Chemsha Bongo!

Chemsha Bongo!

Columbus

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
2,002
Reaction score
652
Kuna kajimtihani kadogo,umeenda dukani kununua sukari kilo 1 lakini kwa bahati mbaya mwenye duka hana jiwe la kilo moja lakini ana jiwe la kilo 10 na la kilo 7.Swali atafanyaje ili aweze kukupimia hiyo kilo moja ya sukari kwa kutumia mawe hayo mawili!
 
toa jibu Mwenyewe
 
Kwanza kabisa unapima sukari kilo 10 , baada ya hapo unachukua sukari kilo 10 ulopima unapunguza kilo 7 kwa kutumia jiwe la kilo 7, hapo itabakia kilo 3. Baada ya hapo pima tena sukari kilo 10 halafu changanya na ile kilo 3 ilobaki, hapa utakua na kilo 13. Tumia jiwe la kilo 7 punguza kilo 7 kutoka kwenye kilo 13 ulizonazo, hapo utabaki na kilo 6. Sasa pima kilo 7 kisha tumia ile sukari kilo 6 kama jiwe la kilo 6 kupunguza kilo 6 za sukari kutoka kwenye kilo 7 ulizopima, ambapo hapa utabaki na kilo 1 ambayo ndo tunayohitaji.... One more chemsha bongo please...!
 
Chukua jiwe la kilo 7 pima kilo saba za sukari weka kwenye mfuko,pima tena kilo 7changanya na zile 7 ziwe kilo14,ongeza tena kilo 7 ziwe kilo 21.Sasa chukua huo mfuko wa kilo 21 kwa jiwe la kilo 10 pima kilo 10 toka ktk huo mfuko zibaki kilo 11,then kutoka katika hizo kilo 11 pima tena kilo 10 zitoe ziweke pembeni.Then sukari iliyobaki ni kilo 1,
Chezea majibu yasiyo ya kuchagua wewe!!
 
Majibu yenu ni mathematically correct lakini hayako economical hasa hili la pili linaloweka mpaka kilo 21. Your manipulation doesn't need to carry more than 10 kgs.

A more economical approach is as follows:
1. Pima kilo kumi za sukari.
2. Toa jiwe la kilo kumi na uweke la kilo saba.
3. Kutoka kwenye kilo 10 ulizopima punguza mpaka ubalance kilo 7. Hapo utatoa kilo 3 na kubakiza 7
4. Chukua kilo 3 ulizotoa uziweke upande wa jiwe. Halafu toa kilo 4 toka kwenye zile 7 ili mzani ubalance.
5. Chukua kilo 4 ulizotoa na uziweke upande mmojawapo wa mzani baada ya kutoa kilo 3 toka kwenye upande huo. Hapo utakuwa na kilo 3 na kilo 4 kwenye mzani.
6. Punguza sukari toka kwenye mfuko wa kilo nne mpaka mzani ubalance. Utakayotoa ni kilo moja.
7. Mpe mteja kilo moja na usisahau kuchukua malipo yako na kurudisha chenji if necessary...
 
Hapa unatakiwa upime kilo saba saba tatu,zitakua kilo 21,punguza kilo kumi kwa jiwe la kilo 10 itabaki kilo 11 tumia tena jiwe la kilo kumi,kupunguza kilo 10 itabaki kilo 1!!
 
Kuna kajimtihani kadogo,umeenda dukani kununua sukari kilo 1 lakini kwa bahati mbaya mwenye duka hana jiwe la kilo moja lakini ana jiwe la kilo 10 na la kilo 7.Swali atafanyaje ili aweze kukupimia hiyo kilo moja ya sukari kwa kutumia mawe hayo mawili!

si ninaenda duka lingine..kwani lazima kununua kwake??
 
Pima kg 7x3 kupata kilo 21.Halafu pima kg 10x2 kupata kilo 20.Weka kg 20 upande m1 na kg 21 upande mwingine.Punguza sukari upande wa kg 21 hadi mzani ubalance,kiasi ulichopunguza ndo kilo 1 (21=20+x: x=1).
 
mi ntachukua Kilo 7 na kugawa kwa kila mteja ukizingatia huu ni mwezi Ramadhan yaani mwezi wa Taqwa...
So ntapata thawab...
 
mbona rahc tu!! pima kilo 7 mara tatu utapata 21kg then tumia jiwe la 10kg kuondoa 20kg itabak mojaaa!
 
mzani unaopima sukari hyo ni wa mabuchani. mizani ya madukani haiwezi kupima kilo zote hzo.
 
Wote njia ndefu. Fupi ni:
Tumia jiwe kilo 7 kupima sukari kilo 7 mara mbili changanya = mfuko wa kilo 14, halafu tumia mawe yote 10 na 7 upande mwingine balance na sukari = kilo 3. Sasa mfuko wa kilo 14 upande wa jiwe na jiwe la kilo 7 na la kilo 10 upande mwingine balance kwa kutumia mfuko kama wa kilo 14 kupata mfuko wa Sukari ya kilo 1.
 
Hii kwel bongo shemsha.......

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom