Chemba ya moyo?!?!?!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,252
2,000
Ndugu wanajamvi,

Kuna neno linanichanganya sana: CHEMBA YA MOYO au wengine wanaita CHEMBA CHA MOYO.

Hivi hii ni sehemu fulani ya moyo au ni eneo au kiungo ktk mwili wa binadamu? Au ni aina fulani ya ugonjwa?

Mara utasikia mganga wa mitishamba akijitangaza: 'ninatibu chemba ya/cha moyo'. Na leo nimesikia mtangazaji mmoja akiripoti kwamba kuna mtu 'amepigwa risasi kwenye chemba ya moyo'. Hapa ndipo amezidi kunichangnya kabisa.

Zamani nilidhani neno 'chemba ya moyo' limetoholewa kutoka kwenye kiingereza: 'heart chamber (any of the four chambers of the heart). Lakini, kwa mujibu wa matumizi ya neno hili, nimekuja kugundua kwamba hii siyo maana yake.

Wandugu, kama kuna mwenye ufahamu juu ya neno hili atujuze tafadhali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions
Thread starter Title Forum Replies Date
KENZY Shairi;moyo umeniweza Jukwaa la Lugha 2

Similar Discussions

Top Bottom