezi sita wakati kakatisha maisha ya mtu.
Sometimes hata kessi haifiki polisi.
Binafsi naona mfumo wetu wa sheria sio mzuri labda wanasheria watuelimishe vizuri tuweze kujua hali halisi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.