FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
Mimi nitaungana na wewe baada ya Kikwete kukamata walioiba fedha BOT (EPA), Meremeta & Tangold, Twin Towers (BOT), Richmond na Import Support. Sioni kama ni ujasiri kwa haya yaliyotokea.
Bado Kikwete na Serikali yake wameshindwa kuwa wawazi, waseme basi Chenge aliandika hiyo akaunti kwenye fomu ya maadili?
Ila nitakuwa si mkweli nisipokubali kwamba Kikwete amefanya vizuri kuvipa uhuru vyombo vya habari, namwombea kwa Mungu ili aendelee kuwa mvumilivu na kuviacha vyombo vya habari vifanye kazi yake.
tunamtaka Rais JK aje hapa atuombe radhi watanzania wote kwa kutuchagulia viongozi mafisadi.
na tuombe radhi tena kwa kutuchagulia viongozi mafisadi mara mbili kwenye baraza lake.
na aje atuombe radhi KABISA kwa waziri mpya atakayetuchagulia kwa vile na huyu atakuwa bogust kama wale waliotangulia.
Tunasubiri kwa hamu MAGUFULI wetu arudishwe miundo mbinu ili akarekebishe mambo ambayo CHENGE alianza kuyaboronga boronga. Nimeamini na kujifunza kuwa: UFISADI + UJEURI= KUKOSA HESHIMA MBELE YA JAMII.
Kujiuzuru ni atua ya mwanzo, vijisenti vyetu atarudisha lini?
Serikali hii ikifika 2010, nchi hii itakuwa imechoka sana nawaomba watanzania wenzangu tuunganisshe nguvu kupambana na mafisadi, wasioitakia mema nchi hii.
Rais hafanyi kazi hivyo, hata kama ni kweli sisi ndio tumemuajiri.
Kuchagua viongozi inabidi upewe information, vipi kama system haiko safi na anapewa uongo?. Msimlaumu sana tumpeni muda taratibu anasafisha.
Si unakumbuka Chenge alisema HAJIUZULU? nini unafikiri kimemfanya ajiuzulu?
BIG UP to Muungwana.
You are right, Hiyo ndio Style ya Kikwete na wazaramo wote, kujikosha, hawapendi kuonekana wabaya kila upande
Chenge kafukuzwa hakujiuzulu.
Hivi hii ni trend ya kujiuzulu au amefukuzwa?
- Majuzi akiongea na waandishi, Chenge alisema hatajiuzulu.
- Jana Kikwete akaingia DSM akitokea NYC, nafikiri hakusubiri hata hotuba ya Pope UN.
- Then, jana hiyo hiyo, Chenge anatangaza kuomba msamaha kwa kutumia neno vijisenti.
- Leo hii anatangazwa kuwa amejiuzulu.
Kama amefukuzwa au kulazimishwa kujiuzulu (which is one and the same), kwa nini alidhani kuwa hatafukuzwa? Lipi lililokuwa linalazimisha yeye kuwapo madarakani hata baada ya kukataliwa na umma? Haya maswali yanahitaji majibu.
LOWASSA alijiuzulu au kufukuzwa..?
balali alijiuzulu au kufukuzwa..?
nadhani hoja hapa iwe ameondoka basi!!
njia aliyoondokea anaijua yeye..
kwani warren G ..WETU Hapendi kumuudhi mtu..au hawezi kumuambia mtu jambo usoni...sijapata kusikia tangazo kutoka ikulu likisema.."..rais ...ameamua kumfukuza kazi....kwa kosa la..." muda mrefu sasa....
JF Admin., please we need to introduce vote of "NO THANKS" teh teh teh!Mimi naamini kabisa kama Mh.Kikwete ni msafi tena msafi wa uhakika...
Aidha, waandishi walipotaka kujua kama kiongozi huyo ameorodhesha mali zake kwenye fomu ya Tume ya Maadili kama ambavyo sheria inaelekeza, Pinda alisema fomu za kiongozi kuorodhesha mali ni suala binafsi, hivyo si rahisi yeye (Waziri Mkuu) kufahamu kiasi cha mali alizonazo ama alichoorodhesha.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/4/21/habari3.php
Naomba msaada ni kweli kuorodhesha mali ni la siri????
Hili sio tatizo la JK!!! Ni tatizo la kitafa...
Kuwa makini kidogo, Sio kila kitu ni cha Rais vingine ni vya jamii nzima tuliyonanyo!!! sasa imebadilika... lazima tuelewe hivyo... Na JK anatuongoza vyema kwenye mabadiliko haya kwa kukubali wanaojiuzulu wajiuzulu...
- Nani alimchagua Chenge kuwa Mbunge ambayo ndiyo sifa no.1 ya kuchaguliwa kuwa waziri?
- Nani alimchagua Chenge kuwa mjumbe wa NEC ya CCM? JK au wanaCCM?
