Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 309
Jana waziri katika ofisi ya rais (Bunge) aliwaambia watanzania (kupitia vyombo vya habari) kuwa mawaziri wa serikali watazunguka mikoani kueleza mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.
Maswali yangu kwao ni je nini manufaa ya ziara hizi kwa wananchi? Kama ni kuwaelezea si dhani kama ni muhimu kwa sababu mafanikio halisi hayahitaji kuelezewa yanaonekana kwa macho. Haya mafanikio ya kwenye makaratasi eti uchumi umekuwa, oo sijui nini, ni wizi mtupu.
Waswahili walisema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza... serikali ya jk inaenda kujitembeza tena na bila shaka watazomewa tena kwani fedha watakazotumia zingetumika kuimalisha miundombinu mtaani kwangu nisingehitaji mtu anielezee jinsi serikali ilivyofanikiwa, ningeona.....