Sitaki ieleweke kwamba Wabunge na Madiwani wa CCM hawana haki ya kuikosoa Serikali. Wanayo haki hiyo. Lakini, kuna tofauti ya kukosoa utekelezaji wa sera, ambao ni wajibu wa Wabunge na Madiwani wa Chama Tawala; na kukosoa sera yenyewe, ambao ni wajibu wa Wabunge na Madiwani wa Upinzani. Katiba na busara zinataka tupambanue wapi na lini tukosoe sera na utekelezaji wake. Mbunge na Diwani lazima aamue yuko upande gani
Chama Cha Mapinduzi ndicho hasa kiongozi wa nchi hii. Au tuseme hivyo ndivyo inavyopasa kuwa. Chama kwanza, mtu baadaye. Ndiyo maana huko nyuma tukasema, "Chama legelege huzaa Serikali legelege". Nami leo naongeza: Chama shupavu, huzaa viongozi shupavu.
Mtaalamu mmoja wa menejimenti alisema: "Wajibu wa kwanza wa kiongozi ni kuwafafanulia anaowaongoza hali halisi." Kama Chama Cha Mapinduzi kinataka kuendeleza sifa zake za uongozi, na nguvu yake katika siku za usoni, lazima kiwe chama shupavu, chama kisichoogopa kusimamia maadili yake, chama kisichoogopa kusema ukweli, chama cha kuwafafanulia wananchi hali halisi ya tulipo, na mahitaji na masharti ya mafanikio ya huko tuendako.
Tunahitaji ushupavu wa uongozi. Nikiwaulizeni hapa mmojammoja, nina uhakika wengi watasema kuwa zimeanza kampeni za chinichini huko mikoani na wilayani. Wengine wameniambia wapo wenye mkakati wa kununua wajumbe wa Mikutano Mikuu ya Wilaya, Mikoa na hata Taifa. Kama ni kweli, ujasiri wa viongozi huko mliko wa kusimamia maadili uko wapi? Kwa nini sisikii viongozi wa CCM wanaokerwa na hali hiyo wakiikemea katika vikao vya ndani? Kwa nini taarifa za namna hiyo haziji rasmi, kwa taratibu zetu, lakini zinakuja kwa njia ya tuhuma, minong'ono na kupakana matope? Waasisi wetu wasingekuwa jasiri na shupavu tusingepata uhuru, wala kufanikisha Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Ujasiri na ushupavu wetu sisi, tunaodai haki ya urithi wa waasisi wetu, uko wapi?
Nimesoma thread hii ndefu sana na ninayo machache ya kuchangia
(1) Tangia siku ya kwanza alipoleta baraza kuuuuuuubwa, JK alionekana ni mlipa fadhila na hatakuja na jipya
(2) Alipopewa angalizo la kutopandisha kodi za mafuta kwa kuwa ataathiri uchumi mzima, akakataa yeye na Meghji kwa madai kuwa hapo ndo tutapata hela maana kila mtu atumia mafuta, aliashiria kuwa Rais asiyetumia walau elimu yake ya uchumi aliyopata UDSM
(3) Shutuma za ufisadi zilipotolewa na yeye hakuona ni vema kuzishughulikia, saaaaana akiwa kanisani alitoa mwito wa watu wa kutokuwa mahakimu, aliendelea kujaza kikombe chake cha kuwa Rais asiye msikivu wa kilio cha wananchi wake
(4) Hata baada ya Lowassa kuanguka, anakuja na maneno ya kuwa alikuwa mchapakazi na kumlilia, alielekea kutoona haja ya kuwa Rais makini mwenye kulinda maslahi ya walio wengi
(5)Chenge alisemwa na wengi kutoingia baraza jipya ambalo nalo liko hoi tu kama la mwanzo...JK kwangu mimi nilimwona ana mkono katika ufuska huu wa VIJISENTI
Mimi nakubaliana na wote wanaosema amevipa vyombo vya habari uhuru..lakini utendaji wake ni wa mashaka, woga, kulipa fadhila, na ni sifa zisizofaa kwa kiongozi mkubwa wa nchi.
Ninaomba wana JF, tuchangie nini kifanyike ili Chenge, Mkapa na mkewe, Yona, Abdala Kigoda, Mramba, Rutabazimbwa, Mgonja, Lowassa, Rostam, Karamagi (orodha ni ndefu) wafanyiwe ili tuondokane na jinamizi hili la ufisadi...
Huwa naona suluhisho moja ambalo haliwezekani kwa wengi
ASSASSINATION (one after another) huenda wataogopa? huenda CCM watafunguka macho waone hee kumbe hivi viti vya moto eeh??
Actually data ni kuwa CHENGE ana £15 million kwenye account moja na wala si £1million kama ambavyo wengi wanavyoamini